Sishauri mtu kusoma PhD OUT


Kila siku nyuzi za kuichafua OUT zinaanzishwa, hii sasa nahizi ni vita kama zilivyo vita zingine.

OUT kwenye supervision wapo vizuri sana ukilinganisha na vyuo vingine, angalia graduates wake kitakwimu wengi wanamaliza ontime!!

Wewe bado huna ground ya kusoma PhD, ungeshajua hatua za kuchukua kuanzia unapopangiwa supervisor na kazi yako inapopokelewa!! Na OUT mtu kama wewe hutoboi, serious nakuambia utaishia kulalamika kwenye social media tu kama mtoto wa kidato cha pili!!

Kuna pande mbili zinakulinda kama mlaji, kwanza Mkurugenzi wa Post Graduate, ulimpa taarifa za usumbufu huo?? Au ulipotuma kazi yako nani alijua ili kuweza kumonitor mwenendo wa hiyo kazi yako??

Pili; Proposal yako imeenda faculty gani?? Kila facult ina departments ambazo zina coordinators wanaopaswa kujua wanafunzi wake wanakwenda vipi!! Umewasilisha malalamiko yako??

Umesema wa mikoani?? Umewasiliana na DRC au unahangaika na Supervisor peke yake??

Supervisor nao ni watu, wana tabia zao ushasema mkali haingiliki, wana matatizo na changamoto mbalimbali. Ujanja ni kutumia zaidi ofisi ya centre, sasa kama ulijua zile ni mapambo rudi nyuma, anza upya. Usipotoboa nipo paleeee....!!
 

Mkuu Bora wewe ungekuwa supervisor wangu.
 
Halafu wanapenda rushwa sana. Ukiwapa chochote kitu supervisor anasoma chap. Yaani ni balaa. Mimi nilitaka kusoma PhD OUT nikashtika baada ya kuona jamaa yangu anvyosumbuliwa.

Wanasimbua Sana mkuu. Halafu wao wanataka ulipe ada kwanza halafu Huduma mbovu.
 

Usipende kuropoka jambo usilolijua. Kama Jambo halikugusi kaa kimya. Sipendi uchawa kwenye mambo serious. Naomba uache mizaha. Au unataka niweke wazi kila kitu ndio ujue jinsi OUT walivyo wazembe na wasiojua majukumu yao.

Nikuulize swali wewe mjuaji, unamfahamu mdada anaitwa Evelyn Shipela? Yupo pale DPGS? Nimeanza na huyo mdada asiyekuwa na haya aliyefanya chuo Cha baba yake. Ukitaka wengine nitakutajia mmoja baada ya mwingine.
 
Walijua hawezi kutoboa tena UDSM,,angalia hata gpa za open zilivyokuwa kubwa
Wewe unaonekana bado una utoto mwingi nenda kasome
hapo OUT ndio uje useme, UDSM ugumu upi na ni spoonfeeding tuu pale.

Ingekuwa ni rahisi hivyo wasingekuja kulalamika huku. UDSM ni extended high school
walianza miaka sawa na University of Nairobi na Makerere University. Je hiyo UDSM
ipo kwenye rank gani Afrika?

Je Mzumbe nacho kina credentials gani ya kukusifia si kama tu sekondari pale.
 
Kwa PhD mkuu ni shida. Maana supervisor anatokea Makao Makuu Biafra
Mkuu lakini Master's by Thesis na PhD supervisors ni wawili sasa wewe

mbona unazungumzia supervisor mmoja je huyo mwingine umeshaongea
nae, mchango wake ni upi?
 
Asante kwa maelezo.mazuri
 

Kama Evelyn tu kakushinda basi tatizo siyo OUT wewe ndiyo kilaza waheeeed, jiangalie tena!!

Rudi nyuma anza upya kimkakati!

PhD siyo matako kwamba kila mtu lazima awe nayo!!! Frankly speaking, huna akili ya PhD wewe, nenda UD utarudi na thread ya malalamiko tena hapa!!
 
Dadeki kumbe nimeingia cha kike, leo ndio nimemaliza kufanya application nataka nisome post graduate
View attachment 3277499

OUT unatoboa ila usitake kusoma kama conventional utaumia!! Huku unajipambania, cheza na network kuanzia kituo chako mpaka ngazi za juu!!

I mean unapofanya kazi jua anayepaswa kuisimamia mfano research kuna coordinator, Faculty Deans na kuna idara rasmi ya PostGraduate inayosimamia.

Kama ni mitihani kuna exams coordinators, easy sana kukusaidia!

Cheza na simu tu wala haihitajiki rushwa wala takrima, wenzio tumetoboa kiulaini sana!! Niamini
 
Kwa mfumo wa elimu wa vyuo vyetu Tanzania nadhani tungeishia tu kwenye bachelor degree then post- graduate programs watu waende kusoma nje ya nchi. Kwa kifupi vyuo vyetu haviko tayari bado kuhandle post graduate studies au programs zinazohusisha research. Factors ziko nyingi sana lakini ikiwamo uwezo binafsi wa hawa lecturers, kuna issues za motivation zinaingia hapa, taasisi zetu za elimu ya juu zinadedicate nguvu nyingi kwenye undergraduate programs zaidi kuliko hizo postgraduate programs, lakini pia teaching load kwa undergraduate programs ni kubwa kwa lecturers kiasi kwamba wanakosa muda wa kudeal na post graduates, imani ya kwamba elimu ya post graduate sio ya lazima na inahitaji efforts binafsi za mwanafunzi nayo ni factor nyingine. Kubwa zaidi kiutaratibu academic level inayohusisha research ina complications nyingi sana ambazo zinahitaji facilities nyingi sana ili kuweza ku accomplish objectives ikiwamo pesa (funding). Kiutaratibu kila hatua ambayo mwanafunzi anapiga kwenye usomaji wake lazima kuwe na uhusika wa moja kwa moja wa supervisor. Sasa wewe unandaa proposal peke yako supervisor hana habari, unatengeneza research design supervisor hahusiki, unaenda field kukusanya data supervisor katulia tu hiyo shule haiwezi kuisha vizuri that's why in most cases siziamini sana PhD zinazotolewa bongo maana supervisors hawafanyi kazi yao ipasavyo na huwezi kuwalaumu maana hizo kazi lazima alipwe vizuri kila hatua ili aweze kushiriki kikamilifu na vyuo haviwabani sana maana vinajua kuna sehemu havitimizi wajibu wake vizuri kwenye kuandaa mazingira mazuri ya supervisor kufanya kazi na mwanafunzi. Nje kila kitu kiko well organized na post graduate studies zote ziko well funded, supervisor anaachaje kufanya kazi maana hata kwake inampa credit. Kwa research degrees nashauri mtu aende tu nje kwasababu pia time frame zao ziko standard, kama PhD ni miaka 3,4 au 5 chuo na supervisor watahakikisha unamaliza ndani ya muda huo sio huku kwetu mtu anafanya PhD 7 years na bado hiyo PhD haina tija yoyote kwa mwanafunzi na taifa kwa ujumla. Naomba kuwasilisha 🙏
 
Mkuu lakini Master's by Thesis na PhD supervisors ni wawili sasa wewe

mbona unazungumzia supervisor mmoja je huyo mwingine umeshaongea
nae, mchango wake ni upi?

Kwenye PhD thesis huyo mkubwa ndio kila kitu. Huyo wa pili ni junior. Huyo Junior alishasahisha kazi yangu ila mkubwa Hana muda.
 

We kweli ndio sababu ya uzembe na ujinha wa OUT. Kumbe tunashindana. Unataka nishindane na secretary?. Yani kunipangia supervisor unataka nishindane na mtu. Sina huo muda wa kushindana na mtu, Kama wanaona kunipangia supervisor ni shida basi nitaenda UDSM na nitamaliza ndani ya muda.

Ila nikuambie ukweli wewe mjinga ni kwamba chuo chenu ni sekondari, na Wala sitaki kukisikia Tena.
 
Umeeleza vizuri lakini sehemu kama nimekuelewa vizuri kwa uelewa wangu inahusu vyuo zaidi ku fund hao supervisors vizuri hayo ni yao chuo
Sio ya Mwana Chuo sababu yeye ada yake analipa yote

Kwa nini mwanachuo aumie kwa sababu ya mambo ya internal faculty wasio fund vizuri supervisors?

Kwa nini mwana Chuo awe mbuzi wa kafara ? Supervisors kuhamishia hasira zao na frustrations zao kwa mwanachuo kwa kutompa ushirikiano badala ya wao kuzodoana na kufokeana huko ndani vikaoni internally kwenye vikao mambo yakae sawa kwenye funding za supervisors?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…