Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL


Ukimaliza utaniambia ' Fungulu Ngenge ' Wewe.
 
Inasikitisha sana...

Vitu vya serikali na viheshimiwe jamani... hizo ndege zilikuwepo kwa ajili ya waliyopita na zinatakiwa ziendelee kuwepo kwa ajili ya atakayokuja...

Tusipoangalia tutaanza kupangisha mpaka jumba jeupe...


Cc: mahondaw
Vitu havitumiki na havizalishi..... Vibaki vya nini??
Huyo anaekuja akija anunue fresh Aeroplane sio vindege vyenye laana ya milele.
Heko JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na Mheshimiwa Raisi kwa asilimia kubwa, serikali ina ndege tatu za raisi, yeye katoa ndege mbili zitumike commercially badala ya kupaki tu bila kufanya kazi. Lakini pia, hata zikiwa branded 'ATCL' bado viongozi wa serikali wanaweza kuzitumia kwa safari zao.

Mleta mada hujaweka hasara za kiuchumi ambazo serikali itapata zaidi ya kuweka "social prestige" kwa taifa. Hatuangalii fahari kuwa raisi anatembea na ndege yake, tunapigana kutoka kiuchumi.
 
Uhai wa ndege ni kuwa hewani ikiwa imepaki inakufa mapema ni sawa na gari, ukiipaki mwaka 1 hadi 2 inapata dents na kisha inakatika na kuwa screper. Raisi yuko sahihi 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app

Rais yuko sahihi kuzibadili Ndege za Rais kuwa za Biashara au? Sijakuelewa hapa naomba uitetee Hoja yako tafadhali.
 

Acha Kudanganya na rudi tena ukamsikilize alichokisema tafadhali. Hakusema kuwa Ndege moja itabaki na zile mbili ndiyo zibebe Abiria bali alisema ni Ndege zote. Siku zingine kama huna uhakika na Kitu au labda hujasikia vizuri Mtu kasema nini jiridhishe Kwanza kuliko kuwahi kuja ' Kupopomika ' hapa Jamvini sawa?
 
Nimesikia akisema Fokker-28 na Fokker-50 zipakwe rangi za ATCL zianze kubeba abiria, wewe ulisikia vipi mkuu?
 
Leo umeandika upumbavu wa hali ya juu.
Bila shaka siku mwenge ukipigwa ban mtakuja kulialia hapa japo mnapiga kelele kwamba hauna umuhimu.
Narudia tena umeandika UPUMBAVU MKUBWA.

Wenzako tumerithishwa Akili nyingi Wewe umerithishwa Utahaira uliotukuka. Pole sana!
 
Ni bwege sana huyu Genta, nilidhani ana hoja kubwa na mbadala kumbe eti moja iuzwe. Hopeless kabisa!

Sikumbuki ni lini umewahi Kuandika au Kuchangia ' something constructive ' hapa Jamvini sana sana mara nyingi huwa unatudhihirishia tu ulivyo ' Fungulu Ngenge ' wa Kutukuka kabisa.
 
Huyo mtanzania atayepanda hzo Fokker ni bwege wa mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ukikata ticket unaona na aina ya ndege utakayo panda. Halafu hiyo fokker inatatizo gani mbona maraisi na matajiri wengi wanazimiliki na kuzitumia nakumbaka ata bombadier zilitoka kauli kama hizi. Raisi wetu anaweza kuwa na mapungufu ila siyo kila atalolifanya tuliseme vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia akisema Fokker-28 na Fokker-50 zipakwe rangi za ATCL zianze kubeba abiria, wewe ulisikia vipi mkuu?

Labda nikuulize Kwanza unavyojua Wewe Ndege za Rais nchini zipo ngapi? Na unadhani alipokuwa anatetea Hoja yake kwa kusema kuwa Kwanza Yeye hasafiri mara kwa mara hivyo zote zipakwe tu rangi kama hizo zingine alikuwa anamaanisha nini? Kuna Watu ni ' Mafulu Ngenge ' chini ya Mbingu hii hadi mnaboa!
 
Nilikuwa nakuona Kama mtu ambae unafanya research kabla ya kuongea lakini Leo umenisikitisha Sana,unajua raisi wa China na viongozi wa juu wanatumia ndege gani?jibu ni kuwa raisi and Co wanatumia Air China ni ndege mbili zimeteuliwa kutoka air china,raisi wa china anapotaka kusafiri ndege anaitumia Kama hasafiri basi ndege zinabeba abiria,ni BOEING 747,sasa wewe Fokker tu hizi unapiga mayowe du? Mimi kwa maamuzi haya Nampa magufuli heko 100% na ikiwezekana zote tatu za raisi ziwe za biashara,siku wakiwa na safari yy na makamu wake basi wazitumie na Kama hawasafiri basi biashara as usual,amenikosha Sana Leo mh raisi japo ni mpinzani wa ccm na watu wake,viva Mr.prezdaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uingereza, wote wanasafiri na british airways, na ni developed nation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angegawa viwanja vya mpira vinavyomilikuliwa na ccm virudi serekalini ningemuunga mkono!
Au jamaa anataka kutawala maisha yake yote kiasi anawaza labda mpaka ifike 2035 zitakua hazifai tena kwa matumizi!
All in all zile ni mali za serekali na zenunuliwa kwa matumizi maalumu so ziheshimiwe!
 
Nimesikia akisema Fokker-28 na Fokker-50 zipakwe rangi za ATCL zianze kubeba abiria, wewe ulisikia vipi mkuu?
Nimemaliza kumsikiliza vizuri tena, amesema ndege 2 ndiyo ameishatoa maelekezo zipakwe rangi na zitumike kubeba abiria endapo kutakuwa na upungufu....nadhani ninemuelewa vizuri. Ki ufupi, ndege moja itabaki kwa matumizi ya raisi na serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…