Sirudi tena Jukwaa la Siasa

Yaani bora mtu upigwe ban usiingie kabisa JF kuliko kuzuiwa ku comment. Inauma sana. Yaani ni sawa na ulale na mkeo kitanda kimoja wote mkiwa watupu halafu akunyime tunda. Pole sana Bujibuji

Hiyo adhabu nimeshaichezea sana...
 
Last edited by a moderator:
jina lako linakusaidia

Jina langu linanisaidiaje mkuu Sista? Kuna member mwingine jana kaninanga eti mimi mchawi kwa kuwa nilimkosoa mzee wa upako na yale mapicha ya freemason. Basi kaniambia eti kwa avator yangu na mimi lazima ni mchawi. Nikamwambia mimi ID yangu ni Bundimkubwa na nimeweka picha ya Bundimkubwa. !!! Ha ha ha!!
 
Huyu si alikuwa anatafutwa na Mangi amfumue ubongo baada ya kumfumania?
 
mie siogopagi na saa nyingine huwa nachokoza tu makusudi nione watasemaje
Heaven kumbe ukija kule unatufanyiaga makusudi eee..haya banah ila ukija kule next time ujipange
Kule tunae washawasha na excel wanatuvurugaaaa! hawajui kuwa mwaka mzima wa jf miezi mitatu tumelazimika kwenda likizo kwa ajili ya watu kama hao..!!
 
Bujibuji nilikupa hiyo taarifa mapema kuwa kule kuna wenyewe, haya umekula ban umetuacha tunaendelea kuwapiga juu na chini mizigo. pole yako kule uwe unakuja kuchungulia unasepa, siasani hakuna like kule, kule ni unatupa jiwe gizani ukisikia yale limempata mlengwa, ila hata mm 2010 nlikula ban ya siku 30 na ndio ikawa ya mwisho ila kuna siku mwekundu alitaka kunisababishia ban. pole na karibu tena ban grocery usiogope sana😛anda:😛anda:😛anda:
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mara ya kwanza kuingia jukwaa la siasa Ritz alinifanya nikaigwa ban la siku 30...Ila kuna watu wanakera kama akina lizabon,mingoi,simiyu yetu,Lukosi na wengine wengi dah yan kero tupu ila tunakomaa nao tu!

Aisee sure vile vijamaaa vinaboa.... Ila mimi nmeshavijulia huwa nawapa za USO live kuna style yake usije kichwa kichwa maana Samuel Luhanga kaajiri vijana maaalumu wakuharibu jukwaa wanaitwa Lumumba buku7 FC.
 
nina hakika hapa JF me ndo naongoza kwa vifungo ndo maana kule nachungulia tu
 
Shosti na wewe unaninyatia mpaka chooni? khaaaaa nilikuwa kijijini kwa siku tatu, kuuguza wazazi treni imeharibika ndio maana nimechelewa Heaven on Earth

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…