Sirro: Marufuku bodaboda baada ya saa 6 usiku

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Kamanda wa polisi mkoa wa Dar Simon Sirro amepiga marufuku boda boda kufanya kazi baada ya saa 6 usiku kutokana na sababu za kiusalama

 
Usalama kwa Watanzania ni kipaumbele nambari moja. Safi sana.
kwa hiyo watu watembee kwa mguu! maana hapa Dar saa saba usiku wapo wanaorudi makazini na wale wanaoenda mfano machinjioni kuchukua nyama za supu na kuuza kesho yake, Hamuoni mtakuwa mmewapa wakati mgumu watu kama hawa. We kujibu ndio bila kubalance, hii haitazuia uharifu, sana sana itaongeza rushwa mana sasa polisi watazunguka mitaani kuwabugudhi bodaboda wawape chochote au kuwakamata.
Serikali iwekezekwa polisi kukabiliana na changamoto hii na wala sio kuwazuia bodaboda usiku, wanatusaidia sana sie wa mtaani tusikabwe ovyo. Hapa kipaumbele unachosema hakizingatiwa
 
hawa watu wanaorudishwa nyumbani na magari hawajui watu wanachelewa kwenye mipango yao na wanategemea kurudishwa nyumbani kwa pikipiki.....ila hii iko poa sana sasa itawagusa raia wengi maana ile ya kutokwenda mjini ilikuwa inawahusu wachache sasa hii ya kulala mapema bodaboda iko poa maana boda watapiga hela ukimpigia au kukutananae kijiweni usiku ujue nauli itakuwa mara mbili ya kawaida.......
 
Nachshsngaa ni haya maamuz ya viongoz wa serikal wanayoyafanya bila kufikiria athar zake kiuchumi. Sasa ukisema mwisho saa 6 boda boda, bado mwingine alishakataza shughuli za bar ziwe mwisho saa 6 usiku. Mara kuna kufanya usafi jmoc so biashara zote zinasimama kwa masaa yaliyopendekezwa. Hiv hawajui kuwa ni sh ngap taifa linapata hasara kwa kusimamisha hzo shughul za kiuchumi?sasahv ajira zimesimamishwaa kwa zaid ya mwaka huku fursa za kujiajue zikiwa finyu kwa ajil ya kodi kuwa kubwa ambapo inasababishwaa biashara nyingi kufungwa. Hii ndo tanzania ya viwanda kwel? Na hivi ndo uchumi wetu utakuwa kwa kubanwa na kodi na muda wakutenda kaz(mwisho saa 6) kwel?
 
Back
Top Bottom