Sirikali Ipunguze Kupiga Chafya!

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Sirikali ya sasa haijambo kwa kutoa matamko, mkuu wa kaya siku za kwanza kabisa ghafla akatokezea pale hazina. Akatoa matamko fulani pale. Akazuka tena BOT akatoa matamko,"Hapa wapo wafanyakazi hewa!" Kisha, akatoka kiranja mkuu wa sirikali huko bandari. Ikawa mshike mshike huko. Mara tamko likatoka. Miongoni mwa wakwepesha kodi hata huyu fulani, mfanyibiashara mkuu yumo. Kakwepesha mabilioni. Sasa, ukitulia ukaangalia utaona kama matamko yanafyatuka tu.

Sirikali iache KUKURUPUKA na kutoa matamko kama vile inapiga CHAFYA. Kwa maana humo humo sirikalini utawasikia wamekazana kuboresha hayo matamko yao kama chafya. "Oh! Unajua ule ulikuwa utani tu. Mkome msiwafyatue!" Mara naye mwangalizi mkuu BOT. "Ah! Hapa kwetu, hao hewa hawapo!"

Basi tena, mkuu wa kaya kaja, "Oh! Bwana huyu, mfanyibiashara huyu ni hodari tena safi kabisa. Analipa kodi zake zote. Hadaiwi huyu! Msaidieni na mengine ayatakayo!"

Kama haitoshi, matamko hayaishi,yanakurupushwa kama chafya. Bosi mmoja kasimama, Hatuna dawa mote humu godauni. Dawa zimeisha. Mara kajibiwa na kiranja mhusika, "Dawa nyingi zipo. Tena na mifweza imetoka kununua na madawa mengine."

Matamko mithili ya chafya, zinapigwa kila kona na yeyote mwenye mamlaka fulani. Huko wilayani katokezea governor mmoja naye kapiga chafya lake, "Tchaaaaaa! Tia ndani huyo, msweke rupango akome! Nani kamwambia huyo mwandishi huku kuna shida ya maji!" Akaendelea kubwabwaja, " Anataka kuchonganisha sirikali na wananchi wake. Huku hakuna kiu ya maji wala tembo!"

Mara sauti ikasikika toka huko afisi ya kiranja wa sirikali yote," Nataka nione sanda, jeneza na kaburi!" Huyo faru joni namtaka miye. Basi jibu likaja,"Wee bw.kiranja. Huku hakuna sanda, hakuna jeneza wala kaburi!" Akafafanuliwa eti huko mbugani seremala hawako wa kuchonga jeneza wala muuza sana wala mchimba kaburi. Huko wako "Scavangers" mfano, fisi, tumbusi, tai na wengineo. Hivyo kila mzoga hata uwe wa faru joni huzikwa ndani ya matumbo ya scavangers hao, kuanzia ukucha hadi mfupa wa mzoga. Hawabakizi kitu hao!

Chafya jengine ni hili. Masodaa waibuka, "Hao maiti wa huo mto mnaokunywa maji yake. Waliharibika, hawatambulikani, wananuka uvundo pyuuu!" Kwa hiyo? akaendelea yule sodaa, "Wananchi wakawazika basi, kwisha habari yao!"
Baadaye kelele zikawa zimezidi. Hatimaye mkuu kabisa wa juu wa masodaa kaibuka, " Eh...ee...Enh! Mnajua qwale maiti ni watoka huko nchi za nje. Tumechukua sampuli tuwajue. Wananchi tulieni tutajua tu!"

Kwa jumla inachosha, kaka miye nionavyo, watendaji wa mteule wetu wamemgeuza mkuu wa kaya "deal". Siku alipowateuwa wakamsoma, wakamwangaliaaa, wakajua huyu ni wa mwendo wa chafya. Basi wote wamegeuka wapiga chafya kwa kwenda mbele. Chafya imekuwa dili ya kubaki umeteuliwa vinginevyo wanahisi watatumbuliwa.
 
Back
Top Bottom