Serikali ya awamu ya sasa inaongoza kwa kutoa matamko. Kwa mara ya kwanza, mkuu alienda pale Hazina akaacha matamko, mara ya pili akaenda BOT akaacha matamko, wafanyakazi hewa hapa wapo. Baada ya hapo, kila kiongozi ndani ya serikali kuanzia mtendaji wa mtaa hadi kiranja mkuu wa serikali imekuwa ni matamko, matamko, matamko...
Bahati mbaya wakati mwingine matamko hayo yamekuwa ya KUKURUPUKA kama kupiga CHAFYA! Popote pale utasikia, "Tchaaaaaa!!!". Chafya hilo! Kesho ataibuka mwingine, "Oh! Ule ulikuwa ni utani tu. Msiwafyatue..." Naye msimamizi mkuu wa BOT akatokezea siku nyingine," Oh! Hapa hao hewa hawapo!"
Siku nyingine tena, zamu ya kiranja mkuu,"... huyu mfanyi biashara kwenye TID yake kakwepesha kodi mabilioni." Miezi kadha baadaye, mkuu wa nyumba kasimama, "Huyu baba huyu, analipa kodi, ni mwaminifu. Mpeni nafasi!"
Mkuu mmoja huko wilayani kazuia waandishi wasitangaze baa la njaa wilayani mwake. Hataki matamko huyo. Mwenziwe mmoja kamseka ndani mwandishi. Eti, kisa! Karipoti wanavijiji wanagombea maji, wanakiu! Mkuu huyo, kapatwa na chafya kla ghafla, " Tia ndani huyo! Nani kamwambia maji watu wanagombea huku. Huyo mchochezi, Asitoke!"
Basi sasa, kila uchao kila kona, matamko...matamko...matamko! Mimi nionavyo, watendaji washamgeuza mwenye nyumba "deal". Ukitaka ubaki humu uongozini basi, shekhe cheza ngoma ya mwenye mji; usije anzisha nyengine. Hana masihara huyo, ohoo...atakutimua! Mkuu kageuka dili.