Siri za wanaume zinazowakera wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri za wanaume zinazowakera wanawake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 22, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa kawaida wanaume na wanawake wanazo tofauti za kimaumbile. Kuna wakati tofauti hizi huweza kusababisha ufa kwenye uhusiano na hata kuangusha kabisa ndoa. Leo nimeona ni vyema kwa wanawake kujua baadhi ya tofauti hizo ili ziwasaidie kuimarisha mahusiano yenu au ndoa zenu:

  1. Mwanaume huwa hataki kuambiwa jambo wakati anafanya mambo yafuatayo. Wakati anaangalia mpira kwenye TV ambapo timu yake inacheza, wakati anakula, wakati ndio kwanza tu ametoka kwenye shughuli zake ameingia nyumbani na wakati anasoma kitu iwe ni gazeti, kitabu au taarifa yoyote. Kama mwanamke asipofahamu jambo hilo anaweza kushangazwa na mumewe kwani atakuwa anamsikiliza nusunusu, kwa hiyo mawasiliano yatakuwa hayajakamilika. Wakati mwingine mwanamke anaweza kugundua udhaifu huo na hivyo kutaka kujaribu kulazimisha kusikilizwa kwa makini, hilo ni kosa kubwa sana na linaweza kusababisha mtafaruku ndani ya nyumba.

  2. Mwanaume huwa hapendi kumfanya mkewe ajue kwamba, anaangalia wanawake wengine. Kwa hiyo anachofanya ni kuvunja shingo kwa namna ambayo hatabainika. Lakini ukweli ambao wanawake hawaujui, ni kuwa wanaume kimaumbile ni watu wanaovutwa na kuchochewa na vitu vyenye kuonekana kuliko kusikia au kunusika. Mwanamke kujaribu kumzuia mumewe asiwe anavunjia shingo wanawake wengine ni kama vile kumwambia afanye hivyo. Mwanaume kuvunja kwake shingo hakuna maana ya mwanaume huyo kutoka au kutaka kutoka nje ya ndoa.

  3. Wanaume huwa wanapenda muda wao wa faragha. Mume anaweza akajikuta tu, anakwenda kutembea mahali, na kurudi akiwa amechelewa kidogo. Kama akimwambia mkewe alikuwa mahali fulani au kwa jamaa fulani, mke hana haja ya kuanza kuuliza na kubabaika hovyo. Bila kumpa mwanaume faragha, anaweza kuingia mahali akachukia nyumba yake na vyote vilivyomo. Lakini hata mwanamke anahitaji faragha pia.

  4. Wanaume huwa wanafanya mambo wanayoombwa na wake zao kwa hatua ambazo wakati mwingine zinaonekana kuwa za polepole sana. Mwanaume anaweza kuombwa na mkewe afanye jambo au kitu fulani na akakubali, lakini ikachukua karne kutekeleza. Mke hana haja ya kuzira au kukasirika kwa sababu, mwanaume hufanya mambo kwa kasi na hatua zake mwenyewe. Mwanaume huchukulia mambo na muda, tofauti na mwanamke anavyochukulia. Kuna mambo ambayo kwake hayana haraka na wala siyo ya kuumiza kichwa.

  5. Usidanganywe, wanaume wanapenda sana umbea. Kama mume akimsikia mkewe anazungumza umbea, labda kwenye simu anaweza kutikisa kchwa kupinga au kudharau jambo hilo. Lakini mwanaume anapoanza kuelezea habari za watu wengine na kuungwa mkono na mkewe, umbea huo humfurahisha sana. Ukweli ni kwamba wanaume hupenda sana umbea, sema tu wameupa jina lingine, labda wanaweza kusema ni kumjadili mtu. Kwa hiyo mwanamke anapaswa kujua ni umbea upi unaomvutia mwanaume.

  6. Mwanaume anapojibu swali kwa kuuliza swali au anapojibu swali kwa sauti ya juu, mwanamke anapaswa kujua kwamba, mwanaume huyo anajaribu tutafuta uongo wa kusema. Kwa mfano, anaweza kuulizwa na mkewe. ‘weekend hii unatarajia kufaya shughuli gani?' Akijibu kwa kuruda swali, ‘Ninatarajia kufanya shughuli gani?' Basi, jua hapo anatafuta kusema uongo, inabidi mwanamke awe makini. Lakini haina maana kwamba, uongo huo una maana ya yeye kutaka kufanya jambo baya au kutaka kutoka nje, hapana, siyo lazima. Lakini jambo la kujua ni kwamba, anajaribu kutafuta uongo.

  7. Kuna wakati wanawake hubabaika sana wanapoona waume zao wamekaa kinyonge sana. Hukimbilia kuwauliza, ‘vipi mbona leo uko hivyo?' Mwanaume anapoulizwa hivyo anaweza kujibu, ‘hapana, hamna kitu, nawaza tu.' Mara nyingi wanawake hawaridhishwi na jibu hilo. Kwa kutoridhishwa, huendelea kuwabana waume zao na kuwafikisha mahali ambapo watawakera. Inabidi mwanamke kujua kwamba, mwanaume pia hutafakari na kuna wakati kutafakari huko huenda kwa kina sana kiasi cha kumfanya kama amekereka. Akishasema, ‘hamna kitu,' inabidi mwanamke aelewe tu. Anaweza kutafuta muda mwingine ambapo anaona mume huyo anaweza kuwa tayari kuzungumza………………

  Nisiwachoshe, nitaendelea kuwaletea siri za wanaume zinazowakera wanawake kwa kadiri muda utakavyoruhusu.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Vingi ya hivi vitu sioni kwanini viwe kero kwa wanawake...

  Namba 1 kwa mfano...iweje anaesumbua ndo aone kero??
  Ni ngumu kiasi gani mtu kuelewa kwamba mwenzake (mume au mke) akiwa anafanya kitu basi anastahili kupewa utulivu amalize anachofanya kabla ya kuingizwa kwenye maongezi/shughuli nyingine zinazoweza kuvuruga kile anachofanya???

  Namba 2...we all look.
  After all..macho hayana pazia. Kinachofanyika baada ya kuona ndo kinachotakiwa kuwa kero.

  Namba 3...kila mtu anastahili muda wa peke yake hata kama ni dakika 10 kwa siku. Sioni kwanini mtu akereke na mwenzake eti kisa anataka kutumia muda kidogo bila yeye...mtafuatana kila mahali mmekua kumbikumbi???

  Namba 4 Hiyo kweli yaweza kuwa kero...muhimu ni kumuelewa tu mtu wako huyo.
  Ukishajua speed yake ya kufanya mambo unamwomba asaidie kitu muda mrefu kabla ya wewe kukihitaji kiwe tayari.

  Namba 5 hehehheh...if we didn't talk about/of other people we would run out of things to talk about.Au labda sijui umbea unapoanzia na unapoishia...maana siwezi hadithia nilichofanya shuleni leo bila kumtaja mtu/watu wengine waliokuwepo.

  Namba 6 ..hehhe..nimejikuta nafikiria kama na mimi hua nafanya hivyo.
  Neway sitaki kukubali kwamba mtu akifanya hivyo lazima jibu atakalotoa liwe la uongo...inawezekana akawa anafikiria kwasababu hata yeye mwenyewe alikua hajui.

  Namba 7 I like...maswali mengi baana ya ''hamna kitu bwana '' hua yanakera!!

  Asante Mtambuzi kwa thread nzuri...hopefully watu watajifunza waache kukereka hovyo kama wapo wafanyao hivyo.
   
 3. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii makala ndefu ntairudia kabla sijaposti.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kuna mchekeshaji mmoja alisema kuwa kila mwanamke anakuwa na mwanamke mwenzake ambaye anamchukia kazini kwake.

  Akirudi kazini inabidi umsikilize tu hata kama hutaki na majibu yako yawe. Yes dear..I know.. she is crazy... didnt i tell you she is a bi... hata kama hum sapoti
   
 5. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu cha kujifunza hapa.........Asante Mtambuzi
   
 6. MASELE

  MASELE JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  makala nzuri
   
 7. M

  MyTz JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nashukuru kwa post yako Mtambuzi
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Asneti kwa kusaidi kuelewesha ulimwengu wa pili......... !!!
   
 9. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  number 2 na 4 zinaongoza sana kwa kukeraaa...

  number tano ni kiboko yaan wanaume ni wammbeya kuliko aisee tena umbeya wa mwanaume unaaminika sana yaan usiombe mwanaume akufanyie umbeya looooh.....hili mnaboa sana watoto wa kiume
   
 10. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante sana mpendwa, kuna kitu nimejifunza
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kitu gani?
   
 12. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,639
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Ebwanae watu mnafikiria nimekubali
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,509
  Trophy Points: 280
  asante mkuu, japo upande wenu umejipendelea sana ila nimejibu haya tu kwa leo:

  1. Hii inaonyesha kuwa una mapenzi na hivyo vitu kuliko mkeo, je mama akifanya hivyo wewe utajisikiaje.

  2. Kwa hiyo hata mimi mkeo nikivaa nakuacha manyonyo nje, au nikivaa kamini mapaja nje nje ina maana bado utavunja shingo tu.

  3. Hee hivi kwanini mnadeka hivyo, kumbe hampendi kuulizwa eeh, na mtaulizwa tu.
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu
  makala imetulia sana
   
 15. M

  Myn17 Senior Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shukran mkuu,
  kweli umesaidia ku2a mzgo nlikuwa nakerekwa sn na namba 7,kwa ujumla nimepata v2.
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Bado ziko nyingi, niendelee kuzimwaga humu..........................!?
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Lizzy labda nikuulize swali, hivi uliwahi kusoma kitabu kinachoitwa Men from the Mars and Women from Venus............? Sijui kama nimepatia hilo jina la kitabu, lakini naamini utakuwa umewahi kukisikia.
  Hicho kitabu kina mengi ya kujifunza juu ya tofauti zetu, kati ya wanaume na wanawake................
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  endelea mkuu maana hoja ni nzito haitakiwi uiache hewani
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  no 5, nakubaliana nawe. Wanaume ni wambeya vibaya mnooo. . !
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  I have heard of it ila sijapata kukisoma.

  Binafsi nakubaliana sana na uliyoandika maana yapo ila tu nashindwa kuelewa kwanini mengine yanaonekana kama kero wakati ni haki ambayo hata huyo anaeona ni kero bado nae anaitaka!!
   
Loading...