Siri za Uchunguzi wa Tukio la Dkt. Ulimboka zaanza Kuvuja

Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.

Nadharia hizo zinazozua utata wa hali ya juu, zinaonyesha na kutoa maelezo ya hatari, ambayo madaktari hawakubaliani nayo hata kidogo, ingawa wamekiri kuwa nao wameyasikia maelezo hayo waliyoyaita ya ‘kipuuzi’.

1. Nadharia ya kwanza inaelezwa kuwa Dk. Ulimboka alipigwa na madaktari wenzake wanaoamini kuwa alikuwa ‘amepotea njia’ na kuanza kuwauza kwa Serikali na taasisi zinazotoa fedha kufanikisha mgomo huo, “Kuna viashiria kuwa alikuwa anachukua fedha kutoka kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na chama fulani, ambao lengo lao ni kutaka vurugu ziendelee kuwapo na nchi isitawalike.

Lakini kilichotokea wanasema zile fedha alizokuwa anapewa alikuwa anawapiga panga njiani, hivyo wenzake wakaona wamshughulikie,” kilisema chanzo chetu kwa siri kubwa.

2. Nadharia nyingine ni ikle inayoelezwa kuwa wapo wagonjwa waliofiwa na ndugu yao mbele ya Dkt. Ulimboka hapo Muhimbili, na waliahidi kulipiza kisasi, hivyo hii nayo inafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kubaini ukweli wake.

3. Nadharia ya tatu na ya mwisho ni ile iliyogusiwa hadi bungeni na wabunge wa CCM - akina Mwigulu Nchemba na Injinia Stella Manyanya - kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahusika na utekaji wa Dk. Ulimboka kwa nia ya kuwafanya wananchi waichukie Serikali.

CHADEMA kupitia Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, John Mnyika, imekanusha mara moja na vikali kuhusika na unyama huu, na baada ya kubainika kuwa hoja hii ingeleta machafuko katika ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge Anne Makinda ameamua kuipiga marufuku isizungumzwe bungeni.

Dkt. Ulimboka, ambaye si mwajiriwa wa Serikali, anadaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Juni 26, mwaka huu Dar es Salaam. Baada ya kupigwa na kujeruhiwa, inadaiwa kwamba alitelekezwa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni jijini humo.

• Wakati utata wa tukio hilo ukiendelea kutanda, kumekuwa na taarifa nyingi, lakini zinazotajwa zaidi ni ile ya kwamba Dk. Ulimboka alifanyiwa kitendo hicho na marafiki zake wa karibu. Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya usalama zimedokeza kuwa chanzo cha kadhia hiyo ni kujitokeza kwa mgongano wa maslahi kati yake na wenzake.

• Inaelezwa kwamba wenzake hawakufurahishwa na matumizi ya fedha na misaada mingine iliyokuwa ikitolewa na asasi zisizo za kiserikali, ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mgomo wa madaktari nchini, “Jambo hili hatujalithibitisha moja kwa moja, lakini tumepata taarifa kuwa baadhi ya rafiki zake ndiyo walioshiriki kumteka kwa sababu za kimaslahi.

Tunaendelea kuchunguza kujua ni maslahi gani ingawa kuna taarifa zinazodai kwamba wenzake walianza kumtilia shaka juu ya mwenendo wake na dhima aliyopewa ya kuwatetea madaktari. “Inasemekana walianza kumtilia shaka kwa ukwasi alioupata ndani ya kipindi kifupi, wenzake wakawa na imani kuwa huenda anajinufaisha na uenyekiti,” kimesema chanzo kingine.

• Kuna madai mengine kwamba tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dkt. Ulimboka lilitokana na ndugu wa mgonjwa mmoja aliyefariki dunia kwa kukosa matibabu, bado nayo ni ya kutia shaka kubwa. Hata hivyo, daktari huyo hakuwa mwajiriwa wa serikali, ingawa inadaiwa kuwa kwa nyakati kadhaa alikuwa amepewa nafasi ya kuwahudumia wagonjwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI).

Mmoja wa wafanyakazi wa MOI aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina amesema; “Kuna ndugu walikasirika baada ya mgonjwa wao kufariki dunia. Hawakufurahishwa na majibu waliyopewa na mmoja wa madaktari (Ulimboka). Walionekana kuchukia. Siku chache baadaye ndipo ukatokea huo utekaji. Baadhi yetu tumelihusisha na kifo cha yule mgonjwa.”

Dkt. Ulimboka kwa sasa anatibiwa nje ya nchi. Taarifa za awali zilisema alipelekwa Afrika Kusini, ingawa kumekuwapo na taarifa nyingine kwamba anatibiwa katika moja ya nchi barani Ulaya.

Madaktari wenzake walikataa msaada wa Serikali wa kumpeleka nchini India kwa matibabu, jambo ambalo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamaja, amenukuliwa akisema limeisikitisha Wizara na Serikali kwa jumla.

Pamoja na kukataa ofa ya matibabu, madaktari hao walizuia viongozi wa Serikali kwenda kumjulia hali Dk. Ulimboka alipokuwa amelezwa MOI.
• Serikali ndiyo mtuhumkiwa mkuu katika sakata la kutekwa na hatimaye kujeruhiwa kwa Dkt. Ulimboka. Maelezo yake ya awali, ya kwamba alitekwa na watu wenye silaha, yamewafanya baadhi ya watu waamini kuwa alitekwa na polisi.

• Aidha, maelezo yake mengine ya kwamba alipotekwa aliwekwa katika gari lililoelekea Barabara ya Bagamoyo, na kwamba walipofika eneo la Victoria alifunikwa uso kwa kitambaa cheusi, yameibua hisia za kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.

Ofisi za Usalama wa Taifa zipo jirani na eneo la Victoria, ingawa mmoja wa viongozi wao alipowasiliana na JAMHURI mwishoni mwa wiki alikanusha vikali wao kuhusika, “Wasihamishie matatizo yao kwetu. Sisi hatupo kwenye siasa zao. Hiki ni chombo huru na wala hatutaki kazi zetu kuingiziwa siasa. Na wala hatutaki kutoa jibu lolote kwenye vyombo vya habari,” alisema Afisa wa Usalama wa Taifa kwa ukali.

Viongozi wengi wa Serikali akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshatoa taarifa za kukanusha madai hayo.

Rais Jakaya Kikwete, katika hotuba yake ya kila mwezi kwa wananchi, alikanusha madai hayo na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitafanya kila linalowezekana ili ukweli wa jambo hilo uweze kujulikana kwa uwazi.

Katika hotiba hiyo, Rais Kikwete alisema; “Napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Stephen Ulimboka usiku wa Juni 26, 2012.

“Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

“Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa viungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.

“Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadamu madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.”

Madaktari wasisitiza Serikali haijinasui

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, aliiambia JAMHURI kuwa hata yeye ameyasikia maelezo hayo kwamba madaktari ndiyo waliomteka au wanatumiwa na vyama.

“Ukweli utabaki kuwa ukweli. Tunajua waliohusika wanajitahidi kweli kweli kujiondoa katika hili, ila itakuwa ngumu. Katika hili Serikali ina kazi ya ziada kujitoa. Tangu mwanzo tumeikataa Tume iliyoundwa na tunasema tunataka uchunguzi huru,” alisema Dk. Chitage.

Alisema wao wanahitaji uchunguzi huru unaopaswa kuwahusisha majaji na kada ya watu wanaoheshimika katika jamii, kitu anachosema kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha imani ya wananchi katika taifa.

Dkt. Ulimboka alindwa na Interpol
Habari zilizolifikia Gazeti la JAMHURI muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka alikuwa akilindwa kwa karibu na polisi wa kimataifa (Interpol) kutokana na maombi yaliyofikishwa kwao na wanaharakati.

Hata hivyo, habari hizi hazikuweza kuthibitishwa mara moja, kwani waliotajwa kufanya kazi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, hawakuweza kupatikana mara moja.

Chanzo: ************************** wavuti - wavuti

jamani, tusifanyane wapuuzi humu bwana! hizo story nenda kazieneze nyamkonge ambako ndio kuna watanzania wenzetu waliosahauliwa na waliokutuma wewe hadi mtandao hawaujui!
 
Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.

Nadharia hizo zinazozua utata wa hali ya juu, zinaonyesha na kutoa maelezo ya hatari, ambayo madaktari hawakubaliani nayo hata kidogo, ingawa wamekiri kuwa nao wameyasikia maelezo hayo waliyoyaita ya ‘kipuuzi’.

1. Nadharia ya kwanza inaelezwa
kuwa Dk. Ulimboka alipigwa na madaktari wenzake wanaoamini kuwa alikuwa ‘amepotea njia’ na kuanza kuwauza kwa Serikali na taasisi zinazotoa fedha kufanikisha mgomo huo, “Kuna viashiria kuwa alikuwa anachukua fedha kutoka kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na chama fulani, ambao lengo lao ni kutaka vurugu ziendelee kuwapo na nchi isitawalike.

Lakini kilichotokea wanasema zile fedha alizokuwa anapewa alikuwa anawapiga panga njiani, hivyo wenzake wakaona wamshughulikie,” kilisema chanzo chetu kwa siri kubwa.

2. Nadharia nyingine ni ikle inayoelezwa kuwa wapo
wagonjwa waliofiwa na ndugu yao mbele ya Dkt. Ulimboka hapo Muhimbili, na waliahidi kulipiza kisasi, hivyo hii nayo inafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kubaini ukweli wake.

3. Nadharia ya tatu na ya mwisho ni ile iliyogusiwa hadi bungeni na wabunge wa CCM - akina Mwigulu Nchemba na Injinia Stella Manyanya -
kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahusika na utekaji wa Dk. Ulimboka kwa nia ya kuwafanya wananchi waichukie Serikali.

CHADEMA kupitia Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, John Mnyika, imekanusha mara moja na vikali kuhusika na unyama huu, na baada ya kubainika kuwa hoja hii ingeleta machafuko katika ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge Anne Makinda ameamua kuipiga marufuku isizungumzwe bungeni.

Dkt. Ulimboka, ambaye si mwajiriwa wa Serikali, anadaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Juni 26, mwaka huu Dar es Salaam. Baada ya kupigwa na kujeruhiwa, inadaiwa kwamba alitelekezwa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni jijini humo.

• Wakati utata wa tukio hilo ukiendelea kutanda, kumekuwa na taarifa nyingi, lakini zinazotajwa zaidi ni ile ya kwamba Dk. Ulimboka alifanyiwa kitendo hicho na marafiki zake wa karibu. Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya usalama zimedokeza kuwa chanzo cha kadhia hiyo ni kujitokeza kwa mgongano wa maslahi kati yake na wenzake.

• Inaelezwa kwamba wenzake hawakufurahishwa na matumizi ya fedha na misaada mingine iliyokuwa ikitolewa na asasi zisizo za kiserikali, ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mgomo wa madaktari nchini, “Jambo hili hatujalithibitisha moja kwa moja, lakini tumepata taarifa kuwa baadhi ya rafiki zake ndiyo walioshiriki kumteka kwa sababu za kimaslahi.

Tunaendelea kuchunguza kujua ni maslahi gani ingawa kuna taarifa zinazodai kwamba wenzake walianza kumtilia shaka juu ya mwenendo wake na dhima aliyopewa ya kuwatetea madaktari. “Inasemekana walianza kumtilia shaka kwa ukwasi alioupata ndani ya kipindi kifupi, wenzake wakawa na imani kuwa huenda anajinufaisha na uenyekiti,” kimesema chanzo kingine.

• Kuna madai mengine kwamba tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dkt. Ulimboka lilitokana na ndugu wa mgonjwa mmoja aliyefariki dunia kwa kukosa matibabu, bado nayo ni ya kutia shaka kubwa. Hata hivyo, daktari huyo hakuwa mwajiriwa wa serikali, ingawa inadaiwa kuwa kwa nyakati kadhaa alikuwa amepewa nafasi ya kuwahudumia wagonjwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI).

Mmoja wa wafanyakazi wa MOI aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina amesema; “Kuna ndugu walikasirika baada ya mgonjwa wao kufariki dunia. Hawakufurahishwa na majibu waliyopewa na mmoja wa madaktari (Ulimboka). Walionekana kuchukia. Siku chache baadaye ndipo ukatokea huo utekaji. Baadhi yetu tumelihusisha na kifo cha yule mgonjwa.”

Dkt. Ulimboka kwa sasa anatibiwa nje ya nchi. Taarifa za awali zilisema alipelekwa Afrika Kusini, ingawa kumekuwapo na taarifa nyingine kwamba anatibiwa katika moja ya nchi barani Ulaya.

Madaktari wenzake walikataa msaada wa Serikali wa kumpeleka nchini India kwa matibabu, jambo ambalo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamaja, amenukuliwa akisema limeisikitisha Wizara na Serikali kwa jumla.

Pamoja na kukataa ofa ya matibabu, madaktari hao walizuia viongozi wa Serikali kwenda kumjulia hali Dk. Ulimboka alipokuwa amelezwa MOI.
• Serikali ndiyo mtuhumkiwa mkuu katika sakata la kutekwa na hatimaye kujeruhiwa kwa Dkt. Ulimboka. Maelezo yake ya awali, ya kwamba alitekwa na watu wenye silaha, yamewafanya baadhi ya watu waamini kuwa alitekwa na polisi.

• Aidha, maelezo yake mengine ya kwamba alipotekwa aliwekwa katika gari lililoelekea Barabara ya Bagamoyo, na kwamba walipofika eneo la Victoria alifunikwa uso kwa kitambaa cheusi, yameibua hisia za kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.

Ofisi za Usalama wa Taifa zipo jirani na eneo la Victoria, ingawa mmoja wa viongozi wao alipowasiliana na JAMHURI mwishoni mwa wiki alikanusha vikali wao kuhusika, “Wasihamishie matatizo yao kwetu. Sisi hatupo kwenye siasa zao. Hiki ni chombo huru na wala hatutaki kazi zetu kuingiziwa siasa. Na wala hatutaki kutoa jibu lolote kwenye vyombo vya habari,” alisema Afisa wa Usalama wa Taifa kwa ukali.

Viongozi wengi wa Serikali akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshatoa taarifa za kukanusha madai hayo.

Rais Jakaya Kikwete, katika hotuba yake ya kila mwezi kwa wananchi, alikanusha madai hayo na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitafanya kila linalowezekana ili ukweli wa jambo hilo uweze kujulikana kwa uwazi.

Katika hotiba hiyo, Rais Kikwete alisema; “Napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Stephen Ulimboka usiku wa Juni 26, 2012.

“Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

“Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa viungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.

“Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadamu madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.”

Madaktari wasisitiza Serikali haijinasui

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, aliiambia JAMHURI kuwa hata yeye ameyasikia maelezo hayo kwamba madaktari ndiyo waliomteka au wanatumiwa na vyama.

“Ukweli utabaki kuwa ukweli. Tunajua waliohusika wanajitahidi kweli kweli kujiondoa katika hili, ila itakuwa ngumu. Katika hili Serikali ina kazi ya ziada kujitoa. Tangu mwanzo tumeikataa Tume iliyoundwa na tunasema tunataka uchunguzi huru,” alisema Dk. Chitage.

Alisema wao wanahitaji uchunguzi huru unaopaswa kuwahusisha majaji na kada ya watu wanaoheshimika katika jamii, kitu anachosema kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha imani ya wananchi katika taifa.

Dkt. Ulimboka alindwa na Interpol
Habari zilizolifikia Gazeti la JAMHURI muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka alikuwa akilindwa kwa karibu na polisi wa kimataifa (Interpol) kutokana na maombi yaliyofikishwa kwao na wanaharakati.

Hata hivyo, habari hizi hazikuweza kuthibitishwa mara moja, kwani waliotajwa kufanya kazi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, hawakuweza kupatikana mara moja.

Chanzo: ************************** wavuti - wavuti

Mtazamo wangu,.....
Ama kweli serikali inajitahidi kwa udi na uvumba kujinasua ila
haitofanikiwa kamwe.

kwenye red hapo juu;

nadharia ya kwanza, kama ni kweli alitekwa na kupigwa na madaktari wenzake iweje wao madaktari wajichangishe na kupata fedha ya kumpeleka nje kwa matibabu?????
na nikwanini wakatae msaada wa serikali?????
na iweje wao wajiunge na wanaharakati katika kumwombea ulinzi wa polisi wa interpol?????
manake kama ni kweli wao wamehusika ni dhahiri wameshaona kwamba Dk Ulimboka anawatia hasara tu na logicaly wangekubali msaada wa serikali ili wasiingie garama kwa mtu wasiempenda,kwa mtu anaewaangamiza.

kwenye nadharia ya pili,hapo sijawaelewa vizuri kwa maana kama Dk Ulimboka sio mwajiriwa wa serikali na anafanya kule MOI kwa part time, iweje awe msemaji wa kuwajibu hao wagonjwa na wauguzaji wao pale MOI?????? Utata mtupu.

kwenye nadharia ya tatu,hii inachekesha kabisa, tokea mwanzo wa kuijua chadema, sikuwahi kuona wala kusikia wameshutumiwa kwa makosa ya jinai, na hta kama wakishutumiwa inakua ni siasa na mwisho wa siku inafahamika kuwa ni uwongo ulio kithiri.

hizi nadharia zote hazina mashiko, na serikali haina namna ya kujinasua katika hili tukio la kinyama, kibabe, na kijasusi
 
Hakuna cha ajabu,hivi nyie mnategemea nini! Ni dhahili atatungiwa uongo wa namna hiyo,ikiwezekana kitatokea kikundi kilicho undwa na kitadai walihusika kufanya unyama huo kutokana na uchungu walioupata wa ndugu zao kupoteza maisha sababu ya mgomo. Mwisho wa siku kesi dhidi yao kesi itaenda itaenda itaenda itaenda itaenda itaenda...
 
Dkt. Ulimboka alindwa na Interpol
Habari zilizolifikia Gazeti la JAMHURI muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka alikuwa akilindwa kwa karibu na polisi wa kimataifa (Interpol) kutokana na maombi yaliyofikishwa kwao na wanaharakati.

Hata hivyo, habari hizi hazikuweza kuthibitishwa mara moja, kwani waliotajwa kufanya kazi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, hawakuweza kupatikana mara moja
Hii ya Ulimboka kulindwa na Interpol kidogo haikukaa sawa maana Interpol ni Internatinal Policing ambayo huandaliwa na vyombo vya Usalama kutokana na makubaliano ya nchi husika Kimataifa. Sasa kama Ulimboka analindwa na Interpol wakati sisi tuna mahusiano na South Ktk Policing inanipa picha nyingine kabisa..I mean what's going on! Ni nani hasa aliyekusudia kumuua Ulimboka? maana kwa maelezo yake mwenyewe sioni hata moja nililo karibiana na hizo nadharia zilo andikwa hapa.
 
You can cheat some people all the time, you can cheat all the people some time BUT YOU CANT CHEAT ALL THE PEOPLE ALL THE TIME
 
These are very childish cooked conspiracies that even a common non-intelligent staff can nullify. The truth lies hereunder:
2719468_orig.png

647529_orig.png

Hii barua yafaa copy yake ipelekwe AU, kwa Ocampo, Mo Ibrahim award committee, nk. kwa wide circulation. Pia itafasiriwe kwa kiswahili ili watanzania wengi waelewe alichoandika Rais wa Madaktari
 
Last edited by a moderator:
Ah As usual, polisi wetu siku hizi wamegeuka kuwa wapiga ramli! Professionism imekwisha, more manual and physical intelligence than intellectual, all brainpowers zimeenda, zilizobaki chache ni corrupted! Ooh My Tanzania, waendeshwa kuelekea wapi nchi yangu?
 
Udhaifu kutoka kwa intelijensia yetu mara nyingine hasa viongozi wake kwa upeo wao chovu wa kujaraibu kuzima moto kwa mafuta ya taa.

1. Kama polisi wamejua kuwa madaktari wenzie ndiyo walihusika kumtesa Ulimboka, kwanini isiwataje? isiwakamate? Huyo silensa na kundi lake vipi lisifahamike Kenya, na iweje polisi imwamini huyo mtu aliyejifanya kukiri kumkamata ulimboka, au ndiyo ile aliyemwua sokoine ni mgeni?

2. Iwaje polisi wamwamini alijisingizia kumkamata na kumtesa ulimboka, lakini isimwamini ulimboka kumtambua afande Hemed Msangi, katika kuhusika kwake katika tukio hilo?

Nafikiri intelijensia hapa inajaribu kujificha kama kenge, maana kenge akijificha kichwa hata kama mwili unaonekana anadhani amejificha. Matokeao yake ni kuwa, majasusi waliopo ktika balozi zote tanzania, wanaliona hili....., na jina la Tanzania linahesabiwa katika listi ya wauwaji.

Kibanga Msese
 
huyu kengemaji sijui anafikiria kutumia nyayo za miguu... hasomeki kabisa labda wangemuanzishia jf ya kijani
 
kesho atajitokeza mwingine, atadai Dr alichukua bibi yake so akaamua kumfanyizia, halafu tutamwona kova kwenye Tv kwa mbwembwe akituambia mtuhumiwa mwingine amekamatwa ni raia wa Burund, hii ni kama EPA tu!
 
Wanatakaja kuja na ya kwao tusiyo yajua, mbona yaliyo wazi na yajulikanayo hawayagusi, mimi nilitegemea kuwa katika hali ya kawaida kwa kauli ya Dr. Ulimboka hao wa chunguzi wa kipolisi wangeingia katika malango ya Ikulu kuwahoji watu au yule mtu ambaye alitajwa Dr. Ulimboka kuwa walikuwa naye siku ile.
Kuna bint nimesikia anaitwa Lulu ambaye anahusishwa na mauaji ya msanii mmoja, naambiwa anashikiliwa, kwa kuwepo eneo lille na marehemu, kuna watu wengi wapo ndani kwa sababu ya kutajwa tu.
Vipi wengine pamoja ya kutajwa hawajasogelewa ili kuhojiwa? Hiyo nyingine ya kusema eti kuna mtu alipoteza ndugu yake pale MOI halafu akajibiwa vibaya na Daktari aliyetajwa katika mabano kuwa ni Ulimboka, haiingii akilini kwani kwa hadithi inavosimulika inaonyesha kama vile Ulimboka ndiye alikuwa na wajibu wa kumhudumia yule marehemu au kama vile ni sehemu ya Staff wa Pale MOI akafuatwa na mhusika na kumjibu hivyo, haiingii akilini kwani Ulimboka si muajiriwa wa serikali.
Naona hili suala limeshawashinda Polisi na sasa wameanza kutumia watunzi wa Riwaya ili kuuhadaa UMMA.
 
Leo tumesikia kuna mtuhumiwa mmoja muhindi kakamatwa alikwenda kuungama Kanisani..
 
Back
Top Bottom