Siri za Uchunguzi wa Tukio la Dkt. Ulimboka zaanza Kuvuja

ukweli utabaki kuwa ukweli,kutokuundwa kwa tume huru ni ushaidi tosha wa serikali kuhusika,serikali iseme kwa nini polisi wanalazimisha kuchunguza wao,hapa haitoki hata kwa nini
 
Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.....​



Ukweli utababki palepale,kwamba serikali haiwezi kujinasua juu ya swala la dr ulimboka. Sasahivi wameamua kutumia propaganda kwa kuweka nadharia zenye ufinyu wa fikra...

Kwakua dr ulimboka alikua na malumbano na serikali kwanini isiwekwe pia nadhalia ya kwamba serikali ilimteka ili ipoteze uelekeo wa mgomo wa madaktari na hata siku ambayo pinda angetoa tamko...madaktari wangekua na mgawanyiko mkubwa kwakuwa pengine walishajipanga kwa hilo...

Huu ni uvumi usio na maana yoyote na kama hivo ndivyo serikali inafanya kazi basi udhaifu wake unadhihilika bayana,matukio mengi sana yanatokea tanzania report zake zinabaki na giza....mimi binafsi siiamini serikali ya ccm.
 
Tuseme yote lakini pia tukumbuke matukio ya vifo vya akina CHACHA WANGWE, kifo cha mtu alisemwa kuwa mfuasi wa CDM wakati uchaguzi mdogo kule Igunga. Tamko la Ulimboka kuwa mmoja wa watekaji wake alikuwa amevaa magwanda.
Hakina matukio hayo yanaweza kubadili kabisa mtazamo wa watanzania walio wengi wa nani anahusika hasa na tukio hili la utekwaji Ulimboka. Kwanini tukio lolote ambalo CDM wanatuhumiwa, wanaharakati nao wanakuwa nyuma kwa karibu sana?

Kama unafikiri ukweli ndio huo kuhusu CDM kuhusika, ni kwa nini serikali haiwajibiki kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua? Mbona tulishuhudia kukamatwa haraka kwa wauaji wa watalii kule mbuga ya wanyama hivi karibuni? Nini kinachoshindikana kuwabaini CDM na kuwakamata wahusika? Kuna jambo linalojificha hapo. Likely utakuwa unajua!!!
 
Hawawezi kudanganya wtz wote, watabwabwaja weeeeeeeeeeee mwisho wa siku serikali inahusika, yaani hapo wamenaswa tena pabaya na hiyo tume yao feki, wao walishaambiwa hiyo tume haitakiwi wakalazimisha halafu majibu yanayotolewa ni yale yale inamaana wamecopy na kupest kweli hayo ni mazuzu.

AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Ukweli haujifichi, utachelewa kidogo tu, natamani hiyo siku wata watakapo aibika, wata achwa uchi, ongeeni uupuzi wenu mpaka mate yawakauke.

Kama mnaweza kumdanganya Mungu basi mmefanikiwa damu ya mtu haiendi bure.... na zaidi mwaka 2015 tunawapiga chini mkichakachua tena tuna wachakachua na nyie.

Tumewachoka vibaya sana
 
Ninyi ni wajinga sana.Hivi mnadhani mnaweza kubadilisha mawazo ya watanzania kuhusu nani hasa anahusika na kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa Dr.Ulimboka kwa hoja zenu za kutunga.No way,we all know kwamba ni usalama wa taifa.Lakini siku moja,siku mbaya ya kuomboleza inakuja,when you will have to answer for your actions. uhiwa
Njia ya muongo ni fupi, Ulimboka alishaongopa Mwenyewe, kusema aliyemteka katoka ikulu bila kumtaja jina nin dhahiri anahisi tu na hakuna ukweli wowote na hata akija leo hana la kusema.
 
Tuseme yote lakini pia tukumbuke matukio ya vifo vya akina CHACHA WANGWE, kifo cha mtu alisemwa kuwa mfuasi wa CDM wakati uchaguzi mdogo kule Igunga. Tamko la Ulimboka kuwa mmoja wa watekaji wake alikuwa amevaa magwanda.
Hakina matukio hayo yanaweza kubadili kabisa mtazamo wa watanzania walio wengi wa nani anahusika hasa na tukio hili la utekwaji Ulimboka. Kwanini tukio lolote ambalo CDM wanatuhumiwa, wanaharakati nao wanakuwa nyuma kwa karibu sana?

Sikia wewe Kenge,
Vifo vyote hivyo vimesababishwa na CCM.
Kama CDM wangekua wameshiriki kwa hayo matukio, wangekwisha kamatwa zamani sana.

Kenge wengi hufikiriaga kinyume kutokana na akili zao kuchanganyika na maji.
 
Waliowauliza usalama wa Taifa wakidhani watakiri ushiriki wao katika jambo hili nakaribia kuwaita wajinga! Kazi za watu hawa hufanywa kwa usiri mkubwa na mara zote hawajawahi kukiri kuhusika. Ila utazijua kazi zao katika namna zinavyofanywa!
 
kuna nadhalia moja siioni, au wameipiga ban? hii nadhalia ya kuwa hata usamlama wa taifa wanahusika mbona hawajaweka?
 
Wengine tumeanza maombi ya kukesha katika maombi na mfungo, mpaka aliyefanya unyama huu ajitaje mwenyewe. la sivyo Mungu aliye hai atamhumbua na atamshughulikia mwenyewe na ukweli napenda kuwaambia ndugu zangu,ukweli utabaki kuwa ukweli na utawekwa adharani na kila aliyeshiriki atajulikana. M
 
Mungu wangu aishivyo watajitokeza wenyewe na watatubu mbele ya umma wa watanzania. Mimi sio mtabiri sio mtume na kama mitume wameshindwa Mungu aliye hai anakwenda kunyanyua watume wengine watathibitisha hili mwaka huu au ishi
 
Mbona wanaanza kujihisi si wasubiri ulimboka apone coz yeye ndo anajua nani alihusika. Ningeshauri tanzania ifanye kama kenya ilivyofanya kwa kuleta tume ya uchunguzi kutoka uk waje kuchunguza wao maana wale hawatishiwi au kupokea rushwa kama wabongo. Kue na tume huru kutoka nje ije kuchunguza tukio hili
 
These are very childish cooked conspiracies that even a common non-intelligent staff can nullify. The truth lies hereunder:
2719468_orig.png

647529_orig.png


 
Last edited by a moderator:
Mbona neno "misaada toka mashirika yasiyo ya koserikali" limetokea mara nyingi kwenye habari hii, ina maana madaktari wamekuwa wakipokea misaada toka huko?

Nadhani hizi tetesi ni za uongo ma siku zote mwongo huwa hakamiliki nyanja zote!
 
Too cheap to divert my attension.one of the state organs walitumika kumteka na kumtesa ulimboka.
 
Nawashauri madaktari mliopanga kuandamana msifanye hivyo. Wanaweza kupewa wahuni tu fedha na mtu yeyote au chombo chochote wakawavurumishia mawe na hata vinyesi ili mradi tu maandamano yenu yaingie doa kwa nia ya kuonyesha kuwa wananchi wana hasira dhidi ya mgomo wenu. Jaribuni kutafakari kwa undani uwekano wa hilo kutokea, haswa ukizingatia kwamba mgomo wenu sasa umeingiliwa na siasa zaidi badala ya ukweli na hali halisia.
 
Back
Top Bottom