tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 26,532
- 26,268
Mara nyingi tumekuwa tukisikia watu wakilaumiwa au kulaumiana kutoa 'siri' za serikali kwa wananchi. Hivi hizo zinazoitwa siri za serikali ni zipi na kwanini zinakuwa siri?
Ikiwa tunaaminishwa kwamba serikali huwekwa madarakani na wananchi na inatawala kwa manufaa ya wananchi, kwanini serikali iwe na siri ambazo wananchi walioiweka madarakani (watawaliwa) hawatakiwa kuzifahamu? Je, siri hizo zina nia njema kwa watawaliwa? Sisi tutaaminije kama hizo siri zina manufaa kwa wananchi wakati zimefanywa siri?
Kwa kuwa mtenda maovu (mwizi, mchawi, mlozi, mkabaji, jambazi, muuaji, fisadi, mnyonya damu, jangili, etc) ndiye hataki siri zake zijulikane, moja kwa moja inajengeka dhana potofu kwamba 'siri' za serikali ni za 'kiovu' kwa kuwa serikali haitaki wananchi wazijue. Ndio maana wakati mwingine serikali imekuwa ikihusishwa katika matendo maovu dhidi ya wananchi, hasa na baadhi ya watu wasioitakia mema serikali yetu tukufu.
Mara zote jambo la kheri hutangazwa sana kwa wananchi ili kuwajuza namna ambavyo serikali yao inawajali. Mfano halisi ni ununuzi wa bombadia, ujenzi wa SGR, mradi wa Stiglier's Gorge, ubanwaji wa mafisadi, n.k. Haya mafanikio yamekuwa yakitangazwa sana kila kukicha. Yasingefanywa SIRI kwa kuwa ni mambo chanya ambayo wananchi wanatakiwa kujuzwa na serikali yao tukufu. Kitendo cha kuficha baadhi ya mambo kwa kuyaita 'siri' ndicho kinacholeta ukakasi juu ya usiri wake.