Siri za Magufuli kuwa Rais zavuja

Siri za Magufuli kuwa Rais zavuja

Magufuli akiwa rais nadhani tutakuwa na kiongozi mbumbumbu sana... Sidhani kama hicho ndo watanzania wanachotaka kwa sasa....!!
 
Mabadirikooooo. Mwaka huu mtajifariji sana rais wetu ni Lowassa hiyo mwingine ataendelea kujidanganya tuu
 
SIRI ZA MAGUFULI KUWA RAIS ZAVUJA.

Katika hali ambayo siyo ya kawaida siri za ndani ya ccm na watanzania kumchagua John Magufuli zimevuja na sasa zinazagaa mtaani na sio siri tena .
Katika mambo ambayo yatasababisha Magufuli kuapishwa na pia kutangazwa hapo tarehe 29 oct kuwa rais wa awamu ya tano ni yafuatayo.

Uwezo wa kujinadi, hasa baada ya kupewa mgombea mpinzani ambaye ni mdhaifu ambaye hawezi hata kujinadi kwa zaidi ya dakika tano, hali hii inamfanya Magufuli kuwa rais na siyo diri tena.

Pili, Team yake ya ushindi ina watu makini ambao ni washauri wazuri na ambayo wamekuwa wakisikilizana na kupanga mikakati mizuri ya ushindi, mikakati ambayo haijawahi kuvuja na imekuwa ikitekelezeka.

Ilani nzuri na yenye maslahi mapana kwa vijana na wananchi wote hai inayosababisha kujinadi na kujiuza kwake kuwe ni kazi rahisi mno kwa wananchi.
Nne ni adilifu na uzalendo wa hali ya juu aliouonyesha wakati akiwa kiongozi mdogo tuu katika wizara na idara mbali mbali za serikali hali inayo mpa sifa ya kuendelea kuwatumikia watanzania.

Watanzania hawapendi kiongozi mbaguzi na mdini, kitu ambacho Magufuli amekuwa si mdini wala mbaguzi, tofauti na mpinzani wake ambaye amekosa sifa hiyo na ameonesha hisia zake hadhari kwa kuwaambia watu wamchague kwa misingi ya dini yake.

Sera yake ya kuwafunga mafisadi na wala rushwa wote nchi pili kuhakikisha kuwa huduma mhimu zinawafikia wananchi imempa kura nyingi na kusababisha Watanzania kumwamini na kumchagua hapo oct 25.Amekuwa mkali sana juu ya watoa na wapokea rushwa ili kuondoa mfumo huo mbovu unaosababisha wananchi kukosa huduma mhimu na za lazima kwa kizuizi cha rushwa, kitu ambacho ni kero kubwa kwa jamii hasa wanapokuwa wanatafuta huduma mhimu za kijamii?

Kwa hali hiyo hizo ndizo siri ambazo Ccm wamekuwa wakificha Kwamda mrefu, ndiyo siri za magufuli kuapishwa na kuwa rais wa awamu ya tano.

labda uwezo wake kuwapigia push up mademu
 
Wacha zivuje na ndio rais wa TZ lkn kuna ilani ya chama kamwee magufuli hatotekeleza Yale anayoyatangaza lazma afate kizingiti cha chama
Viva ccm
 
Kwakweli acha zivuje tu lakini magufuli ndio rais wa tanzania awamu ya tano. Magufuli mzalendo, mchapa kazi, mfuatiliaji na mwadilifu.

Ni kweli Kabisa atarudisha na nyumba zetu,na atamsaidia kibiashara Antony Diallo
 
Mtafute sehemu za kwenda nyie ukawa kwa kuwa rais ni MAgufuli sasa sijui mnatarajia nini baada ya oktoba 25,mwalimu alimkata na sisi tutamkata jmpili hii,hana nafasi hapa

Nikifikiria alivyopiga pushup na kurusha miguu mara katokea juu ya gari naungana na marehemu mtikila juu ya faili la Milembe la huyu jamaa, sasa huko ikulu sijui itakuaje
 
Mleta uzi hii ndio siri eeh, sidhani kama una akili timamu, unakurupuka huko na viroba na bangi zango unatuambia tope ndio siri, kaa kimya jpili sio mbali, mwenye kaya kaisha anza tapatapa we ndio nani huna lolote mtumia Jk huu uzi anaweza pata faraja kwa jinsi anavyoweweseka, oh wapiga kura waliojiandikisha wako m28, oh ukaisha piga kura unde home ????
 
Back
Top Bottom