Siri yafichuka: Membe& Mwakyembe wamuondoa H. Masoud

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1]
IMG_5972.JPG
[/h]Written by zamko // 25/07/2012 // Habari // No comments


Asalamu alaikhum ndugu Wazanzibari wa ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu.Natumai kila mtu atakua amekasirishwa na matokeo yanayotendeka huko nyumbani hasa kuzama kwa Skagit. Lakini kuna wale waliopata afueni kwakuondoka madarakani kwa H.Masoud (Waziri Wa Usafiri). Wengi wetu tumeona hatua aliofanya HM ni hatua nzuri hasa kwavile yeye alikua Waziri na alikua na uwezo wakuondoa uoza wa ubadhirifu lakini hakufanya hivyo. Sio hivyo tu, ila wengi wetu tunaamini wabadhiru ndio waliobakia madarakani na H.Masoudi amekua muhanga wa SMZ vs Tanganyika.
Hii nikutokana na Msimamo wa H.Masoudi juu ya ufufuaji na uboreshaji wa Bandari na Airport katika Nchi yetu ulikua umeshaonekana ni tishio kwa Bandari ya Tanga-Tanganyika na Airport ya Mrimani.
Msimamo wa H.Masoudi juu ya kuifanya Zanzibar kua bandari huru na usajili wa Meli (wanazosema ni za ki Iran) kuliwakosesha usingizi Benard Membe, na Mwakyembe kule Tanganyika. Kwani walijua uombaji wao wa Misaada kutoka USA na Nchi za EU umo hatarini.Hivyo njama za kwanza za kumuondoa H.Masoud zilianza kupangwa wakati wa MV Spice Islander. Lakini hizi zilipangwa na Wahafidhuna-Seif Ali Iddi na Aboudi ili kutekeleza matakwa ya S.Tanganyika – Kwamba Bandari ya Zanzibar isitengenezwa kama wanavotaka CUF (Sobotarge).
Wito wa Ni liazima CCM watumie Sera zao katika uongozi wa SUK ulitoka kutoka Tanganyika/ Muungano na waliambiwa (wahafidhuna) wasiachie Sera za CUF ku- “SHINE THROUGH” kwani Wazanzibari waliokua na imani na CCM watapoteza Imani zao.
Hivo Sobortage ya kwanza yakumuondoa H.Masoudi ilishindikana na ikapangwa ya pili ambayo ndio iliomg´oa Hamadi Masoudi.Wazanzibari tukumbuke kwamba Boti zote mbili zilizozama ziliondokea Dar (Tanganyika) na zilikua zimeshajaza.
Ikiwa tutangalia Katiba ya Tanganyika/Muungano inasema kwamba Usalama wa Nchi na Ulinzi ni katika Mambo ya Muungano. Hapa Usafiri Usalama wa Baharini na angani ni Mambo ya Muungano ambayo Wizara ya VIP2 na Ile ya Tanganyika walikua wanatakiwa Washirikiane kuhusu upakiaji na upakuaji wa mizigo. Au uondokaji na Uingiaji wa Boti. Lakini Spice Islander iliachiwa kupakia kule Tanganyika na ilipofika Unguja hakukua na Onyo wala taarifa kwamba meli iangaliwe kwani imeshapakia sana. Na matokeo hayo yalijirudia hivyo hivyo katika Boti ya “SKARGIT”.
Hivo sababu zakumgoa H:M zilipikwa kwakushirikiana na Viongozi wa CCM-Tanganyika na wale waliopo VIP2 pamoja na Wahafidhuna wengine wa ZMA na bandari akina (GAVU). Lakini hili alionywa H.Masoudi zamani na yeye aliwakumbatia Wahafidhuna nakusahau kwamba (Wahafidhuna) wakisaidiwa na S-Tanganyika wataweza kuivuruga Amani na Umoja wa wazanzibari.
Tukitaka kujikumbusha yaliopita natuangalie tunavokumbuka kabla ya H.Masoudi au (CUF) kuingia katika Uozo wa SMZ. Airport ilikua haijulikani wapi mtu anaingia na wapi mtu atatokea. Mparaganyiko na ubadhirifu wa Uwanja wa ndege, rushwa, jeuri ktk Airport vilikithiri. Licha yakwamba kuna Watalii na Ndege za kila aina zinazoshuka Zanzibar kila siku. Lakini pesa za Airport fees au Tax duty ilikua ikiishia Mikononi mwa Viongozi (Wahafidhuna) na watoto wa Mapinduzi.
Uwanja wa Pemba ulikua ni Shamba la Migomba na Mihogo na watu walifanya njia.Baada ya CUF kuingia ndani ya SUK na H.Masoudi kua Waziri wa mawasiliano wananchi waliofanya mashamba ktk Maeneo ya Uwanja wa Pemba walilipwa compasation nakupewa mwaka ili wamalize kuvuna vipando vyao. H.Masoudi waliweza kuweka Uzio wa Uwanja huo kwa Upanuzi na alianza mbio zake yeye na Waziri wa Fedha Mh. Omar Yusuf. Hili ni jambo jengine ambalo liliwakera sana CCM-Wahafidhuna (hata Abdul Hamid na Kificho) pamoja na Tanganyika. Kwanini uwanja wa Pemba ujengwe wakati ni kaji-Kata kadogo tu. Masuala haya yalikua midomoni mwa Watanganyika na Wahafidhuna walihakikisha hili halita tendeka.
Ndani ya SMZ kabla ya SUK au (CUF) – Zanzibar ilikua mwananchi wa Chini hathaminiwi, Mawizara ya SMZ yaliacha kuajiri Wazanzibari wenye hakki yakuijenga na kuitumikia Nchi yao. Na kujaza Watanganyika, Wakenya, Waburundi na hata Wakongo kama wakitaka kazi wangefanikiwa. Uoza wa wafanyakazi hewa wasiokua na sifa za kufanya kazi ulikithiri. SMZ iligeuka Kinyanganyiro cha Wanamapinduzi na Wahafidhuna kila Mmoja anataka yeye.Wakati wa Abedi Karume ulirudi kwamba Wasomi Wazanzibari walionekana Maadui wa Nchi na kuanza kutafuta kazi Tanganyika.Hii ndio Ajenda ya Kuimaliza Zanzibar waliokua nayo Serikali ya Tanganyika.Ilimradi ilikua paraganya ndani ya SMZ.
Tumeona wenyewe kwamba hata kama kuna makosa mengi ndani ya SUK lakini wananchi sasa wameshikana (Alhamdulillah) Na wengi wetu tunajivunia kua Wazanzibari. Hata kua H.Masodi amefanya Uzembe lakini tunajua Serikali ya Tanganyika ikisaidiwa na Wahafidhuna Wamemuondoa Hamadi Masoudi kwa msimamo wake juu yakusimamia Maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari.
Kupepea kwa bendera ya Tanganyika/Muungano ndani ya meli (wanasoma za Iran) kumeifanya Tanganyika kutafuta njama zakuwaondoa viongozi wa CUF katika madaraka na kuanzisha mizozo ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Zanzibar. Hivyo Siri hii ilisikilikana ikizungumzwa na mmoja wa CCM kindaki ndaki ambaye anatumiliwa na S-Tanganyika. Kusema wamefanikiwa na sasa wanataka kuhakikisha usajili wa Meli za Iran unafutwa.
Samahanini kwakuandika makala ndefu lakini niliposikia haya jana nilisema niwataarifu.
 
Nimefuatilia makala yako ndefu ndugu Abdulsahaf lakini nilichokiona ni malalamiko na shutuma ambazo hazina kichwa wala miguu dhidi ya Membe na Mwakyembe. Sioni wanaingiaje kwenye maamuzi ya ama waziri wa Zanzibar ajiuzulu au abaki madarakani. CUF walijua kuwa wanaingia kwenye SUK inayoongozwa na CCM na ambayo sera zake zinaathiriwa kwa kiasi kikubwa na CCM Taifa yenye makao yake makuu Dodoma. Sioni sababu za CUF kuipinga CCM wakati ni wabia ndani ya SUK. Kama CUF mnahisi kuonewa jitoeni serikalini ili muipinge serikali kwa nafasi.
 
Chombo cha kuwasemea kuhusu muungano mnacho (bunge lenu) kitumieni, acheni kujisaidia barabarani.
 
Hizi CONSPIRACY theory za WAPEMBA ni za ajabu ajabu?

Just imagine Mv Skagit ilisajiliwa na ZMA na sio SUMATRA.

MV Skagit ilikuwa grounded huko USA, kwamba ilikuwa haikidhi marine safety.

MV. Skagit ilinunuliwa na Wazanzibari through mnada wa E-bay.

ZMA ikaipatia Mv Skagit hati ya ubora ya kusafirisha abiria majini.

Watumishi wote waliokatisha ticket siku hiyo ya ajali wote ni Wazanzibari.

MV Skagit baada ya kuzama limekuwa kosa la serikali ya JMT na njama za Tanganyika as if ndiyo iliyonunua na kusajili meli mbovu ambayo ilikuwa grounded USA.

BTW, kuhusu meli za Iran zilizosajilia na ZMA hata kama angekuwepo Hamad Masoud, kama kweli zitathibitika ni za Iran zitafutiwa usaijili. Hata Dr. Shein hawezi kuzuia hilo achilia mbali huyo Hamad Masoud wenu. Tanzania ililidhia azimio la UN la kuiwekea vikwazo Iran. Hivyo kitendo chochote cha Tanzania kuisaidia Iran kukwepa vikwazo vya UN ni kuvunja azimio la UN ambalo Tanzania ililidhia.

Acheni kila mara kufikiria kwasababu mna husda na Tanzania. Get your facts together hii BLAMING GAME WILL TAKE YOU NOWHERE.

Jiandaeni kwa ajali nyingine zaidi, kwasababu ZMA imesajili ma-Meli mabovu ambayo hayakidhi viwango vya usalama vya usafiri wa majini.
 
Hadi lini wazanzibar mtaacha kulalamika, kama hamuutaki muungano semeni live watu wawaelewe na sio kuleta mbwembwe, kwani alipokuwa anajiudhuru uwaziri aliwataja Membe na Mwakyembe ndo waliomsababisha akijiudhuru, kwani kujengwa kwa hiyo bandari kungesababisha hiyo meli isizame?

kwa kifupi hawa jamaa hawautaki muungano! nashangaa govt yetu ina wang'ang'ania nini! tatizo ni ufisadi,wizi!
 
umeshajibiwa wewe NI KILAZA wa kutupwa unacholalamika hakijulikani mm nachoona S/Tnganyika kutumia membe na Mwakyembe wamezizamisha hizo meli na hata Muungano ni wao
 
Back
Top Bottom