Siri yafichuka kukamatwa kwa Kibanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri yafichuka kukamatwa kwa Kibanda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Dec 20, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  JUKWAA la Wahariri nchini (TEF) limesema kukamatwa kwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Absalom Kibanda, ni utekelezaji wa mpango wa siri wa serikali, unaotokana na chama tawala kuitaka iwashughulikie waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi wa serikali.
  Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, anakabiliwa na tuhuma za uchochezi, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Kisutu, Dar es Salaam leo kujibu tuhuma hizo.
  Katika kuonyesha wahariri wanajua undani wa sakata hilo, jana Jukwaa la Wahariri lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likisema hatua ya serikali kutumia polisi kuwakamata waandishi wa habari na kuwafungulia kesi za jinai kunaihatarisha serikali yenyewe na kuuweka pabaya mustakabali mzima wa taifa.
  Tuhuma zinazomkabili Kibanda zinatokana na makala iliyoandikwa na mwanasafu wa wiki katika gazeti hili toleo la Jumatano, Samson Mwigamba, wa Arusha, Novemba 30, 2011.
  Katika makala hiyo, Mwigamba anawaasa polisi kutumia uungwana na akili wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao, hasa wanapotumia nguvu kubwa kudhibiti wananchi ambao wanatetea masilahi ya umma yanayowahusu hata wao wenyewe. Polisi wanadai makala hiyo ni ya uchochezi.
  Kibanda hakuandika makala hiyo, lakini anashitakiwa kwa mujibu wa wadhifa wake kama mhariri mtendaji wa gazeti lililoichapisha, kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, ambayo ni miongoni mwa sheria mbaya ambazo Tume ya Nyalali, wanaharakati na wanasiasa, wamekuwa wakishauri zifutwe au zirekebishwe tangu mwaka 1992.
  Baada ya kuwa wamemhoji na kumfikisha mahakamani Mwigamba siku kadhaa zilizopita, walimgeukia Kibanda; naye akajisalimisha makao makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Desemba 16, mwaka huu; akadhaminiwa kwa sh milioni tano na kuripoti tena polisi makao makuu jana, na kudhaminiwa tena kwa kiasi hicho hicho cha fedha.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Jukwaa la Wahariri iliyosainiwa na Katibu, Neville Meena, kukamatwa kwa Kibanda na Mwigamba na kufunguliwa mashitaka kumedhihirisha taarifa ambazo zimevuja kutoka kwenye vyanzo kadhaa serikalini na chama tawala (CCM) kwamba kuna mpango wa serikali kunyamazisha ukosoaji kwa kupambana na waandishi na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikifukua maovu ya watawala.
  "Mashitaka haya dhidi ya Kibanda na Mwigamba yanatushawishi kuamini taarifa zisizo rasmi juu ya kuwapo kwa mpango wa kuwashughulikia baadhi ya wahariri na waandishi wa habari ambao wamekuwa msitari wa mbele kukosoa waziwazi mienendo ya watawala," imesema sehemu ya taarifa hiyo.
  TEF imesema hatua ya kumkamata Kibanda na Mwigamba imekiuka utaratibu wa siku zote ambao serikali kupitia Idara ya Habari (Maelezo) imekuwa ikiwaita wahusika na kuwahoji sababu za kuandika, kuchapisha ama kutangaza habari ambazo zinadhaniwa kukiuka maadili.
  Wahariri hao pamoja na kupinga mpango huo mbovu, wameitaka serikali kuacha mara moja kuwakamata wahariri na waandishi wa habari, kwa kuwa hatua hiyo si tu inaathiri dhana nzima ya utawala bora wa nchi, bali inaliweka taifa katika hatari ya kutumbukia katika uovu uliokithiri, hasa pale wenye dhamana watakapofanya wapendavyo baada ya kuviziba mdomo vyombo vya habari.
  "Kwanza makala ambayo ni chimbuko la kukamatwa kwa Mwigamba na baadaye Kibanda haikuwahi kulalamikiwa na Ofisi ya Msajili wa Magazeti kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa taarifa nyingine nyingi, si kwa gazeti la Tanzania Daima tu, bali hata kwa magazeti mengine.
  "Kwa maana hiyo, hakuna barua yoyote kutoka Maelezo ambayo iliwasilishwa Tanzania Daima ikimtaka mhariri mtendaji kutoa maelezo ya kimaandishi au kufika kwa msajili kujibu tuhuma za ukiukwaji wa maadili ama sheria katika makala hiyo ya Novemba 30, 2011," imesema taarifa hiyo ambayo imechapishwa katika ukurasa wa tatu wa gazeti hili.
  Wakati Jukwaa hilo likitoa tamko, Kibanda anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo, baada ya jana kushindikana kutokana na kile kilichodaiwa na polisi kuendelea kuchukua maelezo ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd inayochapa gazeti la Tanzania Daima.
  Ijumaa iliyopita, Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini alijisalimisha polisi ambako baada ya kumhoji kwa zaidi ya saa tatu, aliachiwa kwa dhamana ya sh milioni tano, iliyotolewa na Mkurugenzi wa gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea, akitakiwa kuripoti tena jana.
  Hata hivyo, katika hatua isiyo ya kawaida, huku wakijua kwamba bado ana dhamana, polisi walimzuia tena Kibanda akiwa na mawakili wake Nyaronyo Kicheere na Juma Thomas, wakamlazimisha awe na mdhamini mwingine kwa kiasi cha sh milioni tano. Mhariri Mtendaji wa gazeti la Hoja, Yasin Sadiq, alimdhamini.
  Tayari habari zisizothibitishwa zinataja baadhi ya wahariri walio kwenye orodha ya kukamatwa na kushitakiwa katika mkakati wa serikali kutumia polisi kutisha waandishi wa habari na wakosoaji wengine wa serikali.
  Hata kabla ya Jukwaa la Wahariri kutoa tamko lao, vyanzo kadhaa vya habari serikalini vililidokeza gazeti hili kwamba polisi wanatekeleza mpango huu kwa amri ya wakubwa wanaokerwa na ukosoaji unaofanya na baadhi ya waandishi, wanasiasa, wanaharakati na vyombo vya habari

  na Janet Josiah
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ina maana topic hakuna hata mmoja iliyomgusa! mbona watu hawachangii! ajabu kweli!!
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  wana habari shikieni bango msikubali kudondokea mikononi mwa serikali dhalimu
  iliyojaa mafisadi isiyojali wananchi wake !
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ninawaombeni waandishi wa habari kushikamana sana kakatika hili,msimtelekeze mwenzenu kama mlivyo mfanya Jerry muro.pia nawaomba wananchi wenzangu tuungane na waandishi wote,wahariri wote,watangazaji wote wenye mapenzi ya kweli na sisi masikini hadi kufikia hatua ya kufichua uovu wa serikali.
  Nawaomba wahariri mjitokeze kwa wingi katika hili kuweza kulipigia kelele na kutokua woga kuendelea kufichua uchafu wa serikali
   
 5. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Wana habari hawawezi kushikamana kamwe, wao wenyewe wamegawanywa na wamegawanyika katika makundi ya kimaslahi. Wapo wanaotetea ufisadi na mafisadi na wapo wasiotetea ufisadi. Ni mara chache sna kuwa neutral linapokuja suala la maslahi binafsi. Usitarajie makanjanja kama wale waliojaa Habari Leo na wale wa New Habari corporation waungane na Kibanda kusaka haki ilhali kile anachokipinga Kibanda ndio chanzo cha lishe yao. Thubutu
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mi sielewi waandishi wa Tanzania ni lini huwa wanaungana na kuwa kitu kimoja.
  Jukwaa la wahariri pia nao wajue kuwa kutoa statement hiyo tu hakutoshi, wanatakiwa hivi sasa wawepo mahakamani, ili kama uamuzi utakaotolewa ukiwa biased, then waonyeshe counter- reaction.
  Amini usiamini, hizi soda soda wanazopewa baadhi ya waandishi na Wahariri ni mwiba wa sumu kwa taifa!...

  MUNGU SAIDIA!
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  hivi kwenye huo umoja wenu wa wahariri mnakaaga meza moja na wahariri wa jamba leo,habari leo,uhuru,..
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,548
  Trophy Points: 280
  Wajameni kwa msiojua, huu ni utekelezaji wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ni moja ya sheria kandamizi na imo kwenye ile list ya sheria 40 ambazo Tume ya Nyalali ilishauri zifutwe.

  Ninachokiona sasa ni kwa serikali kifanya double standards kwa kuwalenga inaowatafuta na kuwaacha kujivinjari inao wasupport.

  Tusimlilie Mwigamba na Kibanda, bali tupaze sauti zetu sheria hii isitishwe kitumika na badala yake sheria mpya ya habari yenye haki ya kupata habari ambayo serikali wameikalia tangu mwaka 2003, sasa iletwe bungeni na kuireplace hiyo Newspapers Act of 1976.

  Tena tushukuru Mungu kwa miaka hiyo yote, serikali haikuwahi kuitumia sheria hii ipasavyo kwani kama ingetumika huko nyuma, magazeti kama Mwanahalisi, Raia Mwema and the like yaliyojikita kwenye ukosoaji wa serikali, yangekuwa ni hadhithi tuu kwani yangeshafungiwa zamani!.

  Nionavyo mimi, lengo la serikali kwenye hiki kibano kwa Mwigamba na Kibanda tena watamuunganisha na printer, Mwananchi Communications, ni kutuma salamu kwa wahariri wote kuwa very carefull na contents za magazeti yao kwani sheria hiyo bado ipo!.

  Kitendo cha kumuunganisha printer kama sheria inavyosema ni kuhakikisha wachapishaji wanakuwa resiponsible na contents hali itakayopelekea kususa kuchapisha baadhi ya magazeti yatakayo leta burning issues!.

  Nimesema serikali inafanya double standards ili tuu kutishia nyau uandishi critique!.

  Bado sijajua Mwigamba anatetewa na nani, ila wanasheria watetezi wa Kibanda, Nyaronyo Kicheere na Juma Thomas, wote ni wanahabari/wanasheria waliofikia level za editors Nyaronyo akiwa mhariri wa Citizen na Juma Thomas alikuwa mhariri wa the Guardian, natumaini waitumia kesi hii sio tuu kuonyesha jinsi sheria hiyo ilivyo mbaya, bali kumconvince jaji pia atoe order sheria hiyo iwe scrapped off from the books of law!.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna cha serikali wala nini,kibanda nae ni wale wale tu,hana lolote,,,waandishi maslahi wanaochumia tumbo,,,,,hatudanganyiki ng'ooooooooooooooooooooooo!
   
 10. M

  MKWELIMAN Senior Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwa nini serikali kwa miaka yote hii imekuwa iki-dilly dally kuzifuta sheria hizo 40 Kama ilivyo pendekezwa na tume ya Nyalali ?????

  Hiki ni kiashiriyo cha serikali kandamizi. Watawala wanataka kung'ang'ania madarakani kwa gharama yoyote ile.
   
 11. C

  CHIPANJE JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ulitaka nani awe wa kwanza?
   
 12. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na hii case tuone mwisho wake utakuaje!!
   
Loading...