Siri ya waraka wa Mwakyembe yafichuka; Kisa ni kifo cha ghafla cha mhudumu ofisini kwake

Tokea mwishoni mwa mwaka jana 2011 hali yake ilibadilika ghafla, kabla ya hapo alikuwa akiugua kwa siri mpaka pale ambapo alipoamua kuweka wazi kuwa anaumwa ugonjwa wa ngozi na baadae kupelekwa India na Serikali ya JK baada ya JK kumotembelea na kubaini kuwa kweli mpinganaji Dr Mwakyembe ni mgonjwa.

Hata hivyo hivi karibuni Jeshi la Polisi kupitia DCI Manumba lilikanusha kuwa ugonjwa wake hauhusiani na kulishwa, kutupiwa wala kupakwa sumu. Japo Dr Mwakyembe alikanusha taarifa hizo, Serikali haikurejea tena na taarifa za kina kuthibitisha au kukanusha kwa ufasaha aidha kauli za Manumba au Mwakyembe...Serikali imekaa kimya.

Pamoja na haya yote, ukweli upo pale pale, Mpiganaji bado ni mgonjwa na watanzania wengi hawajui kwa undani anaumwa nini...lakini anaumwa. Katika mazingira haya ya utata wa kile anachougua, tulitarajia hata Dr Mwakyembe mwenyewe aruhusu labda hata Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua sampuli mwilini mwake na kumpima kuthibitisha kile kinachodaiwa anaumwa..angekuwa tayari hata kufanya vipimo vya hiyari (voluntary testing) ili kutudhirishia kuwa haumwi maradhi mengine zaidi ya athari za sumu.AU angeruhusu madaktari wake huko India kutoa kwa umma ripoti ya uchunguzi waliofanyiwa huko India (Hili lingepunguza mkanganyiko ambao upo sasa)..Haya bado hayajafanyika lakini mwenzetu anasumbuliwa na Serikali yake aliyoitumikia kwa moyo wa dhati na kujitolea haitaki kusaidia kuondoa kiwingu kilichotawala ugonjwa wake mbele ya wananchi...

Dr aNaumwa.....!!!

Kwahiyo Fikra zako zooote ndiyo umeamka na hili??? Inaonekana wewe vyombo vya habari ndiyo kwanzaaa vinakolea pande zako.
Heading na post ni old vision
 
Mh, hata siamini mambo yanavyofanyika kienjeji. Jamani hakuna hata postmoterm? Naelewa ukiondoka ghafla haukimbizwi kuzikwa kuna uchunguzi sasa hapa si inatuachia maswali mengi? Tunaelekea wapi baada ya miaka 50 ya uhuru.
 
kupambambana na mafisadi ni kazi ngumu sana.watu hawa wanajua kila kitu cha serikaili na wengine wamo ndani ya serikali.Wana kila mbinu za kijasusi zakuweza kufanya mambo yao yafanikiwe.Kuweza kuwapata watu wenye upendo wakweli wa watanzania na nchi yao ni kazi.Watu wakisha yapata madaraka wanabadilika kutoka kuwa waomba kura na kuwa maaramia wa wapiga kura wao!
 
inaniuma sana kwa huyu dada ambaye alibebeshwa sumu bila kujua then mauti yakapanta bila kufanikisha ndoto zake kisa vita vya wakubwa tena vya kifisadi pumbafu!!
 
inaniuma sana kwa huyu dada ambaye alibebeshwa sumu bila kujua then mauti yakapanta bila kufanikisha ndoto zake kisa vita vya wakubwa tena vya kifisadi pumbafu!!
 
WARAKA wa siri ulioandikwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, umezidi kuibua mambo mapya. Waraka huo ulioripotiwa mara ya kwanza wiki iliyopita na gazeti hili na kueleza mbinu, mahala ambapo waziri huyo anaamini aliwekewa sumu kupitia sabuni na taulo vilivyowekwa ofisini kwake kwenye chumba cha kuoshea mikono, safari hii waraka huo unaendelea kwa kumtaja mhudumu aliyetumika kuweka vitu hivyo.

Kupitia waraka huo alioutoa kwa ndugu na rafiki zake wa karibu, Dk. Mwakyembe anasema mhudumu aliyetumika bila kujijua ni wa kike kutoka katika kijiji cha Ipinda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya, ambaye alihamishiwa ofisini kwake. Inaelezwa kuwa mhudumu huyo aliletwa katika ofisi hiyo siku chache kabla ya siku ya kuweka sabuni na taulo jipya ofisini kwa waziri huyo.

“Nilipoona kuwa najikuna mfululizo mara baada ya kunawia sabuni hiyo, siku ya tatu nilikuwa na wazo la kupeleka vitu hivyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini nilipofika ofisini, vilikuwa vimeshatolewa,” anasema Dk. Mwakyembe kupitia waraka huo. Dk. Mwakyembe ambaye yuko nchini India kwa awamu ya pili ya matibabu, anasema alianza kumuuliza maswali ya kina mhudumu huyo ili kujua kwa nini vifaa hivyo viliondolewa ghafla wakati alivitumia siku moja, hakufanikiwa kupata majibu ya kina.

Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anadai katika mazingira ya kutatanisha, tena ndani ya muda mfupi tangu alipoanza kuathirika baada ya kunawia sabuni na kujifutia taulo hilo, mhudumu huyo wa kike alifariki na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. Tukio la kufariki ghafla kwa mhudumu huyo bila kuugua, limeacha maswali mengi sio tu kwa Dk. Mwakyembe, bali pia hata kwa rafiki zake wa karibu ambao wanaamini kwamba aliwekewa sumu.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kuhusiana na taarifa kwamba kuna mhudumu mmoja wa kike wa Dk. Mwakyembe alifariki zilithibitisha kuwa ni kweli.

Mmoja maafisa wa juu wa wizara hiyo, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake kuwa ni kweli mhudumu huyo aliyemtaja kwa jina moja la Sara Richard ambaye alikuwa akimsadia Naibu Waziri huyo alifariki Septemba 29, mwaka jana, na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. “Ni kweli kuna mhudumu mmoja ofisini kwa Dk. Mwakyembe alifariki mwaka jana. Ila sijui aliugua ghafla au vipi hilo sijui; isipokuwa ni kweli kwamba mwaka jana tulimpoteza mtumishi mmoja na tulimsafirisha hadi kwao Mbeya,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Akihojiwa na gazeti hili kuzungumzia waraka huo na tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alisema hajauona na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa jambo hili. Hadi sasa wingu zito limetanda kuhusu afya ya Dk. Mwakyembe. Wakati taarifa zisizo rasmi zikisema amepewa sumu, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Robert Manumba, amesema hajalishwa sumu.

Taarifa hiyo ya Manumba pia inatofautiana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Nahodha, aliyekaririwa jana akisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na kuikana taarifa ya Manumba. Manumba naye kwa upande wake, jana alisema kuwa tayari ameshawasilisha faili kwa DPP kuhusu sakata la Dk. Mwakyembe ili afungue kesi dhidi ya watu wanaodaiwa kutoa taarifa potofu kwamba waziri huyo amelishwa sumu.

Source: Tanzania Daima

Kumbe ilikuwa sumu?
 
Mwaka huu tutasikia Mengi na tatizo kubwa fedha za LOWASSS zinawachanganya watu wanaamua kuandika tu kutumia malipo waliyopewa. Nacho Kijua CCM siyo wajinga hawawezi kumpeleka mwizi,fisadi,jambazi,mhuni,malaya Ikulu.Ikulu ni mahali pa heshima.
 
WARAKA wa siri ulioandikwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, umezidi kuibua mambo mapya. Waraka huo ulioripotiwa mara ya kwanza wiki iliyopita na gazeti hili na kueleza mbinu, mahala ambapo waziri huyo anaamini aliwekewa sumu kupitia sabuni na taulo vilivyowekwa ofisini kwake kwenye chumba cha kuoshea mikono, safari hii waraka huo unaendelea kwa kumtaja mhudumu aliyetumika kuweka vitu hivyo.

Kupitia waraka huo alioutoa kwa ndugu na rafiki zake wa karibu, Dk. Mwakyembe anasema mhudumu aliyetumika bila kujijua ni wa kike kutoka katika kijiji cha Ipinda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya, ambaye alihamishiwa ofisini kwake. Inaelezwa kuwa mhudumu huyo aliletwa katika ofisi hiyo siku chache kabla ya siku ya kuweka sabuni na taulo jipya ofisini kwa waziri huyo.

"Nilipoona kuwa najikuna mfululizo mara baada ya kunawia sabuni hiyo, siku ya tatu nilikuwa na wazo la kupeleka vitu hivyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini nilipofika ofisini, vilikuwa vimeshatolewa," anasema Dk. Mwakyembe kupitia waraka huo. Dk.Mwakyembe ambaye yuko nchini India kwa awamu ya pili ya matibabu, anasema alianza kumuuliza maswali ya kina mhudumu huyo ili kujua kwa nini vifaa hivyo viliondolewa ghafla wakati alivitumia siku moja, hakufanikiwa kupata majibu ya kina.

Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anadai katika mazingira ya kutatanisha, tena ndani ya muda mfupi tangu alipoanza kuathirika baada ya kunawia sabuni na kujifutia taulo hilo, mhudumu huyo wa kike alifariki na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. Tukio la kufariki ghafla kwa mhudumu huyo bila kuugua, limeacha maswali mengi sio tu kwa Dk. Mwakyembe, bali pia hata kwa rafiki zake wa karibu ambao wanaamini kwamba aliwekewa sumu.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kuhusiana na taarifa kwamba kuna mhudumu mmoja wa kike wa Dk. Mwakyembe alifariki zilithibitisha kuwa ni kweli.

Mmoja maafisa wa juu wa wizara hiyo, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake kuwa ni kweli mhudumu huyo aliyemtaja kwa jina moja la Sara Richard ambaye alikuwa akimsadia Naibu Waziri huyo alifariki Septemba 29, mwaka jana, na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. "Ni kweli kuna mhudumu mmoja ofisini kwa Dk. Mwakyembealifariki mwaka jana. Ila sijui aliugua ghafla au vipi hilo sijui; isipokuwa ni kweli kwamba mwaka jana tulimpoteza mtumishi mmoja na tulimsafirisha hadi kwao Mbeya," kilisema chanzo chetu cha habari.

Back
Top Bottom