Siri ya waraka wa Mwakyembe yafichuka; Kisa ni kifo cha ghafla cha mhudumu ofisini kwake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya waraka wa Mwakyembe yafichuka; Kisa ni kifo cha ghafla cha mhudumu ofisini kwake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 29, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  WARAKA wa siri ulioandikwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, umezidi kuibua mambo mapya. Waraka huo ulioripotiwa mara ya kwanza wiki iliyopita na gazeti hili na kueleza mbinu, mahala ambapo waziri huyo anaamini aliwekewa sumu kupitia sabuni na taulo vilivyowekwa ofisini kwake kwenye chumba cha kuoshea mikono, safari hii waraka huo unaendelea kwa kumtaja mhudumu aliyetumika kuweka vitu hivyo.

  Kupitia waraka huo alioutoa kwa ndugu na rafiki zake wa karibu, Dk. Mwakyembe anasema mhudumu aliyetumika bila kujijua ni wa kike kutoka katika kijiji cha Ipinda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya, ambaye alihamishiwa ofisini kwake. Inaelezwa kuwa mhudumu huyo aliletwa katika ofisi hiyo siku chache kabla ya siku ya kuweka sabuni na taulo jipya ofisini kwa waziri huyo.

  "Nilipoona kuwa najikuna mfululizo mara baada ya kunawia sabuni hiyo, siku ya tatu nilikuwa na wazo la kupeleka vitu hivyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini nilipofika ofisini, vilikuwa vimeshatolewa," anasema Dk. Mwakyembe kupitia waraka huo. Dk. Mwakyembe ambaye yuko nchini India kwa awamu ya pili ya matibabu, anasema alianza kumuuliza maswali ya kina mhudumu huyo ili kujua kwa nini vifaa hivyo viliondolewa ghafla wakati alivitumia siku moja, hakufanikiwa kupata majibu ya kina.

  Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anadai katika mazingira ya kutatanisha, tena ndani ya muda mfupi tangu alipoanza kuathirika baada ya kunawia sabuni na kujifutia taulo hilo, mhudumu huyo wa kike alifariki na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. Tukio la kufariki ghafla kwa mhudumu huyo bila kuugua, limeacha maswali mengi sio tu kwa Dk. Mwakyembe, bali pia hata kwa rafiki zake wa karibu ambao wanaamini kwamba aliwekewa sumu.

  Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kuhusiana na taarifa kwamba kuna mhudumu mmoja wa kike wa Dk. Mwakyembe alifariki zilithibitisha kuwa ni kweli.

  Mmoja maafisa wa juu wa wizara hiyo, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake kuwa ni kweli mhudumu huyo aliyemtaja kwa jina moja la Sara Richard ambaye alikuwa akimsadia Naibu Waziri huyo alifariki Septemba 29, mwaka jana, na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. "Ni kweli kuna mhudumu mmoja ofisini kwa Dk. Mwakyembe alifariki mwaka jana. Ila sijui aliugua ghafla au vipi hilo sijui; isipokuwa ni kweli kwamba mwaka jana tulimpoteza mtumishi mmoja na tulimsafirisha hadi kwao Mbeya," kilisema chanzo chetu cha habari.

  Akihojiwa na gazeti hili kuzungumzia waraka huo na tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alisema hajauona na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa jambo hili. Hadi sasa wingu zito limetanda kuhusu afya ya Dk. Mwakyembe. Wakati taarifa zisizo rasmi zikisema amepewa sumu, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Robert Manumba, amesema hajalishwa sumu.

  Taarifa hiyo ya Manumba pia inatofautiana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Nahodha, aliyekaririwa jana akisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na kuikana taarifa ya Manumba. Manumba naye kwa upande wake, jana alisema kuwa tayari ameshawasilisha faili kwa DPP kuhusu sakata la Dk. Mwakyembe ili afungue kesi dhidi ya watu wanaodaiwa kutoa taarifa potofu kwamba waziri huyo amelishwa sumu.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Afrika ndivyo ilivyo, hata akifa Mandela watasema eti na yeye kawekewa sumu na Frederick de Clerk.
   
 3. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Radhia Sweety haya mambo yapo, hii picha wewe hujaielewa tu???
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,191
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  anaielewa sana tu, sema tu kachagua upande wa kusimamia tena ana makusudi na malengo maalum.
   
 5. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wewe umenena mana kama unajifanya huu mchezo mzima huuelewi kwa kweli ni kwamba umeamua tu kujifanya hamnazo.
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,191
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  Jeshi la polisi mbona nao ni watuhumiwa?, kwa response ya manumba, mwenye busara anaweza kuiona ripoti ya jeshi hilo, itatofautiana na ya mwanzo kwa tarehe tu
   
 7. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kuna mtu alishawahi kuandika hapa jf kuwa Mwakyembe aliwekewa sumu kwenye sabuni..naendelea kuunganisha nukta..
   
 8. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ameshindwa katika ukweli, atasema nn wakati ameshkwa pabayaaaa
   
 9. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Manumba anabishana na Boss wake kwenye vyombo vya habari!!Huu ni utovu wa nidhamu. Boss anasema haitambui ripoti ya Manumba, Manumba anasema ameshawasilisha jalada la kesi kwa DPP linalotokana na ripoti yake ya kibabaishaji.

  Hii maana yake nini hasa??? Tumwamini nani??? Nchi hii inapita katika kipindi kigumu sana cha uongozi. Hivi huu unaoendelea sasa sio uhuni????????

  Yani watawala wamekuwa kama kambale, hajulikani nani mama, nani baba na nani mtoto, wote wanamijindevu. Nchi haiwezi fika kwa style hii ya uongozi. Mwenye nchi katulia tuliiii anatumbua mijiallowance tu ya safari za kimataifa!!!
   
 10. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kuna uwezekano kuwa alihusika kufanikisha huo ujasusi kwani waliofanya haya mambo wapo miongon mwetu.
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,191
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  "Tumedhubutu tumeweza na tunasnga mbele"
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,191
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Polisi halina uhalali wa kushughulikia jambo hili! Full stop
   
 13. R

  Rational Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe radhia hii unaishi dunia gani? hayo mambo yapo na si Africa tu Hata ulaya marekani na kila kona sema tu tunatofautiana katika kuyafatilia. Hiyo ni picha ambayo imechezwa, na wameakikisha vithibitisho vyote wanavipoteza ili ionekane ni uongo. Sijui tutafikia wapi kama hali ndiyo hii. Ee Mungu Tusaidie.
   
 14. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Jambo moja halijawekwa wazi. "Ni kwa nini harison ateswe kiasi hicho?"
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Epa, Richmond, KCM etc.. Kuna sehemu ya ripoti ilimfanya Lowasa ajiuzuru hakuimalizia kuisema kwa hofu kwamba nchi ingeyumba, labda watesaji wana wasiwasi siku moja ataimalizia. ANYWAY, nchi sasa imekuwa kama mnara wa baberi, wajenzi wa mnara ule walifika mahala kila mtu aliongea lake. Kuna matukio kadhaa ambayo yamesababisha viongozi kadhaa wabishane hadharani... POSHO ZA WABUNGE.. La Mwakyembe... Etc
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Hata atakayekufa kesho ukimwekea sumu leo maana yake kafa kwa sumu. Awe mzee, kijana au mtoto. NAHISI, WEWE KAMA SI MANUMBA, BASI UMETUMWA NA MANUMBA AU NI NDUGU YAKO AU KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NYUMBA NDOGO YAKE AU BILA YEYE MAISHA YA DUNIANI YATAKUSHINDA
   
 17. M

  MALAGASHIMBA Member

  #17
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Wee!!! Unazo kweli?
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Japo kwenye suala hili la kuugua kwa Dr. Mwakyembe, speculatios na conspiracy theories za kuwekewa sumu ndio the order of the day, nashauri msiziaminie sana hizi habari, nyingine ni 'tales' only!.

  Subirini report ya pili ya Apollo na ya uchunguzi maalum ya Nahodha itakayohusisha forensic investigation kwa sababu by the time ananawia hiyo sabuni na kufutia kile kitaulo, Dr was under heavy medication!. Ni vizuri pia tukajua alikuwa anasumbuliwa na tatizo gani kabla ya incident ya sabuni na kitaulo!.

  Mimi binafsi bado nasimama na taarifa ya DCI Manumba!.

  Kuna kitu kinaitwa "sensionalism" na vifo vya "amaizing coincidence"!.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Ingekuwa US hapa ingefanyika investigation ya maana saa hizi hadi sampuli za toilet zingeshachukuliwa! Ila maigizo tu! Drs hawajui manumba kapata wapi taarifa na kafanya uchunguzi wa makaratasi, manamba anashtaki wazushi as if it ever worked in bongo, na nahodha ana uchunguzi wa kina! Upele umepata wakunaji!
   
 20. k

  kuzou JF-Expert Member

  #20
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  habishani anachosema yeye si polisi na hafanyi uchunguzi na hawezi kuingilia uchunguzi wa polisi hivyo hawezi jua wamepata wapi hizo data,pili wanobishana kuhusu ugojwa wa mwakyembe sijui sumu,ripoti,sijui sabuni kwenye vyombo vya habari wanakosea sasa unataka rais naye aingie kwenye uchemfu huu,no research no right to speak sasa hao wanaosema lbd wanareseach zao
   
Loading...