Sijaiona hii kitu bado naona shughuli zimeingiliana..
Ila hawa jamaa inabidi wajue kwamba hata ukiwa na product nzuri vipi bila promotion ni kazi bure..
Sijui kwanini wasiamue hata kurusha episodes za mwanzo mwanzo youtube ili watu waweze kuangalia kwa wakati wao (hata kama itakuwa ni against contract na ITV) lakini ikiwepo online hata episodes za mwanzo zitawavutia wengine hata walio nje kuweza kuona (unless otherwise hii kitu inaweza kushika kasi na watu kuitambua baada ya miaka kadhaa ambapo huenda itakuwa imeshaanza kuchuja)
Ki ukweli wamejitahidi sana kujitangaza, matangazo yao yapo
sehemu nyingi mno hadi humu Jamii Forums, pia wana page kule
facebook na hata youtube...
Duh! kama huo ni uoga na uoga utakuwaje? Kosa la wazungu ni kutuaminisha kuwa wao wanajua tamaduni zetu. Kwamba tamthiliya ya kiafrika ina mahadhi ya kizungu. Uongeaji ule kiukweli sio. Nimependa sana kazi ya CREW. Pia nawe usiogope kuhusishwa na jambo unalolitetea. Nilidhani nawe uko kwenye crew ili nami nije kuiba ujuzi huko maana wamejipangaDah mkuu naona umetokelezea hatimaye, vipi za masiku?? Na heri ya Mwaka mpya!
Sijui kwanini toka naanzisha hii sred tu nilijua kuna mtu ataleta hoja za "wazungu" lol....
Naona wadau karibia wote mnamsimamo unaofanana juu ya hichi kitu maana nina kijana wangu mtaani naye ni mdau sana wa tasnia toka mwanzo nimemwambia acheki hii kazi kakazana oohh wazungu wazungu!!
Miaka yote tupo sisi kama sisi "wabantu" na tasnia yetu, na wote tunajua nini tumekuwa tunafanya, Bishop Hiluka kaandika wee kukosoa na kurekebisha lakini wapi, kazi zetu tunazijua wenyewe mpaka sasa.
Kosa hasa la hao "wazungu" ni nini hapo?
Kuwa na uwezo na kugharamia kukamilisha walichoona wao kinafaa kwa kupitia sanaa yetu?
Raia Fulani ushaanza uoga wako wa kunihisia vitu ambavyo havipo, mi pia ni raia fulani tu ambaye nina mguso wa kipekee na hizi sanaa.
Wa kwanza kulia hilo ni Mwalimu na msanii mzuri sana pale chuo cha sanaa Bwagamoyo kwa kweli jamaa ana kipaji
Leo nilikuwa naongea na dada mmoja aliyekuwa akiitazama hii tamthiliya na akasema kuwa hajapenda jinsi wasanii wanavyoongea mechanically. Wamemezeshwa script na wanaongea kama vile wanaogopa kukosea wakati katika uhalisia hayo sio maongezi, tena ya kiafrika. Hii naifananisha na filamu ya chumo. ​Nadhani waliotengeneza siri ya mtungi ndio waliotengeneza chumo
Nimependa sana kazi ya CREW. Pia nawe usiogope kuhusishwa na jambo unalolitetea. Nilidhani nawe uko kwenye crew ili nami nije kuiba ujuzi huko maana wamejipanga
Roho inaniuma sana ninapokuwa na wadau wanaojua na bado wanatetea vitu tu ilimradi kushinda ligi, ila uzuri wa kitu kizuri hata ukikipinga bado utajichanganya tu hebu cheki hapo chini ulivyotoa comment nzuri.... lol
Pamoja saaaaana bro!
Roho inaniuma sana ninapokuwa na wadau wanaojua na bado wanatetea vitu tu ilimradi kushinda ligi
Duh! kama huo ni uoga na uoga utakuwaje? Kosa la wazungu ni kutuaminisha kuwa wao wanajua tamaduni zetu. Kwamba tamthiliya ya kiafrika ina mahadhi ya kizungu. Uongeaji ule kiukweli sio. Nimependa sana kazi ya CREW. Pia nawe usiogope kuhusishwa na jambo unalolitetea. Nilidhani nawe uko kwenye crew ili nami nije kuiba ujuzi huko maana wamejipanga
Tukirudi kwenye tamthilia hii, sioni kama ina tofauti sana na tamthilia zingine za nje hasa
linapokuja suala la maudhui na matumizi ya movements: mfano mdogo ukiwa kwa wapenzi
na mikao yao; kwa mfano sisi (Waafrika) hatuna desturi ya kupeana visogo unapoongea na
mpenzi wako, lakini humo ni kawaida kumuona binti kusimama akiwa kasimama kampa kisogo
mpenzi wake halafu wanaongea. Au pale mtu anapomuuliza rafiki yake
usishangae kuona jamaa anamletea mpenzi wake maua akiwa kayaficha mgongoni na kusema
"surprise!".
Yani umeeleza vizuri mno! We ni mchambuzi wa kweli. Gwalu nae inabidi aanze kuitazama hii tamthiliya kwa jicho la tatu. Halafu kumbe nilipatia kufikiri kuwa hawa ndio waandaaji wa chumo? Kiukweli zinafanana MNO! Pozi ni zile zile. kukakamaa kwa stori ni kule kule... Ila bado naendelea kukiri kuwa CREW iko njemaMkuu, Wachina wana msemo wao kuwa: "kama kila mnapokutana huwa mnakubaliana
kwa kila jambo basi baadhi yenu wana matatizo ya kufikiri". Ni kawaida kutofautiana
hasa ukizingatia kuwa kila mmoja ana angle anayoitumia kuangalia jambo. Binafsi naweza
kusema kuwa in terms of equipments, quality, cast, story na jinsi ya mgawanyo wa kazi
jamaa wamejitahidi sana kwa kuwa walijiandaa kabla ya kuanza kazi. Bajeti yao ni kubwa
mno kwa kuwa walipata funds kutoka kwenye taasisi mbalimbali za nchini kwao (Marekani)
na hapa nchini.
Pamoja na uzuri wa kazi husika lakini hilo la uzungu ki ukweli limo sana. Llilikuwemo hata
kwenye filamu ya chumo kwa kutuwekea mashindano ya vijana wawili (Sharo na Mlela)
kumgombea binti (Jokate) huku baba wa binti ndiye akiwa referee.
Tukirudi kwenye tamthilia hii, sioni kama ina tofauti sana na tamthilia zingine za nje hasa
linapokuja suala la maudhui na matumizi ya movements: mfano mdogo ukiwa kwa wapenzi
na mikao yao; kwa mfano sisi (Waafrika) hatuna desturi ya kupeana visogo unapoongea na
mpenzi wako, lakini humo ni kawaida kumuona binti kusimama akiwa kasimama kampa kisogo
mpenzi wake halafu wanaongea. Au pale mtu anapomuuliza rafiki yake "vipi ulitumia kondomu?"
wakati tamthilia hii inaangaliwa na watu wa rika zote wakiwemo watoto wadogo. Kwangu mimi
haya ni mapungufu ya kimaadili, hata kama ni utandawazi lakini bado hatujafikia huko. Pia
usishangae kuona jamaa anamletea mpenzi wake maua akiwa kayaficha mgongoni na kusema
"surprise!".
Kwa hiyo kama wadau wanapinga ni kwa sababu wao hawaangalii ubora wa picha au sauti tu,
au kumwangalia mtu mmoja mmoja kama huyo mzee Nkwabi wa Bagamoyo, bali katika angle
waliyoitumia kuna vitu vinawaudhi kiasi cha kuwafanya wasiyaone hata hayo mazuri mengine.
Mwisho, kila mtu huwa ana hobbies (vitu avipendavyo) na vitu asivyovipenda, na huwa
tunatofautiana katika mitazamo, hivyo anaweza asiyaone kabisa hayo unayoyasema wewe
kuwa ni mazuri. Najua wanakukera lakini ukweli utabaki kuwa hivyo...
Actually umeelewa angalau. haimaanishi tulazimishe kuangalia kazi za kwetu japo mbovu. Kwanza tuna mapungufu katika uandikaji wa stori zenyewe. Pili hatuna utaalam wa kutosha kama wazungu. Tatu bajeti zetu finyu sana. haijawahi kutokea hapa mtu akatengeneza filamu iliyogharimu mil 50. sasa kitu kama chumo na siri ya mtungi ni zaid ya mil 200 hivi. Hayo ndio yanayowafanya hawa wenzetu kuja kuamini kuwa hata itikadi na tamaduni zetu wanaweza kuzilipiaDuh labda sijaelewa wakuu ndio maana nashindwa kuelewa huu mjadala na uhusiano baina ya wazungu (na ubovu au ubora wa kazi zetu), nadhani hapa ni kusingizia uwepo wa bunduki kwa mauaji badala ya aliyeitumia hio bunduki..
Sijaelewa kama unasema kwamba watu hawaangilii kazi zetu sababu sio za kizungu au waigizaji wanaigiza uzungu.., kama ni hivyo nadhani tunawaonea hao wazungu (kwa ufupi ni mediocrity ya wanasaa na kazi mbovu za kurashiarashia za wabongo ndio zinazosababisha kazi mbovu)
Nimeangalia kazi nyingi za sehemu tofauti na hata kuna kazi za huko huko kwa wazungu ambazo nyingi naacha kuziangalia sababu tu ni mbovu na sio sababu nyingine.., pia kuna kazi za watu wa kawaida mfano wa-Brazil walipotoa The City of God (kuonyesha reality ya nchini kwao kazi ilipendwa dunia nzima bila kujali ni wapi ilitoka) au kuna kazi nzuri kutoka Afrika Kusini n.k.
Nadhani hapa tunaweza kujikuta tunatumia neno Uzalendo kulazimishana kuangalia makapi sababu tu yametoka nyumbani au ni vijana wa nyumbani ndio wametoa hayo makapi (tatizo kubwa na wabongo ni over-acting na hii sidhani kama walifundishwa au wanaiga hao wazungu) sababu hata hao hawafanyi hivyo
Samahani kama sijaelewa huu uhusiano wa kuwalaumu wazungu au kazi za wazungu kwa kutoa kazi zetu mbovu (labda sijakueleweni au nimekosea) mnamaanisha nini
Najua wanakukera lakini ukweli utabaki kuwa hivyo...
Mkuu, labda tutafute focus maana tumekuwa tukiongelea vitu vingi mno,Hapana Mkuu hapo umekosea!
Hebu we mwenyewe angalia unazungumzia suala la mkao wa wapenzi, kweli??
Tuongelee maudhui yaliyoko kwenye script pamoja na uwasilishaji wa hiyo script. Tuachane na technical part of itMkuu, labda tutafute focus maana tumekuwa tukiongelea vitu vingi mno,
ungependa tujikite kwenye kuangalia nini? Inawezekana naongea vitu vingi
nikajikuta naacha mada ya msingi ambayo wewe umeikusudia. Suala la
mapenzi nililoliongelea lina maana sana unapotaka kuzama kwenye maudhui.
Haya niliyoyaongea kwenye tamthilia hii ndiyo nimekuwa nikiyapigia kelele haya
kwenye movie zetu. Tena yameshakuwa ni kitu cha kawaida siku hizi. Anyway,
labda tuongelee nini...
Mkuu, makosa mawili hayawezi kuhalalisha jambo. Huu usharobaro naMkuu hivi haya siku hizi hayatokei kwenye hii karne ya dot.com na hawa vijana wetu ? kama mtu ana-act kama sharobaro (kama wenyewe wanavyojiita unategemea kwenye ku-act abadilike awe kama mstaarabu fulani au mtoto mwenye malezi ?
Kwahio mkuu ingawa na mimi naona kasoro nyingi sana kwenye Bongo Movie hadi kupelekea nisiziangalie sana lakini nadhani kwa mfano hapo juu tutakuwa tumewaonea.., nadhani hapo labda tuwalaumu watunzi kwanini wasitengeneze na filamu zinazohusu sana maisha ya watanzania na mila na desturi ili nazo ziingie sokoni sababu unajua watu wanaangalia soko na huu usharobaro ndio soko la vijana wetu (kwahio watengeneze na tamthiliya za familia na nyingine zinazohusu mila zetu)
Mkuu sijasema kwamba hakuna makosa ila hayo uliyosema ni makosa sioni kama ni makosa.., different strokes for different folks na sababu movies zinareflect jamii tunayoishi basi since vijana wetu ndio wanavyoishi mitaani kwanini hata wabunifu wabadilishe ?, ndio kuna watu wanaoishi kwa maadili tofauti basi watunzi watengeneze movies za maadili tofauti pia.., hii ni kama watu wanaosema nyimbo nyingi ni za mapenzi (kama basi nyimbo nyingi ni za mapenzi ubaya haupo kwenye nyimbo za mapenzi bali ni wingi wake) kuna themes tofauti na ubaya haupo kwenye themes labda upo kwa watunzi kusahau themes zenye mafunzo na utamaduni wetu (ingawa hata hizo themes nyinginezo sio mbaya sababu zina nafasi yake)Mkuu, makosa mawili hayawezi kuhalalisha jambo. Huu usharobaro na
hayo mengine unayoyasema ni mambo ambayo nimekuwa nikiyapigia
kelele kila siku.
Na mimi pia sijaangalia hizi movies na muda mwingi naona matatizo yapo kwenye plot mbovu wala hazina substance..., yaani story nyepesi nyepesi ambapo naona kwenye nchi yenye historia na utamaduni mkubwa kuna Gap kubwa sana kwa watunzi kuweza kupata stories za nguvu.. (tatizo sio acting pekee, bali ni utunzi mbovu na story nyepesi nyepesi) na mimi suala la gharama naona kama ni kisingizio tu kuna movies zilikuwa blockbuster kwa kutumia pesa ya kawaida tu, alafu mkuu nadhani hatujaelewana kwenye issue ya mambo ya weledi (nimesema kama actor ana-potray Sharobaro au kijana wa sasa wa mtaani) unategemea ata-act tofauti na kujifanya mtu wa weledi.., kwahio mkuu hapa kosa ni watunzi na wanaoandika script kutokutoa movies za weledi (sio kwamba kila movie ambayo haina weledi ni mbaya)Sote tunayajua matatizo makubwa yaliyopo kwenye
movie zetu za Bongo ambazo kiukweli nyingi (90%) sijawahi kuziangalia
japo mimi ni mdau mkubwa. Siziangalii kwa kuwa najua nitakerekwa baada
ya kuziangalia, hivyo tusipende kulinganisha Bongo movie na kazi za watu
wenye weledi, waliojiandaa kwa kila hali na waliowekeza gharama kubwa.
Kwa hiyo unataka kuniambia kama Bongo Movie wanafanya mambo haya basi
hata wenye weledi ni ruksa kuyafanya?
Mwisho, labda niweke wazi, binafsi waliotengeneza hii kazi ni rafiki zangu,
nimeshafanya nao kazi, pia nilikuwa na mkataba nao wa script ambao umekwisha
December 31, 2012, na sasa niko huru lakini kuna kazi nyingine tumekubaliana kufanya
baadaye mwaka huu kama Mungu akipenda na kama tutafikia makukubaliano. Haya
ninayoyachangia humu huwa nawaeleza hata wao wenyewe physically, bila unafiki wala
kuongopeana na wao huwa wananipa ufafanuzi, na mwisho wa siku tunamaliza mjadala...
Mkuu, nakubaliana na wewe katika mambo mengi ila pengine tofauti yetu ni lughaNaam sasa kumbe hapa ndio tumegundua ubaya na tatizo la hii tasnia yetu kutokuwa na movies za kutosha zenye themes tofauti na zenye stories zilizokwenda shule.., sababu nyie mnaoandika script zinapwaya.., mkuu umeshaandaa movies ngapi au script ngapi zenye utamaduni na weledi kama wewe unaosema..? nina uhakika ukiandika kama hii watu wataangalia na kuna Gap kubwa kwenye soko la movies kama hizi..