Siri ya maendeleo ya taifa masikini kuinuka

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,023
12,315
Siri muhimu kwa taifa masikini kuinuka kutoka katika dimbwi la umasikini.

Hii siri ambayo viongozi na wananchi wengi wa mataifa masikini hatupo tayari kuipokea na kuikubali.

Kama taifa tunataka tutoke haraka hapa tulipo kuna siri moja ya muhimu sana ambayo tunapaswa kuifahamu na kuikubali hata kama itapingana na mawazo na fikra zetu kwa kiasi kikubwa.

Maendeleo ya taifa ya haraka ni safari ya maumivu na machungu mengi sana ni safari iliyo jawa na miba mingi sana.

Hakuna maendeleo ya taifa yayoletwa kwa sisi kupiga domo tu bila kusacrifice miili yetu na roho zetu kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

Tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati kwa mapenzi ya taifa letu liwe strong kuliko lolote ili tusirudi utumwani tena.

Mapambano haya sio kwamba yana hitaji mioyo ya dhati ya viongozi pekee la hasha hata wananchi wote kwa pamoja wakubwa kwa wadogo lazima tupambane bila kukata tamaa.

Tufanye kazi kwa bidii kwa maendeleo ya taifa kama vile kesho haipo.

Napenda kuwapa mifano ya hii jamii ya wakorea, wajapan, wachina hawa watu wanafanya kazi kuliko kawaida kama umewahi kufanya kazi na hii jamii utaelewa nini maana ya kufanya kazi kama vile kesho haipo ikiwezekana mtafute moja wapo kati ya mkorea, mjapan, mchina na uchunguze spirit yake ya kazi.

Hawa watu wanajenga nchi zao kwa dhati ya mioyo yao bila mashinikizo ya viongozi wakipanga wapambane wafanye hili au wawe pale watapambana kwa jasho na damu mpaka taifa linafanikiwa.

Kwa msaada wa kihistoria juu ya hawa watu miaka walio sacrifice maisha yao kwa maendeleo ya taifa lao umetawaliwa na maumivu na machungu mengi sana mfano:-

i. Taiwan (miaka ya 1960- 1990 )
ii. Japan (miaka ya 1860- 1990 )
iii. China (miaka ya 1950- 2000)
iv. Korea (miaka ya 1970-1990/2000)
V. Singapore (miaka ya 1960- 1990 )

Hio ni michache tu ya kugusia kwa atakae taka kujifunza.

Mazee hawa watu wanafanya kazi na wana spirit kutaka kuona nchi zao zinafika juu sio viongozi sio wananchi.

Hii jamii inatoa funzo kubwa sana kwetu kama tukiamua kuwa serious na kujifunza spirit yao lakini lazima tuhakikishe kweli tunaipenda nchi yetu na tunataka nchi yetu iwe giant of Africa na dunia.

Jambo la kufurahisha zaidi hawa watu hufikia mpaka hatua ya kulia kwa machozi mengi kwa uchungu juu ya nchi especially hao wachina ni mara nyingi sana nimeshuhudia hili mapenzi yalipo pitiliza kwa nchi hawa ndio wanayo.

Bila kukubali maumivu ya ujenzi ya nchi yatupitie hakika hatuwezi kufanikiwa kamwe maendeleo ya haraka hayaletwi kwa kupiga sogo na kelele za majukwaani.

"Siku zote nchi inapo piga hatua kubwa kimaendeleo wananchi wenye true spirit ulia kwa uchungu pale wimbo wa taifa unapo pigwa ukiwakilisha machungu yao katika ujenzi wa nchi".

R.I.P mashujaa (mabibi na mababu) wote mliopinga utumwa na ukoloni mpaka teno la damu la mwisho🕊️.
 
Watu wanafanya kazi matokeo yake watawala mali za umma wanazitumia kwa anasa, bora tukose wote, unakuta DC/DED/DAS wanaenda safari moja kila mtu na V8 lake mafuta, posho yake na dereva, kwanini wasitumie gari moja na wote ni watumishi wa umma na wanaenda sehemu moja? Tanzania haina shida ya pesa ina shida ya matumizi mabaya na ufisadi, hakuna haja ya kufanya kazi
 
Sema nini kweli viongozi wetu wana tumbua pesa mpaka sio poa
 
Umeandika ukweli mtu mtupu, nani sasa wa kuongoza hizo harakati manake kwa mataifa ya watu weusi ni adimu kumpata kiongozi mwenye moyo wa kuwavusha watu kama hizo tiger economy countries
Ni wananchi kuungana kwa pamoja na kufanya mabadiliko makubwa
 
Upo sahihi ila kwa rasilimali tulizonazo ilitakiwa kila mtu awe anakula kiyoyozi huko ulaya mda huu tupo vacation, we usiwaone waarabu wanataka kumiliki bandari tu, wanajua wanachokitafuta kina maslahikiasi gani
Rasilimali zinahitajika nguvu kazi zetu zote
 
Ukweli ni kwamba rasilimali watu wenye akili ndio Siri kubwa ya mataifa ya Ulaya,America na Asia kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Taifa la watu wajinga huzalisha viongozi wajinga maana kharamu haiwezi kuwa hali, ndivyo hivyo halali haiwezi kuwa kharamu,na waafrika tuna sifa ya ujinga ndio maana kila kitu ni hovyo ukitaka kuthibitisha hili angalia Tanganyika ya mkoloni na Tanganyika ya kina Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete,John na sasa Samia,angalia South Africa ya Makaburu na, sasa ya waafrika,angalia Zimbabwe ya mkoloni naya sasa waafrika ni mbingu ma ardhi katika nyanja zote.

Tungepata viongozi kama Emperor Meiji wa Japan au Deng wa China tungekuwa mbali sana katika bara hili.
 
Umeandika ukweli mtu mtupu, nani sasa wa kuongoza hizo harakati manake kwa mataifa ya watu weusi ni adimu kumpata kiongozi mwenye moyo wa kuwavusha watu kama hizo tiger economy countries
Tunao watu kama akina January makamba, Nape,Mwigulu n.k naimani watatupeleka huko.
 
Ukweli ni kwamba rasilimali watu wenye akili ndio Siri kubwa ya mataifa ya Ulaya,America na Asia kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Taifa la watu wajinga huzalisha viongozi wajinga maana kharamu haiwezi kuwa hali, ndivyo hivyo halali haiwezi kuwa kharamu,na waafrika tuna sifa ya ujinga ndio maana kila kitu ni hovyo ukitaka kuthibitisha hili angalia Tanganyika ya mkoloni na Tanganyika ya kina Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete,John na sasa Samia,angalia South Africa ya Makaburu na, sasa ya waafrika,angalia Zimbabwe ya mkoloni naya sasa waafrika ni mbingu ma ardhi katika nyanja zote.

Tungepata viongozi kama Emperor Meiji wa Japan au Deng wa China tungekuwa mbali sana katika bara hili.
Ni kweli tuna shida nyingi sana ndani yetu ambazo tunabidi kukubali kuzibali kwa njia yoyote ile inayowezekana
 
Ukweli ni kwamba rasilimali watu wenye akili ndio Siri kubwa ya mataifa ya Ulaya,America na Asia kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Taifa la watu wajinga huzalisha viongozi wajinga maana kharamu haiwezi kuwa hali, ndivyo hivyo halali haiwezi kuwa kharamu,na waafrika tuna sifa ya ujinga ndio maana kila kitu ni hovyo ukitaka kuthibitisha hili angalia Tanganyika ya mkoloni na Tanganyika ya kina Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete,John na sasa Samia,angalia South Africa ya Makaburu na, sasa ya waafrika,angalia Zimbabwe ya mkoloni naya sasa waafrika ni mbingu ma ardhi katika nyanja zote.

Tungepata viongozi kama Emperor Meiji wa Japan au Deng wa China tungekuwa mbali sana katika bara hili.
Kuna vitu vyengine vipo ndani ya uwezo wetu wala sio kwa sababu hatuna akili kama hao wenzetu, ni watu ambao hatuna utashi na hatupo serious tu kwenye suala la maendeleo. Kuna watu wengi waliyokuwa na elimu na wapo vizuri kichwani ila kuingia serikalini tu wanabadilika inakuwa kama wameingia ulimwengu mwengine ambao hauhitaji hizo akili zake.
 
Back
Top Bottom