Nimekuwa na uhusiano niseme km mchumba au mpenzi ndani ya miaka 12, tumejaliwa watoto wawili, wakike na kiume, maisha niliyoishi na huyo mtu km sio uvumilivu basi sina Jina la kulipatia sahihi, kwanza ni vile
Nilizaa nae nikawa naogopa sana kutengana nae, na yeye alitumia huo udhaifu wangu ipasavyo, mbinfsi, mnafki, mchoyo, kiburi Yaani wkt mwingine mwanamke
/mwanaume ukiishi na mtu wa namna hii ata unatamani ufanye jambo baya iLi maisha yako yawe na amani, ndugu zangu walinionea huruma
Sana, ila kwakuwa nilikuwa naogopa sana kuwatenga wanangu na baba Yao wakiwa wadogo, na kuanza uhusiano mwingine ambao sijawahi ujua pia, nilivumilia sana, anapokosea kitu mfano umemfumania na mwanamke au umeona kurudi kwake usiku wa manane sio sahihi ukamweleza kwa upole sio tabia njema kunitendea hivyo na watoto wanaona unachokifanya, atakujibu kwani nimekuoa, si tumezaa tu!! Unaweza kuendelea na maisha yako ukiona nakusumbua na "maisha yangu" well mi ni mwombaji sana, nilimuomba sana Mungu anipe nguvu ya kutojali hayo, nilipata chuo uk na nikaja kusoma hapa miaka 2, nikamuacha na watoto ! Akaona watoto wanamsumbua sana kuwa huru atakavyo, akawapeleka kwa mama yangu, mara Ampeleke pesa za matunzo mara aseme kwani huyo wa ulaya kazi yake
Nini uko, atume yeye, Ukweli Mungu alinipa neema ya ajabu , nikaanza kufanya vibarua hapa ulaya na shule pia, baadae nikaomba wanangu waje kunitembelea, walipoingia tu , nikaomba kuongeza muda wa kusoma , wkt huo haukuwa ngumu km sasa , kwahiyo hata watoto wangu waliweza kubaki na kuanza shule hapa uk. Nilipomaliza shule yangu nikapata kazi hapa uk , Ukweli nimeuona mkono wa Mungu ,wanangu sasa wako university na wanafanya vizuri sana, hutanielewa kabisa Nilikuambia sijawahi tena jiingiza kwenye mahusiano na mwanaume
Kwanza kwa uoga,
Pili maumivu niliyo pitia?tatu wanangu bado wananijihitaji kuliko yeyote Yule duniani? Sio kwamba sijawahi kujaribu? But kwa vile niling'atwa na nyoka hata nikiona unyasi tu nakimbia, bahati mbaya hayo nimepitia ndani ya usichana wangu wote, sina ushuhuda mzuri juu ya suala mahusiano, na hapo haya ndoa haikufungwa!! Kwavile mwenzangu ye kila
Siku anakuambia hajaamua kuoa bado , mtu km mimi bado nataka tena ndoa jamani!!! BIG NO, ndio
Maana nikiona mtu km mtoa mada hapo juu Ukweli najizuia sana kutoa koment Kali , but all in all maisha yanaebdelea na nina furaha zaidi ya muda wote
Nilipokuwa kwenye mahusiano.
Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha