Siri kubwa ya CCM kushindwa ni wananchi kuichoka kutokana na utawala mbovu wa Jakaya Kikwete na kundi lake la wezi Kikwete amekuwa na kasumba za kunawa lawama kuonekana kiongozi madhubuti kwa kuwafanya wanamtandao wamsifie na kumlaumu Mkapa kuwa alikuwa mwizi wakati na yeye Kikwete ni mwizi mkubwa kupitia Lowassa, William Ngereja na Rostam Azizi. kutokana na pesa za wizi wa kuibia serikali uchumi wa Tanzania umeyumba na kusababisha mfumuko wa bei mkubwa kuliko nchi yeyote ya ukanda wa Afrika Mashariki na kati ukitoa Zimbabwe
Sasas hivi pesa ni ngumu kupatikana na ukiipata haina thamani tofauti na wakati wa Mwinyi ingawa pesa haikuwa na thamani vilevile ilikuwa rahisi kuipata, vivyo hivyo wakati wa Mkapa pesa ilikuwa ngumu kuipata lakini ilikuwa na thamani mara uitiapo mfukoni. Kwa sasa mfumuko wa bei juu, ajira hakuna, uuzaji wa bidhaa nje umepungua, huduma za jamii zimedorola shule hazina madawati, mahospitali hayana dawa, umeme wa mgao kupindukia na mfumo wa maji ya kutumia mbovu. kilichobaki Kikwete kabaki kutaja urefu wa barabara kana kwamba barabara za lami ni muhimu kuliko ajira pia kuwawezesha kiuchumi wananchi.
Kikwete na serikali yake ya kihuni inabidi atambue kuwa bila ajira na kuwawezesha wananchi urefu wa barabara za lami anazojenga hzina thamani ingawa barabara za lami ni muhimu lakini ajira ni ya kwanza kabla ya barabara ya lami maana mtanzania anaweza kuishi kwa barabara zilizopo lakini hawezi kuishi bila ajira