CCM wakubali kwamba wameshindwa kihalali na ni kwa sababu wamepoteza mvuto. Kuna mengi sana ambayo yanakatisha tamaa wananchi kwa kuwa wanaona wabunge wao mambo wanayoyafanya Bungeni ambayo ni ya aibu.
Wanamkomoa Lowassa, kwani aliwalazimisha CC wampitishe Sioi? Wakati Sioi anapitishwa, Lowassa alikuwa Ujerumani.
Kama walikuwa wanamkomoa Lowassa ilikuwaje, Secretariat ya NEC ihamie Arumeru? Ambaye sikumuona huko ni Chiligati na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar. Lakini wengine wote walikuwa huko kuanzia Mukama, Makamba, Nape, Yule mama Mzanzibari (Asha Abdallah) na Mwigulu. Bado Msekwa naye alikuwa huko.
Mawaziri Wasira, Nagu, na Medeye walikuwa huko. Wabunge kibao wa CCM walikuwa huko. UVCCM uongozi wa Taifa, Mkoa, na Wilaya karibu zote za Arusha na Kilimanjaro walikuwa huko. UWT Taifa nao walikuwa huko na ahadi za kuwapa mikopo akina mama.
Sasa kama CCM ilikuwa inamkomoa Lowassa ilikuwaje itume jeshi lote hilo la Jumuiya zote za chama, uongozi wa Taifa wa CCM, na mawaziri juu.