Yaani mapenzi yanakuwa hot inatokea hadi kufa mnaweza msipishane hata mwaka.
Mwanamke uliyemtoa bikra ukimjali hata kama huna hela za magorofa na magari si rahisi kuchepuka. Lakini upande wa pili ni kucheza na shilingi chooni.
Embu sikia hii stori ya kweli kumhusu Dada yangu ambayo bila shaka anasadifu wanawake wengi duniani.
Ilikuwa ni harusi ya Dada yangu, Miaka mitano iliyopita. Dada alikuwa amerembwa akarembeka. Kila mmoja home alifurahi nikiwamo mimi. Yalikuwa ni mafanikio ya familia yetu kuona dada yetu akiingia katika ulimwengu wa ndoa. Siku ya Harusi iliwadia. nderemo na shamra shamra zilitawala. Wenye madera walikuwepo, suti haya, magauni ya gharama nao hawakuwa nyuma basi ilimradi harusi ifaane. Matarumbeta na ngoma ziliwafanya waalikwa kuiona siku ile hakuna nyingine ingefuata kumbe ni hisia tuu za furaha.
Tulikuwa ukumbini, maputo na vitu kama unyoya unyoya vilikuwa vikiranda randa mule ukumbini mwa kanisa. Dada yangu alikuwa kapendeza sana. Alivalishwa gauni jeupe kubwa ungedhani asingeweza kuliburuza. Muda mwingi alikuwa kajificha kwa aibu ndani ya shela. Wengi walitaka afunuliwe ili wamuone vizuri lakini wakumfunua alikuwa ni mmoja naam ndiye huyo shemeji yangu aliyekuwa anamuoa.
Muda wa kula viapo uliwadia, sikuamini nilichokiona. Nilimuona Dada akilia kwa hisia kali sana hali iliyompa tabu mshenga wake kumfuta kila mara machozi yake. Moyoni nilijiuliza badala dada afurahi anaolewa yeye analia, ni furaha gani kupitiliza hiyo.
Hatimaye ndoa ilifungwa na historia ikaandikwa.
Baada miezi kadhaa kupita nilienda kumtembelea Dada yangu. Nilipofika tulipiga soga za hapa na pale. Nyingi zilikuwa ni kukumbuka baadhi ya matukio ya harusi yake. Alinionyesha baadhi ya picha na mwisho aliweka CD ya harusi yake. Ndipo nikakumbuka kumuuliza kwa nini alilia siku ile kwa hisia kiasi kile. Hii ni Baada ya kuona kipande kikimuonyesha akilia kwa kwikwi.
Sio Mimi tuu hata wewe usingeamini jibu alilonipa. lilikuwa jibu lililopasua mishipa ya moyo wangu na kufanya mwili kufa ganzi. Aliniambia kuwa alilia kwa sababu hakuamini kama kweli Allen hatamuoa. Binafsi sikumjua huyo Allen zaidi ya Shemeji aliyefunga naye ndoa siku ile. Aliongeza kusema; kilichoniliza si furaha ya kuolewa bali hakuamini ni kweli Alleni mwanaume aliyempenda kwa dhati kuwa hatamuoa tena.
Binafsi nilishikwa na kigugumizi.
mkuu stori hii inahusu wadada wengi wanaoolewa. Wewe wakati unadhani mwanamke unayemuoa analia kwa furaha siku ukiwa kanisani. Kumbe mwenzako analia kutokuamini kuwa hivi ni kweli hatakuwa tena na Ex wake.