Siri ya Chuki ya Mwigamba dhidi ya Zitto Kabwe

Kasegela

Senior Member
Joined
Mar 24, 2019
Posts
127
Reaction score
261
MAUMIVU YA MWIGAMBA KWA ACT-WAZALENDO BAADA YA KUTELEKEZWA NA CCM NDIYO YANACHOCHEA CHUKI ZAKE DHIDI YA ZITTO KABWE.

Samson Mwigamba ni mwanachama wa CCM. Kabla ya hapo alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo. Mwigamba aliasisi ACT akitokea Chadema ambako alipata kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha. Historia yake ya nyuma kisiasa si mihimu kwa andiko hili leo.

Utajua Mwigamba ni Mwayaona wa pili kwa kutazama rekodi. Je, aliondokaje Chadema kwenda kuanzisha ACT? Mwigamba alifukuzwa Chadema. Sababu ya kufukuzwa Chadema ni kuandika waraka wa kumwandaa na kumtengeneza Zitto Kabwe kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Zitto alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mwigamba aliona ndiye kiongozi mwenye kufaa kuongoza chama. Mwigamba aliandika kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, uwezo wake ulikuwa umefika ukingoni. Mwigamba alindika "Mbowe ana akili ndogo", Mwigamba aliandika "Zitto ana akili kubwa kuliko Mbowe".

Ni dhahiri Mwigamba alimpenda na kumwamini sana Zitto. Andiko la Mwigamba, maarufu kama Waraka wa Mabadiliko, lilinaswa na viongozi wa Chadema mwishoni mwa mwaka 2013. Ikabainika kuwa Mwigamba aliandika, Prof Kitila Mkumbo, alihariri waraka huo.

Oktoba 2013 Mwigamba alitimuliwa uenyekiti Mkoa wa Arusha, kisha Novemba 2013 alifukuzwa uanachama pamoja na Prof Kitila. Mwaka 2014, ndipo alipoanza michakato ya kuanzisha ACT. Mwigamba akawa Katibu Mkuu wa ACT.

Novemba 2014, Kamati Kuu Chadema ilipomhoji Mwigamba kuhusu waraka huo, alikiri kuandika. Akasema alifanya hivyo bila kumshirikisha Zitto. Kwamba mpaka wakati waraka unabainika, yeye na Prof Kitila walikuwa hawajamshirikisha Zitto.

Inafahamika kuwa Zitto aliingia kwenye matatizo na Chadema kwa sababu ya waraka wa Mwigamba. Kumbe Mwigamba ndiye aliyemchonganisha Zitto na Mbowe kutokana na waraka wake. Ooh, Mwigamba mahaba yake kwa Zitto yalizidi mpaka akaandika waraka kumkashifu Mbowe ili Zitto awe Mwenyekiti wa Chadema.

Unapofika hapo unakuwa huna cha kubisha tena kuwa Mwigamba anampenda Zitto. Mwigamba anamhusudu Zitto. Mwigamba anamkubali Zitto. Mwigamba haambiwi chochote kuhusu Zitto. Mwigamba akilala anamuota Zitto. Mwigamba akinywa maji anamuona Zitto kwenye glasi!

Mwigamba alifanya kazi kuanzisha ACT. Hilo hakuna wa kulipinga. Wakati chama kikianzishwa Zitto alikuwa bado Chadema. Nyakati za aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa ACT, Kidawi Limbu, kutaka kuzuia Zitto kujiunga na chama hicho, Mwigamba alipambana naye vikali. Mwigamba alikuwa tayari "afe beki afe kipa", Zitto ajiunge ACT. Unawezaje kusema kuwa Mwigamba hampendi Zitto?

Basi, Zitto naye akajitahidi kumjali Mwigamba. Akampa gari la kutembelea. Zitto akampiga Mwigamba "sopsop", angalau akaanza kung'ara, ingawa alimeremeta sana kwa sababu alipenda kuvaa zile nguo za kung'aa sana. Nguo ambazo ukipita Tandika, mtu akikutana naye kwa mara ya kwanza, jioni akikutana naye tena, atamkumbuka haraka sana katikati ya maelfu ya watu.

Siwezi kusema kuwa ni nguo za kishamba. Ila, akitokea mtu akasema Mwigamba hupangilia nguo kishamba, siwezi kumpinga. Naanzaje kumpinga kwa mfano! Ni kwa sababu ujanja na uelewa wa Mwigamba ni mpaka kuutafuta kwa darubini. Shida ya kubwa ya Mwigamba ni kutojitambua. Ni mshamba lakini anajidanganya ni mjanja. Ana upungufu wa busara, ila anadhani ana busara. Hekima zimempita kushoto, mwenyewe anajiona Suleiman.

Matunda ya kujengwa akaanza ya kuyatumia vibaya. Akaanza kuwadanganya warembo kuwa angewapa nafasi za ubunge viti maalum. Katika hivyohivyo viti maalum, alitaka kumuweka na mkewe, Lilian Mwigamba. Yaani alishaona chama mali yake. Viti maalum ateue mkewe na mahawara zake. Mwigamba ni sheeeda!!! Kichwa cha Mwigamba kina upungufu wa vitamini aibu. Kwa hiyo hana aibu.

Na ukishaona binadamu hana aibu huyo kaa naye mbali. Mwigamba ni wa kukaa naye mbali. Mwigamba anataka shida zake zote za kimaisha zitibiwe na siasa, halafu na wanawake awabadili kwa jina la siasa. Na kauli yake, "wewe nikubalie tu nitakupa ubunge wa viti maalum", hata kutongoza hajui maskini ya Mungu!

Kwa taarifa yako Mwigamba, wenzako Zitto na Prof Kitila walikuwa wanakutazama tu. Walishajua 'umaluuni' wako, kwa hiyo walikuwa wanakuvizia ACT ipate kura za kutosha kupewa viti maalum, ungeona kama ungempenyeza hata hawara yako hata mmoja. Ulishasema Zitto ana akili kubwa, sasa wewe ungeweza vipi kumzidi ujanja na umchafulie chama kwa tamaa zako?

Ninaposema haya ni kwa sababu Mwigamba mimi mwenyewe alinitongoza. Aliniambia angenipa ubunge wa viti maalum. Hakuna siku nilijisikia vibaya kama hiyo. Nilimwangalia na ile sura yake iliyokosa nuru. Nikamtathmini na lafudhi yake isiyo na urafiki na Kiswahili wala Kiingereza. Nilimaliza na zile suruali mbaya-mbaya kama yule daktari bingwa wa kutoa mimba Manzese. Eti na mimi nimkubali! Si kujitia laana jamani?

Hata ningekua na kiu ya mwanaume kiasi gani. Ningekuwa na tamaa kubwa kiasi gani ya kupata ubunge wa viti maalum. Kweli kabisa mimi nikubali kulala na wewe Mwigamba. Siku hiyo hata babu mzazi wa bibi mzaa mama angeamka. Angenicharaza viboko vingi sana. Mkosi gani huo mimi kulala na wewe Mwigamba?

U'MWAYAONA WA MWIGAMBA

Mwigamba alikuwa Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo. Zitto akampa na gari la kutembelea. Akaanza kuonekana wamo. Alitegemea chama kingepata ruzuku nyingi ili achote. Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, akaona hakuna ulaji tena, maana ACT hakikufikisha kura za kutosha kupata ruzuku. Ruzuku pekee ambayo chama kinapata ni ya ubunge wa Zitto.

Mwigamba alipoona hivyo, akaomba kujiuzulu Ukatibu Mkuu aende akasome. Chuo alichokwenda nako masomo yakamshinda. Akataka apewe Ukatibu Mkuu aliojiuzulu, Zitto na Kitila walikataa. Maana uchafu wake wote wanaujua.

Kuna ile kashfa ya kula michango ya wanachama. Mwigamba alikusanya fedha za wanachama kwa lengo la kuanzisha gazeti la chama. Mwigamba baada ya kuona fedha ni nyingi, akaingia tamaa. Akazitafuna. Mwigamba ni mwizi aisee! Halafu ndiyo alinitongoza. Mimi mwanaume mwizi hivyo wa kazi gani?

Mwigamba alipoona Prof Kitila ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akategemea yeye ndiye angeteuliwa kuziba nafasi ya kuwa Mshauri wa Chama. Watu wakampuuza, akateuliwa Albert Msando.

Anna Mghwira alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mwigamba akajua yeye ndiye angeteuliwa na vikao vya chama kukaimu uenyekiti. Watu wakampuuza. Tena wakati Rais Magufuli anamteua Mghwira, Zitto alikuwa kwenye ziara nje ya nchi. Alipoondoka alimteua Mwigamba kukaimu Uongozi wa Chama.

Sasa Mghwira alipoteuliwa tu kuwa Mkuu wa Mkoa, Mwigamba kwa nafasi yake ya Kaimu Kiongozi wa Chama, aliitisha kikao na kumwondoa Mghwira kwenye uenyekiti. Alifanya makusudi ili Zitto akisharejea, afikiriwe yeye kupewa uenyekiti wa chama. Nani ampe? Wakampuuza!

Alipoona na uenyekiti amenyimwa ndiyo akaanza kushawishi wanachama na viongozi wa chama ili wahamie CCM. Eti kuna vyeo vinawasubiri. Haya CCM alishakwenda, aliyodhani yamo hayamo, sasa anaona ACT inasonga mbele ndiyo anazua maseke.

Kila siku Mwigamba anaishambulia ACT, anamshambulia Zitto. Anamsema mpaka kwa historia za kutunga za miaka ya 2009 na 2010. Anasahau kuwa mwaka 2013 aliandika waraka akisema Zitto ni akili kubwa, aliyefaa kuongoza Chadema kuliko Mbowe. Mwaka 2009 na 2010 Zitto hafai, mwaka 2013 anafaa, ni akili kubwa, mwaka 2018 Zitto hafai kwa sababu alikuwa hafai miaka ya 2009 na 2010. Huu ni uzezeta wa wapi?

Tunarejea kule kwa Mwayaona. Mume alikuwa hafai kwa sababu hakuwa hata na kitanda, ila huyohuyo akakubali kuolewa naye. Wakaishi wote. Baada ya kuachana ndiyo anasema mume hafai kwa sababu alimkuta hana kitanda. Mwayaona na Mwigamba ni kama mapacha.

Mwigamba yupo CCM hivi sasa, ila haishi kuizungumzia ACT. Ni kama Mwayaona, alishamwacha Chatta na kwenda kwa Chaddy, lakini kila siku anamzungumzia Chatta. Kumbe Mwayaona bado anampenda sana Chatta. Na Mwigamba bado anaipenda sana ACT.

Kinachomuumiza Mwigamba ni kupoteza ukaribu na Zitto. CCM aliko leo hana mtu wa kumjali. Bahati za Kitila na Mghwira, alifikiri naye zitamwangukia haraka. Yupo tu anasugua. Anageuza shingo ACT, anaona mambo yanaendelea. Zitto aliyekuwa akimlea, hana habari naye tena. Kwa hasira ndiyo sasa anaamua kumshambulia Zitto. Kama tu Mwayaona anavyomshambulia Chatta.

Huyo ndiye Mwigamba a.k.a pacha wake Mwayaona. Kinachomtesa Mwigamba ni kuona hana nafasi ya kurejea ACT. Ni kama Mwayaona, kinachomtesa ni kuona nafasi yake kwa Chatta imeshazibwa.

Mwigamba ndiye Katibu Mkuu wa kwanza kugombea kura za maoni za ubunge na kutoka wa nne. Katibu Mkuu Taifa akakosa mvuto jimbo moja tu la Ubungo, wanachama wakampiga chini. Akawa wa nne. Mwanaume mwenye nyota yenye giza hivyo alale na mimi kweli? Tuheshimiane Mwigamba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Hata ningekua na kiu ya mwanaume kiasi gani. Ningekuwa na tamaa kubwa kiasi gani ya kupata ubunge wa viti maalum.
Kweli kabisa mimi nikubali kulala na wewe Mwigamba. Siku hiyo hata babu mzazi wa bibi mzaa mama angeamka. Angenicharaza viboko vingi sana. Mkosi gani huo mimi kulala na wewe Mwigamba?"

Hapo mkamalizane tu, ugomvi wa mapenzi huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani aliyeandika ni Mwigamba mwenyewe ili walau akumbukwe ktk jamii na ccm imuonee huruma. Jina lake limekufa kwa kifo cha kawaida, Kutajwatajwa ni kumpaisha. Nashauri uifute tu post yako ikibidi.

images (19).jpeg
 
Duu, naanza kueleewa Sasa kwanini asilimia 90% ya wabunge wa viti maalumu wa kike ni Warembo!
 
Wewe dada Kasegela Corona ikiisha rudi shuleni. Kutongozwa pia unafungulia uzi JF! Au ndo unajiproud hapa tufahamu kuwa ulitongozwa na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama Cha Siasa?

Au unachuki baada ya kulala nae, amekutupa! Andaa mazingira rafiki mkutane, umwambie namna ulivyolimiss penzi lake. Acha Mambo ya kudhalilisha watu. Akija hapa na uzi nae, kuwa Kitumbua Cha Kasegela ni sawa na Ziwa Victoria, utafurahi? Jifunze kuheshimu watu Mkuu, Mwanamke kutongozwa ni Suna! Katika maisha yako ulishatongozwa na Mwigamba peke yake? Utakosa mashiko kwa kujadili watu badala ya kujielekeza kwenye hoja.

Mkitongozwa mnalalamika, msipotongozwa mbio mbio Bagamoyo kwenye viringe. Jiheshimu bana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAUMIVU YA MWIGAMBA KWA ACT-WAZALENDO BAADA YA KUTELEKEZWA NA CCM NDIYO YANACHOCHEA CHUKI ZAKE DHIDI YA ZITTO KABWE.

Samson Mwigamba ni mwanachama wa CCM. Kabla ya hapo alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo. Mwigamba aliasisi ACT akitokea Chadema ambako alipata kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha. Historia yake ya nyuma kisiasa si mihimu kwa andiko hili leo.

Utajua Mwigamba ni Mwayaona wa pili kwa kutazama rekodi. Je, aliondokaje Chadema kwenda kuanzisha ACT? Mwigamba alifukuzwa Chadema. Sababu ya kufukuzwa Chadema ni kuandika waraka wa kumwandaa na kumtengeneza Zitto Kabwe kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Zitto alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mwigamba aliona ndiye kiongozi mwenye kufaa kuongoza chama. Mwigamba aliandika kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, uwezo wake ulikuwa umefika ukingoni. Mwigamba alindika "Mbowe ana akili ndogo", Mwigamba aliandika "Zitto ana akili kubwa kuliko Mbowe".

Ni dhahiri Mwigamba alimpenda na kumwamini sana Zitto. Andiko la Mwigamba, maarufu kama Waraka wa Mabadiliko, lilinaswa na viongozi wa Chadema mwishoni mwa mwaka 2013. Ikabainika kuwa Mwigamba aliandika, Prof Kitila Mkumbo, alihariri waraka huo.

Oktoba 2013 Mwigamba alitimuliwa uenyekiti Mkoa wa Arusha, kisha Novemba 2013 alifukuzwa uanachama pamoja na Prof Kitila. Mwaka 2014, ndipo alipoanza michakato ya kuanzisha ACT. Mwigamba akawa Katibu Mkuu wa ACT.

Novemba 2014, Kamati Kuu Chadema ilipomhoji Mwigamba kuhusu waraka huo, alikiri kuandika. Akasema alifanya hivyo bila kumshirikisha Zitto. Kwamba mpaka wakati waraka unabainika, yeye na Prof Kitila walikuwa hawajamshirikisha Zitto.

Inafahamika kuwa Zitto aliingia kwenye matatizo na Chadema kwa sababu ya waraka wa Mwigamba. Kumbe Mwigamba ndiye aliyemchonganisha Zitto na Mbowe kutokana na waraka wake. Ooh, Mwigamba mahaba yake kwa Zitto yalizidi mpaka akaandika waraka kumkashifu Mbowe ili Zitto awe Mwenyekiti wa Chadema.

Unapofika hapo unakuwa huna cha kubisha tena kuwa Mwigamba anampenda Zitto. Mwigamba anamhusudu Zitto. Mwigamba anamkubali Zitto. Mwigamba haambiwi chochote kuhusu Zitto. Mwigamba akilala anamuota Zitto. Mwigamba akinywa maji anamuona Zitto kwenye glasi!

Mwigamba alifanya kazi kuanzisha ACT. Hilo hakuna wa kulipinga. Wakati chama kikianzishwa Zitto alikuwa bado Chadema. Nyakati za aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa ACT, Kidawi Limbu, kutaka kuzuia Zitto kujiunga na chama hicho, Mwigamba alipambana naye vikali. Mwigamba alikuwa tayari "afe beki afe kipa", Zitto ajiunge ACT. Unawezaje kusema kuwa Mwigamba hampendi Zitto?

Basi, Zitto naye akajitahidi kumjali Mwigamba. Akampa gari la kutembelea. Zitto akampiga Mwigamba "sopsop", angalau akaanza kung'ara, ingawa alimeremeta sana kwa sababu alipenda kuvaa zile nguo za kung'aa sana. Nguo ambazo ukipita Tandika, mtu akikutana naye kwa mara ya kwanza, jioni akikutana naye tena, atamkumbuka haraka sana katikati ya maelfu ya watu.

Siwezi kusema kuwa ni nguo za kishamba. Ila, akitokea mtu akasema Mwigamba hupangilia nguo kishamba, siwezi kumpinga. Naanzaje kumpinga kwa mfano! Ni kwa sababu ujanja na uelewa wa Mwigamba ni mpaka kuutafuta kwa darubini. Shida ya kubwa ya Mwigamba ni kutojitambua. Ni mshamba lakini anajidanganya ni mjanja. Ana upungufu wa busara, ila anadhani ana busara. Hekima zimempita kushoto, mwenyewe anajiona Suleiman.

Matunda ya kujengwa akaanza ya kuyatumia vibaya. Akaanza kuwadanganya warembo kuwa angewapa nafasi za ubunge viti maalum. Katika hivyohivyo viti maalum, alitaka kumuweka na mkewe, Lilian Mwigamba. Yaani alishaona chama mali yake. Viti maalum ateue mkewe na mahawara zake. Mwigamba ni sheeeda!!! Kichwa cha Mwigamba kina upungufu wa vitamini aibu. Kwa hiyo hana aibu.

Na ukishaona binadamu hana aibu huyo kaa naye mbali. Mwigamba ni wa kukaa naye mbali. Mwigamba anataka shida zake zote za kimaisha zitibiwe na siasa, halafu na wanawake awabadili kwa jina la siasa. Na kauli yake, "wewe nikubalie tu nitakupa ubunge wa viti maalum", hata kutongoza hajui maskini ya Mungu!

Kwa taarifa yako Mwigamba, wenzako Zitto na Prof Kitila walikuwa wanakutazama tu. Walishajua 'umaluuni' wako, kwa hiyo walikuwa wanakuvizia ACT ipate kura za kutosha kupewa viti maalum, ungeona kama ungempenyeza hata hawara yako hata mmoja. Ulishasema Zitto ana akili kubwa, sasa wewe ungeweza vipi kumzidi ujanja na umchafulie chama kwa tamaa zako?

Ninaposema haya ni kwa sababu Mwigamba mimi mwenyewe alinitongoza. Aliniambia angenipa ubunge wa viti maalum. Hakuna siku nilijisikia vibaya kama hiyo. Nilimwangalia na ile sura yake iliyokosa nuru. Nikamtathmini na lafudhi yake isiyo na urafiki na Kiswahili wala Kiingereza. Nilimaliza na zile suruali mbaya-mbaya kama yule daktari bingwa wa kutoa mimba Manzese. Eti na mimi nimkubali! Si kujitia laana jamani?

Hata ningekua na kiu ya mwanaume kiasi gani. Ningekuwa na tamaa kubwa kiasi gani ya kupata ubunge wa viti maalum. Kweli kabisa mimi nikubali kulala na wewe Mwigamba. Siku hiyo hata babu mzazi wa bibi mzaa mama angeamka. Angenicharaza viboko vingi sana. Mkosi gani huo mimi kulala na wewe Mwigamba?

U'MWAYAONA WA MWIGAMBA

Mwigamba alikuwa Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo. Zitto akampa na gari la kutembelea. Akaanza kuonekana wamo. Alitegemea chama kingepata ruzuku nyingi ili achote. Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, akaona hakuna ulaji tena, maana ACT hakikufikisha kura za kutosha kupata ruzuku. Ruzuku pekee ambayo chama kinapata ni ya ubunge wa Zitto.

Mwigamba alipoona hivyo, akaomba kujiuzulu Ukatibu Mkuu aende akasome. Chuo alichokwenda nako masomo yakamshinda. Akataka apewe Ukatibu Mkuu aliojiuzulu, Zitto na Kitila walikataa. Maana uchafu wake wote wanaujua.

Kuna ile kashfa ya kula michango ya wanachama. Mwigamba alikusanya fedha za wanachama kwa lengo la kuanzisha gazeti la chama. Mwigamba baada ya kuona fedha ni nyingi, akaingia tamaa. Akazitafuna. Mwigamba ni mwizi aisee! Halafu ndiyo alinitongoza. Mimi mwanaume mwizi hivyo wa kazi gani?

Mwigamba alipoona Prof Kitila ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akategemea yeye ndiye angeteuliwa kuziba nafasi ya kuwa Mshauri wa Chama. Watu wakampuuza, akateuliwa Albert Msando.

Anna Mghwira alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mwigamba akajua yeye ndiye angeteuliwa na vikao vya chama kukaimu uenyekiti. Watu wakampuuza. Tena wakati Rais Magufuli anamteua Mghwira, Zitto alikuwa kwenye ziara nje ya nchi. Alipoondoka alimteua Mwigamba kukaimu Uongozi wa Chama.

Sasa Mghwira alipoteuliwa tu kuwa Mkuu wa Mkoa, Mwigamba kwa nafasi yake ya Kaimu Kiongozi wa Chama, aliitisha kikao na kumwondoa Mghwira kwenye uenyekiti. Alifanya makusudi ili Zitto akisharejea, afikiriwe yeye kupewa uenyekiti wa chama. Nani ampe? Wakampuuza!

Alipoona na uenyekiti amenyimwa ndiyo akaanza kushawishi wanachama na viongozi wa chama ili wahamie CCM. Eti kuna vyeo vinawasubiri. Haya CCM alishakwenda, aliyodhani yamo hayamo, sasa anaona ACT inasonga mbele ndiyo anazua maseke.

Kila siku Mwigamba anaishambulia ACT, anamshambulia Zitto. Anamsema mpaka kwa historia za kutunga za miaka ya 2009 na 2010. Anasahau kuwa mwaka 2013 aliandika waraka akisema Zitto ni akili kubwa, aliyefaa kuongoza Chadema kuliko Mbowe. Mwaka 2009 na 2010 Zitto hafai, mwaka 2013 anafaa, ni akili kubwa, mwaka 2018 Zitto hafai kwa sababu alikuwa hafai miaka ya 2009 na 2010. Huu ni uzezeta wa wapi?

Tunarejea kule kwa Mwayaona. Mume alikuwa hafai kwa sababu hakuwa hata na kitanda, ila huyohuyo akakubali kuolewa naye. Wakaishi wote. Baada ya kuachana ndiyo anasema mume hafai kwa sababu alimkuta hana kitanda. Mwayaona na Mwigamba ni kama mapacha.

Mwigamba yupo CCM hivi sasa, ila haishi kuizungumzia ACT. Ni kama Mwayaona, alishamwacha Chatta na kwenda kwa Chaddy, lakini kila siku anamzungumzia Chatta. Kumbe Mwayaona bado anampenda sana Chatta. Na Mwigamba bado anaipenda sana ACT.

Kinachomuumiza Mwigamba ni kupoteza ukaribu na Zitto. CCM aliko leo hana mtu wa kumjali. Bahati za Kitila na Mghwira, alifikiri naye zitamwangukia haraka. Yupo tu anasugua. Anageuza shingo ACT, anaona mambo yanaendelea. Zitto aliyekuwa akimlea, hana habari naye tena. Kwa hasira ndiyo sasa anaamua kumshambulia Zitto. Kama tu Mwayaona anavyomshambulia Chatta.

Huyo ndiye Mwigamba a.k.a pacha wake Mwayaona. Kinachomtesa Mwigamba ni kuona hana nafasi ya kurejea ACT. Ni kama Mwayaona, kinachomtesa ni kuona nafasi yake kwa Chatta imeshazibwa.

Mwigamba ndiye Katibu Mkuu wa kwanza kugombea kura za maoni za ubunge na kutoka wa nne. Katibu Mkuu Taifa akakosa mvuto jimbo moja tu la Ubungo, wanachama wakampiga chini. Akawa wa nne. Mwanaume mwenye nyota yenye giza hivyo alale na mimi kweli? Tuheshimiane Mwigamba!

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuu makubwa hayo una point nzuri sna mengi uliyo andika ni ukweli mtupu ukiacha hayo ya kutakana ww na mwigamba Mh Zitto Pamoja na mapungufu yke hkn ubishi Mh Zitto ni Akili kubwa hkn shaka kuanzia mwaka 2021 ACT kinaenda kuwa chama Kikuu cha upinzani Tanzania Ushauri wngu kwenu au kwako kukaa mbali na Siasa za maji taka km hizo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote hao waliondoka chadema kwa msaada wa ccm wakitegemea wangeiua chadema, waliposhindwa mwigamba akaamua kujiunga ccm ili apate mkate wa kila siku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom