Siri nzito uteuzi wa Dr. Hamis Andrea Kigwangala kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Nzega

Huko siku za nyuma niliwahi kuandika hoja hii hapa hebu fuatilieni na mnaweza kujifunza kitu:

"Ndugu zangu, As I was walking from the Parliament office building in Dar es salaam today, heading to my office located in Makunganya, I passed through the twin towers, and for a second there a feeling of patriotism emerged and I begun to think very seriously on some major political scandals of our times, of course I remembered Dr. Daudi Balali and the sequential sagas he died with.*
From the committee meeting I was thrilled to have learnt of a lot of policies, plans and strategies put in place by the Ministry of Education and Vocational Training. I had a lot of hopes then. But on crossing down the twin towers, I got put off. When I reached my office the spirit for work had vanished, so I decided to read newspapers and books. They could never rekindle my work spirit either. For a moment there I asked myself what is wrong with this country? Is it laws, policies, plans, people who make and implement them or the famous Watson was right? I decided to then look on some documents...first I passed through the constitution? Except for a few clauses, which I already know are deficient, I learnt that, the founding book would never be a reason for our failure. I decided to scan through the MKUKUTA, wow, what a beautifully crafted book! Complete in all 'sectors'. I went through the Vision 2025, same thing...then what? Why are are we still there?*
As I was reading the vision 2025, I got interested to read and read and read! Of particular interest in the document was a section on 'MINDSET'> Je, do we really have the right mindset as a nation? Probably this could be the reason for being where we are today! What do you think? What should be done?
"Section 4.1 DEVELOPMENTAL MINDSET AND EMPOWERING CULTURE
High priority must be given to education and continuous learning. Equally, the effective transformation of the mindset and culture to promote attitudes of self-development, community development, confidence and commitment to face development challenges and exploit every opportunity for the improvement of the livelihood is of prime importance. The effective ownership of the development agenda coupled with the spirit of self-reliance, at all societal levels, are major driving forces for the realization of the vision. Tanzanians should learn to appreciate and honour hard work, creativity, professionalism and entrepreneurship and strive to develop a culture of saving and investment. "
...and on and on...
*
Best regards,
Kigwa."
Naamini natakiwa nikuone,nawezaje kukupata dr?!
 
.....the effective transformation of the mindset and culture to promote attitudes of self-development, community development, confidence and commitment to face development challenges and exploit every opportunity for the improvement of the livelihood is of prime importance. ......... Tanzanians should learn to appreciate and honour hard work, creativity, professionalism and entrepreneurship and strive to develop a culture of saving and investment. "...and on and on..."

Nimeipenda hiyo kwenye red! (Dr Hamis Endrew Kingwangalla (MSK Soulution MD) and MP for Nzega).
Kwanza nakupa Pole kwa yote yaliyotokea na uendelee kutujuza habari zote zile unazolushiwa na wahasimu wako, ila kama kuna hoja ya msingi ijibiwe kwa HOJA! Mie binafsi nakwazika sana pale HOJA zaifu zinapotolewa humu Jamvini na watu. Tunahitaji Hoja yenye Mantiki ambayo imebeba USHAHIDI na si vinginevyo! na hoja inapotolewa ijibiwe kwa HOJA na si USHABIKI.
Ni kweli Watanzania tuna matatizo ya kutokusoma na kuwa waongeaji sana kuliko kutenda! Hii ndio imekuwa KANSA katika jamii yetu na tumekosa UTHUBUTU wa kujaribu! (tumeendelea kuwaachia Wahindi, Wachina na sie kubaki kulalamika tu. Oh Mabenki si rafiki wa wafanyabiashara, oh Mabenki yanatoza RIBA kubwa, wakati wahindi hao hao ndio watumiaji wazuri wa mabenki yetu hapa hapa na ndio yanawapa UTAJIRI na riba hiyo hiyo ambayo sie tunailalamikia kuwa ni kubwa.
Naomba tuache kulalamika, tuwe na udhutu najua tutafanikiwa tu, tusioneane gele pale mmoja wetu anapofanikiwa, ila tujiulize yeye kafikaje hapo?? kwani mie siwezi kufanya hivyo hivyo nami nikatoka!!.
 
quote_icon.png
Originally Posted by HKigwangalla
Kwa kweli Slaa anatia huruma, nilimsikiliza jana alivyokuwa anahaha na Kigwangalla (MB) tu nikasema sasa huyu Mkuu akianza kunishughulikia mimi, nani atamshughulikia Rais wa CCM, nikajiuliza au mimi MB wa CCM ni sawa na mgombea URAIS wa CDM aliyegaragazwa? Kwa kweli Slaa hana jipya yule Mzee, labda ma-think tank wa CDM (kama hata mpo!) mtafute agenda nyingine, na siyo ufisadi, kwa ajili ya kuibeba CDM la sivyo itapotea kabla ya 2015. yaani ameishiwa sera na hoja. Kwa mtindo huu basi kasi ya kuporomoka kwa CDM, na Slaa itakuwa kubwa mno. Slaa - hadi kufikia 2015 atakuwa amepoteza prospects za kuingia Ikulu kwa kiasi kikubwa mno!

VIPI MBONA HUPENDI KUWAELEZA WATU NAMNA ULIVYOFUKUZWA KAZI PALE MUHIMBILI KWA KOSA LA KUKODI GAR LENYE SEBENE NA KUWAFURUMISHIA WAGONJWA WAKIWEMO WAMOYO MUZIKI MZITO?????......IKIWEMO PIA KUMZOMEA WAZIRI MKUU PALE DENTAL.....SUMAYE AKAWAFURUMUSHA ....MLIKUWA WATATU ....?????
PAMOJA NA HAYO NATAMBUA USINGEWEZA KUWA DAKTARI MZURI....MUNGU AMBARIKI SUMAYE NA MWAKYUSA KWA KUWAFUKUZA KAZI.....BUT NAKUPONGEZA KWA JUHUDI ZAKO KWENYE BIASHARA....NA NAPENDA KUKUTIA MOYO.........USIJALI FITNA ZA WASWAHILI AMBAO WANAWAACHA WAGENI WANAANZA KUHARIBIA WAZAWA....

SUALA LA JINA ..WEWE UNAUJUWA UKWELI....LAKINI LAZIMA UKUBALI ULIKOSEA..MIMI NIMESOMA NA WATU WENYE TATIZO KAMA LAKO...KUANZIA o LEVEL...LAKINI WENGI WALIKUWA WAJANJA ...WALIFANYA AFFIRDAVIT KUYAKANA MAJINA YA SHULE MARA TU WALIPOINGIA CHUO KIKUUU.....UNGETAKIWA KUELEWA KUWA KWENYE SIASA HII ISSUE NI KUBWA SANA NA ITAKUHARIBIA NDOTO .....PENGINE HATA IMESHAKUKOESHA UWAZIRI KWENYE VETTIN YA JAMAA ZETU....,UNAWEZA KUENDELEA KUWA MBUNGE LAKINI HUTAKAA UPATE PRESIDENTIAL NOMINATION .....ULITAKIWA ULIVYOJUWA TU UNAINGIA KWENYE SIASA ....USAFISHE MAMBO YAKO NA SIMPLY UNGEENDA MAHAKAMANI KURUDIA JINA LAKO.......UKITAKA HATA SASA HUJACHELEWA .......YOU CAN DO IT.......
CHADEMA WALIKUWA HAWAIJUI HII ISHU BALI IMEPEKEKWA MEZANI KWA SLAA NA HASIMU WAKO NDANI YA CHAMA KUPITIA KWA MWANACHAMA WA KAWAIDA WA CHADEMA....NA FOR SURE HE IS SO FAR AHEAD OF YOU KUELEKEA 2015.....ILE KAULI KUWA WEWE NI HOUSE BOY UNAEMUANGALIZIA NYUMBA YAKE ITATIMIA ....I FEEL SO SORRY!!!
 
Nakushukuru Phillemon, naomba nikutaarifu kuwa kwenye jina langu hakuna kashfa yoyote ile na nimeazimia kumshtaki mahakamani yeyote yule atakayeendelea kunichafua. Huyo jamaa yako anahangaika na jina langu ili kujaribu kunipunguzia umaarufu (kitu ambacho hakiwezi!). Kwa sababu kufanya hivyo ni kupambana na MUNGU aliyenitunuku mimi. Leo hii kuna zaidi ya watoto 47 na watu wazima waliopewa na au waliojipa jina 'al maaruf' la 'KIGWANGALLA'- kuuzima moto huu wa mapenzi ya wanaNzega kwa Mbunge wao ni kazi nzito! Toka jimbo lile lianze hajatokea mtu mmoja akapata umaarufu na watoto na watu wazima wa kike kwa wa kiume wakaitwa kwa jina lake! Haijatokea hata siku moja!

Kamwambie aliyekutuma kuandika hapa kuwa sitetereki na nipo tayari kuwafanyia kazi wananzega. Mimi ni Mbunge wa 2010 - 2015 na sina hakika kama ntagombea hiyo 2015. Sijafanya maamuzi hayo. Nina mambo mengi sana ya kufanya na siyo lazima kwamba nitarudi kwenye Ubunge. Ila huyo jamaa yako sidhani kama atakuja kuwa Mbunge katika jimbo la Nzega, achilia mbali katika nchi hii - sijui ataipanguaje ile kashfa yake ya Uraia? Anajua zaidi. Mi nashangaa anahangaika na kujaribu kunisiliba mimi kwa kile anachodhani kitanichafua wakati anajua kabisa hakitomfikisha popote na kwamba hakuna hoja yoyote, badala ya yeye kuanza kujaza fomu za kuomba uraia. Sifa ya kwanza mbele ya zote kabla hujawa kiongozi katika nchi yoyote ile!

Na kama ntaomba tena Ubunge wa Nzega, basi ni Mungu atakayeamua niwe ama la. Nafanya kazi kwa bidii ili wanaNzega, mwisho wa siku, wanipime kwa utendaji wangu! Na nataka 2015 niwe tayari kupimwa bila wasiwasi!

Hayo mambo ya Uwaziri anajua MUNGU, kama nimeandikiwa nitakuwa, lau kama la, haitokuwa! Hivyo sihangaiki kuutafuta uwaziri ndg yangu. Mimi ni Mbunge na hicho ndo nilichokiomba!
 
Dr, ushamshtaki Kubenea ?

Waliopita, waliobebwa kura za maoni CCM | Gazeti la MwanaHalisi

Waliopita, waliobebwa kura za maoni CCM

--------------------------------------------------------------------------------

Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 August 2010

HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepitisha wanachama 238 kugombea ubunge wa majimbo Tanzania Bara na Visiwani.

Miongoni mwa waliopitishwa, wapo waliotabiliwa na wale waliobebwa. Baadhi ya waliobebwa, ni Hamisi Kigwangala, aliyepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Nzega mkoani Tabora.

NEC imepitisha jina la Kigwangala baada ya kumuondoa katika kinyang’anyiro hicho, Hussein Bashe aliyeibuka kidedea katika kura za maoni.

Kuondolewa kwake kulitokana na kile Rais Jakaya Kikwete alichoita, “utata wa uraia wake.” Kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni, Kigwangala alishika nafasi ya tatu nyuma ya Bashe na Lucas Selelii.

Hivyo basi, aliyestahili kupitishwa kuchukua nafasi ya Bashe, alikuwa Selelii ambaye alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha kura za maoni.

Hadi sasa, hakuna anayejua sababu za NEC kutompitisha Selelii na kumbeba Kigwangala. Kinachofahamika kwa wengi ni kwamba Kigwangala ni mtumishi wa WAMA – taasisi inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete.

Wengine wanasema uamuzi wa Kikwete wa kutomrudisha Selelii umelenga kufurahisha maswahiba zake, Rostam Aziz na Edward Lowassa, ambao wamedaiwa kusikika wakiapa kuwa Selelii hatarejea tena bungeni.

Sasa wachunguzi wa masuala ya siasa ndani ya CCM wanasema Kikwete aliona kwamba hatua yeyote ya kumrejesha Selelii, ingepanua ufa kati yake na maswahiba zake hao wawili.

Mbali na Bashe, mwingine ambaye hakutarajiwa kuteuliwa ni Justin Salakana aliyepitishwa kuwania jimbo la Moshi Mjini.

Kwanza, katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, Salakana alishika nafasi ya tatu nyuma ya Athuman Ramole na Thomas Ngawaiya.

Pili, Salakana hana ubavu wa kupambana na mbunge wa CHADEMA katika jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Tatu, kumpitisha mtu ambaye si chaguo la wanachama wenzake na ikitiliwa maanani kwamba hana ubavu wa kushindana, ni kudhoofisha chama na kudidimiza demokrasia.

Nne, mwaka 1995 Salakana alikuwa mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA, lakini katika uchaguzi uliofuata alishindwa vibaya na mbunge wa sasa, Basil Mramba kutokana na kile kilichodaiwa kuwa “kugeuza ubunge wake kuwa sehemu ya familia yake.”

Wachunguzi wa siasa wanasema Salakana kwa Ndesamburo, hata kama waliwahi kuwa chama kimoja, ni sindano na shoka. Wanasema amewekwa ili ashindwe na kupotea kisiasa.

Mwingine ambaye amepitishwa baada ya kumwagwa katika kura za maoni, ni Gerson Lwenge anayewania ubunge jimboni Njombe Magharibi. Alikuwa mtu wa tatu nyuma ya Thomas Nyimbo na Yono Kevela.

Hatua ya NEC ya kumuengua Nyimbo ambaye aliibuka kidedea, tayari imeleta kizaazaa ndani ya chama hicho. Nyimbo na wanachama wenzake kadhaa wa chama hicho, wamejiengua na kujiunga na upinzani ambako akigombea, hasa kupitia CHADEMA, ana uwezekano mkubwa wa kushinda.

Kwa zaidi ya miaka 10 Nyimbo amekuwa akituhumiwa na viongozi wake ngazi ya taifa kwa kudhoofisha chama, tuhuma ambazo zimekanushwa na viongozi wake wa mkoa.

Hata hivyo, hata kama madai ya Nyimbo yamebaki hai, NEC haikuwa na sababu za msingi za kutompitisha Kevela ambaye amekuwa mbunge katika jimbo hilo kwa kipindi kimoja tu. Badala yake imembeba aliyeshika mkia.

Orodha ya waliopitishwa na ambao hawakustahili ni ndefu. Lakini kubwa zaidi hapa ni hili: Kinyang’nyiro hiki, kimethibitisha kwa mara nyingine tena, kwamba rushwa ni dondandugu ndani ya CCM.

Hata ndani ya mkutano wa NEC, madai ya rushwa yaliibuka. Baadhi ya viongozi wa CCM, akiwamo mtendaji mkuu wa chama, Yusuph Makamba walituhumiwa kuvuruga uchaguzi kwa maslahi binafsi.

Tuhuma dhidi ya Makamba zilitolewa na wajumbe wengi akiwamo mwanasiasa machachari, Nape Nnauye. Akiongea kwa lengo la kukinusuru chama chake, Nape alisema Makamba alijipa mamlaka ya kubadilisha taratibu za uchaguzi bila idhini ya NEC.

Alisema jambo hilo linatafsiriwa na wengi kuwa mtendaji wa chama “alihongwa” ili kubeba baadhi ya wagombea. Makamba hakujibu tuhuma hizo.

Hata hivyo, wiki moja kabla ya mkutano wa NEC Makamba alinukuriwa akisema, “Kila mgombea wa ubunge na udiwani ametoa rushwa, isipokuwa walizidiana viwango.”

Ukiondoa haya mawili, jingine linaloonekana katika mchakato huu, ni kuwa wagombea wengi waliopitishwa ni wapya.

Kwa mfano, katika mkoa wa Morogoro, kati ya wabunge 10 waliokuwapo katika Bunge lililopita, ni wabunge watatu tu waliorejeshwa kuwania tena ubunge.

Waliorejeshwa ni Celina Kombani (Ulanga Mashariki), Shabiby Ahmed (Gairo) na Mustafa Mkullo (Kilosa).

Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge lililopita, Dk. Lucy Nkya kutoka mkoa wa Morogoro, sasa amepata jimbo. Amepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Morogoro Mashariki.

Wabunge ambao wameshindwa katika kura za maoni na ambao NEC imebariki kutokomea kwao kisiasa, ni Dk. Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi) na Dk. Omari Mzeru (Morogoro Mjini).

Wengine ni Sulemani Sadiq (Mvomero), Clemence Liyamba (Mikumi), Casto Ligalama (Kilombelo), Hamza Mwenegoha (Morogoro Kusini Mashariki) na Sameer Lotto (Morogoro Mashariki).

Wabunge wapya waliopitishwa kuwania nafasi hiyo, ni Aziz Abood (Morogoro Mjini), Lucy Nkya (Morogoro Mashariki), Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini),
Amos Makala (Mvomero), Abdulsalaam SAS (Mikumi), Hadji Mponda (Ulanga Magharibi) na Abdul Rajabu Mteketa (Kilombero).

Katika mkoa wa Kagera, kati ya wabunge 10 waliokuwapo katika Bunge lililopita ni wabunge watano tu, waliopitishwa kuwania tena nafasi zao.

Hao ni pamoja na John Magufuli (Chato), Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini), Eustace Katagira (Kyerwa), Gosbert Blandes (Karagwe) na Oscar Mukasa (Biharamulo).

Waliofungiwa nje ni Willison Masilingi (Muleba Kusini), Diodorus Kamala (Nkenge), Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini), Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini) na Profesa Fetham Banyikwa (Ngara).

Katika majimbo hayo wagombea waliopitishwa ni Assumpter Mshama (Nkenge), Jasson Rwekiza (Bukoba Vijijini), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini) na Deogratias Ntukamazina (Ngara).

Mkoani Tabora, kati ya wabunge wanane wa zamani, ni watatu tu waliorejeshwa katika kinyang’nyiro. Hao ni Samwel John Sitta (Urambo Mashariki), Said Nkumba (Sikonge) na Rostam Aziz (Igunga).

Dk. James Msekela (Tabora Kaskazini), Teddy Kasela-Bantu (Bukene), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini), Lucas Selelii (Nzega) na Tatu Ntimizi (Igalula), hawakurejeshwa kutetea nafasi zao.

Wagombea waliopitishwa kuchukua nafasi za wabunge hao wa zamani, ni Ismail Aden Rage (Tabora), Rostam Abdulrasul Aziz (Igunga), Athuman Mfutakamba (Igalula), Sumar Mamlo (Tabora Kaskazini), Seleman Zedi (Bukene) na Hamisi Kigwangala (Nzega).

Profesa Juma Kapuya ambaye alikuwa mbunge wa Urambo Magharibi jimbo lake limehamishiwa mkoa mpya wa Katavi. Jimbo lake linafahamika kama jimbo la Kaliua.

Mkoa mwingine ambao umevunja rekodi ya kupata wagombea wapya ni Iringa. Wabunge wa zamani waliopita katika kinyang’anyiro cha sasa ni watano tu kati ya 11 waliokuwapo katika bunge lililopita.

Waliorejea ni Monica Mbega (Iringa Mjini), Peter Msolla (Kilolo), William Lukuvi (Ismani), Binilith Mahenge (Makete) na Anne Makinda (Njombe Kusini).

Wagombea wapya, ni Wiliam Augustino Mgimwa (Kalenga), Deo Filikunjombe (Ludewa), Hassan Mohamed Mgimwa (Mufindi Kaskazini), Mendrad Lutengano Kigola (Mufindi Kusini), Deo Sanga – Jahpeople – (Njombe Kaskazini) na Gerson Hosea Lwenge (Njombe Magharibi).

Je, hatua hii ina maana gani? Kwanza, inaonyesha kwamba kinyang’anyiro cha uspika kitakuwa kikali baada ya uchaguzi. Hii ni kwa sababu, kila anayetaka nafasi hiyo atalazimika kushawishi wabunge wapya watakaoingia baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, iwapo atatokea mgombea mwanamke kujitosa katika kinyang’anyiro hicho, kuna uwezekano mkubwa wa mgombea huyo kushinda, hasa iwapo ataungwa mkono na wanawake wenzake.

Tayari naibu spika wa sasa, Anne Makinda amenukuliwa akiwaambia baadhi ya marafiki zake, kwamba amekataa ofa aliyopewa na kundi la wapinzani wa spika wa sasa Samwel Sitta.

Makinda amenukuliwa akisema alifuatwa ili kuombwa kugombea nafasi hiyo, lakini kutokana na mahusiano yake mazuri na Sitta, amekataa ombi hilo.

Haijulikani kundi hilo litamfuata nani baada ya karata yao hiyo ya kwanza kuchanika. Bali kwa ushindi mkubwa wa upinzani na wingi wa wabunge wapya ambao wanaelewa alichokuwa akifanya Sitta, uwezekano wa spika wa zamani kurudi kwenye nafasi yake bado upo palepale.

Pili, vigogo wanaotaka kujiimarisha kufanikisha malengo yao ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kujijenga kwa wabunge wapya.

Tatu, CCM kitakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya wananchi, pale wagombea wake watakapokutana na wagombea wa upinzani.

Hii ni kwa sababu, katika orodha ya wagombea waliopitishwa na NEC, wengi watakuwa hawana rasilimali za kutosha, hasa majigambo ya kufanikisha miradi ya maendeleo.

Sita, katika orodha iliyopitishwa, wagombea wengi wana uwezo mdogo wa kuchambua na kuainisha mambo, jambo litakalofanya CCM kupata wakati mgumu wa kuuza wagombea wake. Wanafahamika hata kwa majina.

Saba, kupitishwa kwa wagombea hawa kunaweza kuwa ni anguko jingine kwa Lowassa. Tofauti na mwaka 2005 ambapo wagombea wengi waliopitishwa walitokana na kundi la mtandao, waliopitishwa katika kinyang’anyiro hiki ama hawana upande, au ni vigumu kuwatambulisha na kundi lake.

Jingine ambalo limejitokeza katika mchakato huu, ni kuibuka kwa mbunge wa zamani wa jimbo la Tarime, Kisyeri Chambiri ambaye sasa amepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Babati Mjini.

Haikutarajiwa kwa kiongozi ambaye anadaiwa kuvuruga mkoa wa Mara, hadi kuotesha makundi yaliyosababisha mtafaruku mkubwa wa uongozi, kupitishwa kuwania ubunge katika jimbo hili.

Ni Chambiri huyuhuyu aliyesababisha jimbo la Tarime Mjini kuangukia upinzani. Ni yeye na kaka yake, Enock Chambiri waliokuwa wanatuhumiwa kuhubiri “ukabila na uzawa.”

Yawezekana yaliyomkumba Chambiri huko Tarime yakamrudia Babati ambako ni mhamiaji. Bali harakati zake za kurejea bungeni kupitia mbali na nyumbani, zimeonyesha ujanja au ujasiri wa aina yake.

Gazeti toleo na. 202
 
Nakushukuru Phillemon, naomba nikutaarifu kuwa kwenye jina langu hakuna kashfa yoyote ile na nimeazimia kumshtaki mahakamani yeyote yule atakayeendelea kunichafua. Huyo jamaa yako anahangaika na jina langu ili kujaribu kunipunguzia umaarufu (kitu ambacho hakiwezi!). Kwa sababu kufanya hivyo ni kupambana na MUNGU aliyenitunuku mimi. Leo hii kuna zaidi ya watoto 47 na watu wazima waliopewa na au waliojipa jina 'al maaruf' la 'KIGWANGALLA'- kuuzima moto huu wa mapenzi ya wanaNzega kwa Mbunge wao ni kazi nzito! Toka jimbo lile lianze hajatokea mtu mmoja akapata umaarufu na watoto na watu wazima wa kike kwa wa kiume wakaitwa kwa jina lake! Haijatokea hata siku moja!

Kamwambie aliyekutuma kuandika hapa kuwa sitetereki na nipo tayari kuwafanyia kazi wananzega. Mimi ni Mbunge wa 2010 - 2015 na sina hakika kama ntagombea hiyo 2015. Sijafanya maamuzi hayo. Nina mambo mengi sana ya kufanya na siyo lazima kwamba nitarudi kwenye Ubunge. Ila huyo jamaa yako sidhani kama atakuja kuwa Mbunge katika jimbo la Nzega, achilia mbali katika nchi hii - sijui ataipanguaje ile kashfa yake ya Uraia? Anajua zaidi. Mi nashangaa anahangaika na kujaribu kunisiliba mimi kwa kile anachodhani kitanichafua wakati anajua kabisa hakitomfikisha popote na kwamba hakuna hoja yoyote, badala ya yeye kuanza kujaza fomu za kuomba uraia. Sifa ya kwanza mbele ya zote kabla hujawa kiongozi katika nchi yoyote ile!

Na kama ntaomba tena Ubunge wa Nzega, basi ni Mungu atakayeamua niwe ama la. Nafanya kazi kwa bidii ili wanaNzega, mwisho wa siku, wanipime kwa utendaji wangu! Na nataka 2015 niwe tayari kupimwa bila wasiwasi!

Hayo mambo ya Uwaziri anajua MUNGU, kama nimeandikiwa nitakuwa, lau kama la, haitokuwa! Hivyo sihangaiki kuutafuta uwaziri ndg yangu. Mimi ni Mbunge na hicho ndo nilichokiomba!

Kipenzi cha watu wa Nzega? Ya kweli hayo? Mazee hata second place kwenye kura ya maoni hukupata halafu unadiriki kupindisha ukweli?

Kuondolewa kwake kulitokana na kile Rais Jakaya Kikwete alichoita, "utata wa uraia wake." Kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni, Kigwangala alishika nafasi ya tatu nyuma ya Bashe na Lucas Selelii.

Halafu hii habari ya kumu-invoke Mungu ni kawaida ya madikteta, Makaveli na hangers on wao, kuanzia Mafarao, Chinese dynasties mpaka kina Louis Ufaransa all the way down to George W. Bush na juzi hapa Laurent Gbagbo.

We ungekuwa chaguo la mungu ungeshindwa kura za maoni ?
 
Nakushukuru Phillemon, naomba nikutaarifu kuwa kwenye jina langu hakuna kashfa yoyote ile na nimeazimia kumshtaki mahakamani yeyote yule atakayeendelea kunichafua. Huyo jamaa yako anahangaika na jina langu ili kujaribu kunipunguzia umaarufu (kitu ambacho hakiwezi!). Kwa sababu kufanya hivyo ni kupambana na MUNGU aliyenitunuku mimi. Leo hii kuna zaidi ya watoto 47 na watu wazima waliopewa na au waliojipa jina 'al maaruf' la 'KIGWANGALLA'- kuuzima moto huu wa mapenzi ya wanaNzega kwa Mbunge wao ni kazi nzito! Toka jimbo lile lianze hajatokea mtu mmoja akapata umaarufu na watoto na watu wazima wa kike kwa wa kiume wakaitwa kwa jina lake! Haijatokea hata siku moja!

Kamwambie aliyekutuma kuandika hapa kuwa sitetereki na nipo tayari kuwafanyia kazi wananzega. Mimi ni Mbunge wa 2010 - 2015 na sina hakika kama ntagombea hiyo 2015. Sijafanya maamuzi hayo. Nina mambo mengi sana ya kufanya na siyo lazima kwamba nitarudi kwenye Ubunge. Ila huyo jamaa yako sidhani kama atakuja kuwa Mbunge katika jimbo la Nzega, achilia mbali katika nchi hii - sijui ataipanguaje ile kashfa yake ya Uraia? Anajua zaidi. Mi nashangaa anahangaika na kujaribu kunisiliba mimi kwa kile anachodhani kitanichafua wakati anajua kabisa hakitomfikisha popote na kwamba hakuna hoja yoyote, badala ya yeye kuanza kujaza fomu za kuomba uraia. Sifa ya kwanza mbele ya zote kabla hujawa kiongozi katika nchi yoyote ile!

Na kama ntaomba tena Ubunge wa Nzega, basi ni Mungu atakayeamua niwe ama la. Nafanya kazi kwa bidii ili wanaNzega, mwisho wa siku, wanipime kwa utendaji wangu! Na nataka 2015 niwe tayari kupimwa bila wasiwasi!

Hayo mambo ya Uwaziri anajua MUNGU, kama nimeandikiwa nitakuwa, lau kama la, haitokuwa! Hivyo sihangaiki kuutafuta uwaziri ndg yangu. Mimi ni Mbunge na hicho ndo nilichokiomba!

Mmmmh Mh nimethibitisha kwamba hali ya Chama chenu ni mbaya kama haya yametoka kwako! Hadi 2015 mtakuwa mmemalizana kama sio kuuana. Lakini kama lengo ni kututumikia sisi wananchi kwanini mnalumbana kiasi hiki? Haya piganeni vita vya wenyewe kwa wenyewe maana ndipo tulipofikia
 
Mh Dk pamoja na kuwa kuna baadhi ya wachangiaji wanamtuhumu aliyenziasha hii thread kuwa alete ushahidi kudhibitisha, allegation aliyoitoa ni serious sana. Sio ya kuchukulia kijujuu. Kweli inawezekana aliyeleta hii thread ulimfukuza kazi or alikuomba pesa ukamkatalia. Lakini unajua kabisa kwamba habari za siri (inside infromation) huwa zinaleak kupitia hizo njia.

Kwangu mimi sio mara ya kwanza kusikia hii allegation ya matumizi mabaya ya "Stimulus package". Mara ya kwanza kabisa niliiskia mwanzoni mwa mwaka jana, lakini sikuifuatilia sana, as I thought it was the usual ufisadi stuff. Baadae nikaja kuisoma hii allegation kwenye gazeti la Raia Mwema pia mwanzoni mwaka jana. Raia Mwena ilitaja makampuni mengi tuu yanahusishwa na ufisadi wa "Stimulus package". Moja ya makampuni hayo ni MSK Solutions ya jijini Mwanza. Wakati huo nilikuwa sijawahi kukusikia na sikujua kama wewe ni moja ya wamiliki wa hiyo kampuni mpaka ulivyokuja kudhibitisha kwenye hii thread. Labda niiweke tuu habari iliyoandikwa na na gazeti la Raia Mwena wakati.

Maswali yangu ni kuwa
1) ulishawahi kuisoma hii habari?
2) Kama jibu ni ndiyo, ukiwa kama mmiliki wa wa hiyo kampuni mlikubali au kukanusha hizo tuhuma kwenye vyombo vya habari?
3) Nirudie swali la Nsiande hapo juu ambalo hujalijibu ipasavyo kwenye posts zako. Ni kwamba, kama ulifukuzwa kazi wewe na wenzako mliwezaje kupata mtaji wa kuanzisha hiyo kampuni? Mlikuwa na source nyingine ya income? Kama mlichukua mkopo benki, mlikuwa na security gani? Mlipataje hiyo security?
4) Wakati huo ulikuwa na uhusiano wowote na kigogo serikalini au mwanasiasa?
5) Kama ungekuwa mbunge wakati huo ungeisupport hii "Stimulus package" policy kama ilivyopitishwa?
6) Kwa vile kulikuwa na option ya kuchukua mkopo benki au kupitia "Stimulus package" huoni kuwa ingekuwa bora zaidi kwa kampuni yako kuchukua loan kupitia Stimulus package?

Vigogo watajwa kujipa fedha zilizotolewa BOT

Ni Zile za Kunusuru Uchumi (Stimulus Package)

MATUMIZI ya Sh trilioni 1.7 kuhami uchumi dhidi ya mtikisiko wa kiuchumi duniani ulioathiri kampuni za ununuzi pamba mikoa ya kanda ya ziwa na hatimaye kampuni hizo kumegewa sehemu ya fedha hizo sasa yamezua utata, na sasa baadhi ya wakubwa wanatajwa kuwa sehemu ya walionufaika na fedha hizo, Raia Mwema imeelezwa.

Fedha hizo kupitia mfuko maalumu, maarufu kwa jina la ‘Stimulus Package' , zilipitishwa na Bunge wakati wa bajeti lakini Kambi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwa kiongozi wake Hamad Rashid Mohamed ilionya fedha hizo kuibua kile kilichoitwa kashfa ya EPA namba mbili, na kupendekeza fungu hilo liundiwe sheria ili kuwabana wahusika lakini serikali ilipuuza, ikitumia wingi wa wabunge kutoka CCM.Takriban miezi sita sasa tangu fedha hizo kuanza kutolewa, uchunguzi wa Raia Mwema katika kipindi hicho umebaini kuwa baadhi ya fedha zimekwenda katika kampuni zisizofahamika ama ambazo wahusika halisi hawajulikani na badala yake wamewatanguliza watu wengine.

Imeelezwa kwamba sehemu ya kampuni zilizochotewa mamilioni kutoka kitita hicho cha Sh bilioni 1.7 zina uhusiano na vigogo serikalini na wanasiasa na kwamba fedha hizo hazikukidhi matarajio ya serikali kwa wakulima wa pamba.

Kampuni ambazo zinaonekana katika orodha ya zilizopendekezwa ama zilizopata fedha hizo ni pamoja na S & C Ginning Co.Ltd (yenye makao yake Bulamba), Simon Agency Ltd (Mwanza), Fresho Investment Co. Ltd (Shinyanga), Gaki Investment Co. Ltd (ya Shinyanga), Bedugu Ginning Co. Ltd (ya Musoma), Intergrated Cotton Fields Ltd ( ya Mwanza), Igunga Cotton Company (makao yake yako Dar es Salaam), Robasika-Agroproducts Ltd yenye makao yake Kaliua, Tabora na Chesano Cotton Ginnery yenye makao yake Bariadi, Shinyanga.

Kampuni nyingine kwenye orodha hiyo ni Copcot Cotton Trading (Geita), Allanoe Ginneries Ltd (Mwanza), Shinyanga Region Co-op Union (Shinganya), Vsarrian Tanzania Ltd (Bunda), Birchand Oil Mill (Mwanza), Jambo Oil Mill (Shinyanga), Afrisian Ginning Company (Dar es Salaam) na S.M Holdings Ltd (Mwanza).

Nyingine ni Nida Textile Mills Ltd, Hassanal R. Waiji (Maswa), Blore Tanzania Ltd (Mwanhuzi, Shinyanga), Al-Adawi Co.Ltd (Mwanza), Olam Tanzania Ltd (Mwanza), Kahama Oil Mill (Kahama), Kahama Cotton Co. Ltd (Kahama), NGS Investment Co. Ltd (Bariadi), Roko Investment Co Ltd, Cotton Agency & Ginners Ltd na Aham Investment Co. Ltd (Dar es Salaam).

Nyingine ni New Sam Trust Co Ltd (Bariadi), Busangwa Organic Farming Association (Shinyanga), BioSustain Tanzania Ltd (Dar es Salaam), MSK Solutions (Mwanza), Mass Trading (Tabora), Sibuka Co Ltd (Maswa), Nsagali Co. Ltd (Bariadi) na Vitrecs Oil Mill ya Mwanza.

Haikuweza kufahamika mara moja kama kampuni zinazoelezwa kuwa na uhusiano na wakubwa ndizo zilizoorodheshwa ama ni zile ambazo zinatajwa kupokea fedha bila majina ya kampuni hizo kuwa hadharani, lakini Raia Mwema, limethibitishiwa kuwapo wakubwa walionufaika na mamilioni kutoka kwenye "stimulus package."

Katika hali inayothibitisha kuwa mambo si shwari kati ya wakulima wa pamba na wanunuzi ambao wengi wamepata mgawo wa stimulus package, Bodi ya Pamba Tanzania imejikuta katika lawama kali si tu kutoka kwa wananchi bali hata baadhi ya viongozi wa CCM, akiwamo Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, kukiibuka shinikizo kwa Rais Jakaya Kikwete kuifuta bodi hiyo kwa madai kuwa, imeacha shughuli za ununuzi pamba kufanyika holela kupitia kwa mawakala ambao wanawaumiza wakulima.

Kwa upande mwingine, taarifa zaidi zinabainisha kuwa licha ya Bunge kupitisha Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya stimulus package, ni sh bilioni 870.8 pekee hadi sasa, ndizo zimekwishatolewa na Benki Kuu (BoT), chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa fedha hizo.

Mpango huo wa stimulus package ilitiliwa shaka na Kambi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa kiongozi wake, Hamad Rashid Mohamed na kupendekeza utungiwe sheria maalumu ya udhibiti kwa kurejea uzoefu wa baadhi ya nchi za Asia.

Mapendekezo hayo ya kambi hiyo yalilenga kuinusuru nchi na "EPA namba mbili." Katika hotuba yake bungeni wakati wa kujadili stimulus package mwaka jana, mjini Dodoma, Hamad Rashid Mohamed, kwa niaba ya wabunge wenzake kutoka vyama vya CUF, CHADEMA na UDP, alihoji masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha hizo Sh. trilioni 1.7, zilizotangazwa na Rais Kikwete.

"Tunataka sheria ya Appropriation Act iwe na Schedule maalumu ya Stimulus Package na iseme waziwazi nani atapata nini, kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge iwe inapata taarifa kila miezi 3 ya utekelezaji wa hiyo stimulus package.

"Ni ukweli uliowazi kuwa stimulus package inazinufaisha benki tu, kwa kuzipa mwanya wa kufanya biashara nzuri na Serikali kwa kutumia fedha za Serikali yenyewe, na ndio maana katika nchi nyingine serikali imelazimika kuwa na hisa ili kuhakikisha kuwa fedha iliyotolewa ambayo inatokana na kodi za wananchi inadhibitiwa na kurudi kwa walipa kodi na wapiga kura."

Hamadi alisema katika bajeti ya mwaka 2007/08 na ile ya 2008/09 serikali ilijizuia kukopa kwenye mabenki, kwa kigezo kikubwa kuwa mabenki yaweze kufanya biashara ya kukopesha sekta binafsi na kuwa zuio hilo liliongeza ufanisi kwa mabenki kukopesha sekta binafsi kwani mikopo kwa sekta binafsi ilipanda hadi kufikia asilimia 40.

Stimulus Package itapunguza mikopo ya benki kwenda kwenye sekta binafsi, na yale mafanikio yaliyokwishafikiwa yatayeyuka, vinginevyo mabenki yawekewe viwango vya kufikia katika kutoa mikopo nje ya stimulus package.

"Kwa mujibu wa taarifa ya Sera ya Fedha ya BoT serikali itazikopesha benki Sh bilioni 270 kwa ajili ya kuzikopesha sekta binafsi. Itatoa Sh bilioni 205 ili kukopa kwenye benki hizo.

Je, benki hizo zikishindwa kutumia fedha zile ambazo serikali imeziweka ili kukopesha sekta binafsi kutumia fedha hizo kufanya biashara na serikali kwa fedha za serikali? Hili litadhibitiwa vipi? Waziri atueleze,", alihoji Hamad na kuongeza kuwa;

"Mwaka huu wa bajeti ni ya kuongeza matumizi na madhara yake ni mpango huo wa kuhami uchumi kuongeza mfumuko wa bei.

"Serikali imeamua kufidia vyama vya ushirika na kampuni zinazonunua mazao ya wakulima na kuyauza kwa hasara. Katika soko huria kuna kupata faida na kupata hasara. Wafanyabiashara makini wa mazao hupanga bei zao za kununulia mazao kwa kuzingatia bei walioipata katika soko la baadaye.

"Hata hivyo wengine hawapendi kuchukua tahadhari kwa kutegemea kwamba bei itapanda na kwa hiyo watapata faida kubwa. Bei imeshuka kwa hiyo wamepata hasara." Alihoji akisema; Je, hakuna wafanyabiashara wa mazao waliolipa mikopo waliokopa kwa kujibana. Serikali ina uhakika gani kuwa mikopo hii ilitumiwa vizuri?"

Pia alipendekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua kampuni zitakazopewa fedha kutoka katika mpango wa kuhami uchuni.

Alitaka CAG kwanza kuthibitisha kuwa hasara waliopata haikutokana na matumizi mabaya ya mikopo na kwamba, gharama ya ukaguzi huu ilipwe na benki zilizokopesha. Alionya kuwa, la sivyo serikali inaweza kuliingiza taifa katika EPA namba mbili.

CHANZO: Raia Mwema (Vigogo watajwa kujipa fedha zilizotolewa BoT)
 
Nakushukuru Phillemon, naomba nikutaarifu kuwa kwenye jina langu hakuna kashfa yoyote ile na nimeazimia kumshtaki mahakamani yeyote yule atakayeendelea kunichafua. Huyo jamaa yako anahangaika na jina langu ili kujaribu kunipunguzia umaarufu (kitu ambacho hakiwezi!). Kwa sababu kufanya hivyo ni kupambana na MUNGU aliyenitunuku mimi. Leo hii kuna zaidi ya watoto 47 na watu wazima waliopewa na au waliojipa jina 'al maaruf' la 'KIGWANGALLA'- kuuzima moto huu wa mapenzi ya wanaNzega kwa Mbunge wao ni kazi nzito! Toka jimbo lile lianze hajatokea mtu mmoja akapata umaarufu na watoto na watu wazima wa kike kwa wa kiume wakaitwa kwa jina lake! Haijatokea hata siku moja!

Kamwambie aliyekutuma kuandika hapa kuwa sitetereki na nipo tayari kuwafanyia kazi wananzega. Mimi ni Mbunge wa 2010 - 2015 na sina hakika kama ntagombea hiyo 2015. Sijafanya maamuzi hayo. Nina mambo mengi sana ya kufanya na siyo lazima kwamba nitarudi kwenye Ubunge. Ila huyo jamaa yako sidhani kama atakuja kuwa Mbunge katika jimbo la Nzega, achilia mbali katika nchi hii - sijui ataipanguaje ile kashfa yake ya Uraia? Anajua zaidi. Mi nashangaa anahangaika na kujaribu kunisiliba mimi kwa kile anachodhani kitanichafua wakati anajua kabisa hakitomfikisha popote na kwamba hakuna hoja yoyote, badala ya yeye kuanza kujaza fomu za kuomba uraia. Sifa ya kwanza mbele ya zote kabla hujawa kiongozi katika nchi yoyote ile!

Na kama ntaomba tena Ubunge wa Nzega, basi ni Mungu atakayeamua niwe ama la. Nafanya kazi kwa bidii ili wanaNzega, mwisho wa siku, wanipime kwa utendaji wangu! Na nataka 2015 niwe tayari kupimwa bila wasiwasi!

Hayo mambo ya Uwaziri anajua MUNGU, kama nimeandikiwa nitakuwa, lau kama la, haitokuwa! Hivyo sihangaiki kuutafuta uwaziri ndg yangu. Mimi ni Mbunge na hicho ndo nilichokiomba!

Mheshimiwa mbunge wa Nzega, nakushukuru kwa majibu yako mazuri na hasa uwazi wa kunifunulia ni nani huyo unayedhani ndiye anajaribu kuchafua nyota yako. BASHE! Hili sikuliona tangu mwanzo na nina hakika anayaona haya na kama ni jasiri kama wewe basi atajaribu japo naye kutupa majibu ili tuendelee kufurahia show! Kwa siasa za leo hii na bongo yetu si rahisi kujua nani anasema ukweli. Lakini nakupongeza, umepasua anga!
 
@Kiranga, sikuwa wa tatu kwenye kura za maoni kwa haki. Mafisadi kupitia aliyeshinda kura hizo walinunua vituo vya kura kwa gharama kubwa sana. Ungekuwepo Nzega kipindi hicho ungeshangazwa sana kwa uwiano wa umaarufu na difference ya kura. Hayo tuyaache. Ni ya ndani kwetu.

@Nsiande, huwezi kutegemea kukopa kwa security inayotokana na salary yako hlf ukanunue pamba (ambayo ni biashara ya mabilioni). Huwa tunakopa pesa kwa njia ya kuweka dhamana ya assets kiasi fulani na pia kutumia collateral manager anayekuwa anareport mzigo unaoingia, unaokuwa processed kila siku na unaotoka kwa bankers. Bankers wanakupa initial disbursement based on your asset (about 65 perc.) Of the forced value of your mortfaed assets. Ukipewa hiyo hela unaenda kununua pamba, ukiingiza godown 'collateral manager anaushikilia mzigo (anaweka kufuli na label) kisha anareport quantity and quality kwa banker na banker ana-issue pesa against 80perc to 100 perc of the value of the goods in the warehouse and on and on...katika arrangement kama hii, Nsiande, unaweza kufungua credit line ya 3 billion huku ukiwa na asset base ya 400mn TZs tu na ukanunua pamba nyingi kwa ku-maximize efficiency na ku-increase cycle time! Hizi asset si lazima ziwe za kwako, unaweza kutumia za wazazi, za familia, za marafiki au hata za kukodi kwa gharama fulani! (Hapa kuna mtihani; na hapa sasa uwezo wako wa kumshawishi big brother akubaliane na risk unayotaka kubeba, lakini pia wewe kama wewe unaaminika kiasi gani ni muhimu ili kufanikisha hili!)

@EMT, kampuni ya MSK Solutions Ltd haimo kwenye orodha ya makampuni yaliyopewa stimulus package, nenda pale BoT kaulize! Huyo mwandishi alipotosha. Na kama ukifanya siasa za kupeleka magazeti mahakamani utatajirika au utayafunga magazeti mengi kwa kuandika uongo au habari za kuchakachua. Katika miezi michache nimekuwa nikiandikwa kwenye magazeti kwa uongo tupu kiasi kwamba nikiamua kuyafuatilia nitayafirisi haya magazeti. Story ya kubenea uongo, hiyo ya Rai uongo mtupu. Nikiamua kuwafuatilia hawa nitakuwa nashinda na wanasheria au mwenyewe na-hang out kule high court!
 
Unaposema kampuni yangu ililipwa wakati haikulipwa roho inauma maana nabeba hasara na interest ya benki inayohatarisha uhai wa kampuni yetu. Pesa hizo zilikuwa na malengo mazuri lakini huweziamini zilizotoka ni 9bn tu na hiyo trillion 1.7 inayotajwa hapo haikuwepo na kama ilikuwepo sasa hapo wazee wa mabomu chunguzeni ufisadi mlete tukalipuwe!!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mhe. I must say i am impressed by the depth of details in your contributions! Keep it up...waambie hao kina Msekwa pia kwamba what is required ni wao ku-engage na public in all platforms...nasiokusingizia kuhujumiwa na CDM!!!

Respect

PS: I'm not CCM nor CDM....but currently more likely to vote for CDM than any other party!!

Unaposema kampuni yangu ililipwa wakati haikulipwa roho inauma maana nabeba hasara na interest ya benki inayohatarisha uhai wa kampuni yetu. Pesa hizo zilikuwa na malengo mazuri lakini huweziamini zilizotoka ni 9bn tu na hiyo trillion 1.7 inayotajwa hapo haikuwepo na kama ilikuwepo sasa hapo wazee wa mabomu chunguzeni ufisadi mlete tukalipuwe!!!
 
We ungekuwa chaguo la mungu ungeshindwa kura za maoni ?
Anasema alifanyiwa mbinu za mafisadi ndio maana akawa wa tatu.

Ina maana anamkufuru Mungu kwamba Mungu alishindwa kupambana na mbinu za kifisadi za Bashe na Selelii.
 
Anasema alifanyiwa mbinu za mafisadi ndio maana akawa wa tatu.

Ina maana anamkufuru Mungu kwamba Mungu alishindwa kupambana na mbinu za kifisadi za Bashe na Selelii.

Mungu ana njia zake nyingi za kufanya mambo! Na kila akifanyacho ana maana yake! Basi na ahimidiwe mwenyezi milele yote, amina!
 
Unaposema kampuni yangu ililipwa wakati haikulipwa roho inauma maana nabeba hasara na interest ya benki inayohatarisha uhai wa kampuni yetu. Pesa hizo zilikuwa na malengo mazuri lakini huweziamini zilizotoka ni 9bn tu na hiyo trillion 1.7 inayotajwa hapo haikuwepo na kama ilikuwepo sasa hapo wazee wa mabomu chunguzeni ufisadi mlete tukalipuwe!!!

Mkuu HK hili nakubaliana na wewe kwamba MSK hawakulipwa S/package.
Nakubaliana na wewe ktk kuendesha biashara kwa mkopo wa benki kwa kushirikisha mtunza dhamana (collateral manager)

Mine is on how did you guys acquire hiyo ginnery (Mwalujo) maana Lintex mliwalipa hela yote. Ni kweli benki iliwapa dola milioni hizo kwa ku-pledge asset za marafiki na wajomba??? Bahati nzuri ni kwamba wewe na wakurugenzi wenzako mnatoka kwenye familia za kawaida sana. Hicho kishika uchumba Mheshimiwa ndo kinaleta ukakasi ukitusaidia na sie tunatamani kuwa na biashara kubwa. Mitaji ya milioni kumi inazidi kukatika.

Usikubali wanaoshadidia kusema tunakuonea wivu maana hatuna sababu hiyo. Kizuri kula na wa kwenu, hebu tumegee basi!
 
@EMT, kampuni ya MSK Solutions Ltd haimo kwenye orodha ya makampuni yaliyopewa stimulus package, nenda pale BoT kaulize! Huyo mwandishi alipotosha. Na kama ukifanya siasa za kupeleka magazeti mahakamani utatajirika au utayafunga magazeti mengi kwa kuandika uongo au habari za kuchakachua. Katika miezi michache nimekuwa nikiandikwa kwenye magazeti kwa uongo tupu kiasi kwamba nikiamua kuyafuatilia nitayafirisi haya magazeti. Story ya kubenea uongo, hiyo ya Rai uongo mtupu. Nikiamua kuwafuatilia hawa nitakuwa nashinda na wanasheria au mwenyewe na-hang out kule high court!

Mh nashukuru kwa maelezo yako. Nafikiri labda hukuelewa maswali yangu niliyokuuliza hapo awali. Swali langu sio kampuni ya MSK Solutions Ltd kuwa au kutowemo kwenye orodha ya makampuni yaliyopewa stimulus package. Swali langu ni kama whether kampuni ya MSK Solutions Ltd imefaidika kwa namna yoyote ile na hiyo stimulus package. Kampuni inaweza isiwe kwenye orodha ya makampuni yaliyopewa stimulus package lakini still ikawa imenufaika na package kwa njia nyingine whether legal or illegal.
 
Back
Top Bottom