Kimey
JF-Expert Member
- Mar 25, 2009
- 4,117
- 831
Du.....Ebwanaaeeee! Watu wana mavipaji yao ya ukweli.
hivi vipaji vingekua vinatumika kwa vitu vya maana tunge kua mbali saana....
Du.....Ebwanaaeeee! Watu wana mavipaji yao ya ukweli.
Watz jamani! Hii janja iko kwenye vitu vingi vyenye kuhitaji ...vipimo ( weights and Measures) huwa ni tatizo.....Huwezi kununua kitu kwa wafanya biashara wa kibongo bila kukagua! THIS IS CRAZY!
tz kila mtu ana uhuru wa kumkandamiza mlaji nawaambieni, hakuna sheria wala mfuatiiaji sheria, imagine nimeenda mahali kubuy dining table imebandikwa bei laki 9.5 nikaongea na mhudumu akadai bro km unataka ntakuuzia kwa laki 4, but untanikabidhi laki yangu mapemaaa!! imagine huu km sio ufisadi, walaji tunabaki kuwa hoi hoi kwa matumizi na gharama ziszo za lazima, je wafanyabiashara wananeemmeka kikweli? kihalali? duh kila raia tz ni mwizi i believe!!
Pdidy,
Kwa suala la mbao,hasa pale buguruni ni kweli hata mie nilikwenda na fundi wangu na tukiwa na futi kamba yetu,kwani nilikuwa tayari na taarifa hizo za kutumia vipimo feki,Mwanangu wale jamaa ni kiboko wakati mie nipo ofisini naongea na mwenye mbao jamaa wakaomba kuoina ile futi kamba yetu wakatoka na fundi wangu kule nje mmoja akawa anamsemesha fundi wangu wawili wakaifungua futi kamba yetu na kuikata 8ft katikati na kuiunga na super-glue ni kitendo cha haraka bila kuchelewa kwa bahati mie nikawaona kupitia dirisha la ofisini,palikuwa hapatoshi kwa kifupi hiyo ndio deal yao wote wafanyabiashara wa mbao pale Buguruni.Nikaamua kwenda depo SAO HILL kununua mbao.
Bongo kaazi kweli kweliNdugu zanguni habarini za jioni
ni wasaa mwingine tena nimeona niwashirikishe kwa mambo ya ajabu yaliotaka kunitokea leo hii...hakika tunatakiwa kumwamini MUNGU Mkubwa..
Leo hii nilikuwa nimeenda kununua mbao....pale BUGURUNI...kama kawaida nikajaribu kuwakimbia madalalali kupunguza bei....nikampata ndugu mmoja ofisini kwake kabisa..nikiwa na wadogo zangu wawili...tukashuka kutoka 430 mpaka 390 kwa feet..baadae tukaanza kuhesabu mbao kwa kuanza kupima kwa feet...nikashangaa akaja jamaa mmoja akauliza kichwani mguuni...la hasha sikujua kinachoendelea...tukaweka pembeni kama mbao 80...,nikanza kuangalia vizuri jinsi wanavyopima kwa kuangalia ile futi yao vizuri...uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nilitaka kuangua kilio nikaja kukumbuka kumbe sijatoa hela...nikaingia ndani kumuulizia yule mwenye ile sehemu tulioelewana naeakaja tulipofika nikashangaa kukuta baadhi ya watu tuliokuwa tunapima nao hawapo..nikamwambia unaweza kuangali hiyo futi yako vizuri...hatimae alipoiangalia akakana kwamba ile si yake ndugu zanguni UHUNI uliotumika ni huu
ILE FUTI IMEUNGANISHWA UNGANISHWA....MWANZONI INASOMA
1................6..KATIKATI INAINGIA 10............16...INAUNGWA NA 20.......24..KWA HIYO NDUGU ZANGUNI HUU MCHEZO NI KILA SEHEMU WANAPOUZA MBAO...UKIANGALIA 6....10 WAMECHOMOA 4FT
16....20 IMECHOMOLEWA 4FT AGAIN...KWA UJUMLA UNAKUTA UKIPIMA KILA MBAO WANA FT KAMA 8 ZIKO MFUKONI...KWA HIYO UNAPONUNUA MBAO ZAIDI KAMA ZA MILLIONI MOJA UJUE WANA KAMA LAKI 4 MFUKONI......NAOMBA WATANZANIA TUANZE KUFUNGUKA KWA HILI NAJUA WENGI TUNAHANGAIKA KUPATA HELA ZA UJENZI...SASA SI VYEMA WATU WACHACHE KUJA KUCHUKUA KIRAHISI HIVI......
LINGINE NI KWENYE MABATI.....
USIDANGANYIKE KUNUNUA MABATI YAMEFUNGWA KWA BANDO...LOHHHHH
NDUGU PALE JUU NA LABDA MANNE NDIO YAMEANDIKWA GAGE 28 ZINAZOFWATA NI 30--32 KWA MBELE
LETS OPEN OUR EYES
Mie sio Mwizi-Alhamdulillah..na sitamuibia mtu...!!
Back to the Mada...Unajua ktk watu ambao wanauzi ni hawa TBS...Shirika la Viwango...wanafanya nini...? Natamani niwatukane...Wavivu..Wazembe....Vichwa Maji....Jamani Hata kama Haya tunahitaji Kikwete....?...Believe me nenda Tandika/K.KOO au Tandale utakuta Gunia linaitwa Lumbesa...!!
Hivi kwanini Hatuna standards...? Hawa TBS walivyokuwa wahuni eti wanasema wameingia Mikataba na baadhi ya Kampuni kuchunguza Mizigo kabla haijaingia.....Huku wanaochek Magari Dubai na UK....Usipokuwa na Cheti chao..Angalia Zali...!!
Ukifika K.KOO uliza Visadolin vya Nyanya...au Viazi..Utakuta Viazi vimesimamishwa kwa chini..ukipewa tu unaviona vidogo...Nafikiri TBS inabidi ifumuliwe...hawa ni Mafisadi numberi one...kwani ndio contact no.1 ya mtanzania wa kawaida...Kwanini tusitumie Kg za Uhakika...ktk kila measuremts....!!!
Bahati mbaya sasa hata hawa wenye kutumia Kg nao wanabambika kichizi.....kwani wanakuwekea SUMAKU....Nenda kwa wauza nyama...Mzani washauweka Sumaku....kama una mzani wako nyumbani ukirudi pima kila ulichonunua kwa mzani...Utakuta sehemu kubwa umepigwa Changa la Macho..!!! Wauza Madhiwa nao.....
...inatia Hasira hadi kwa wauza ASALI.....washakuchanganyia matakataka ya mbao...wengine maji...ndani yake anakuwekea Nyuki wa kubabaisha ujue ni Halisi haijachanganywa...!!!
Mkuu Pdidy Poleni sana.....!!! next time ukienda uwe na measurement yako...kumkoma Nyani Giladi...!!!