Siri nzito kwa wanaojenga nyumba/vibanda vya biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri nzito kwa wanaojenga nyumba/vibanda vya biashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 30, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni habarini za jioni
  ni wasaa mwingine tena nimeona niwashirikishe kwa mambo ya ajabu yaliotaka kunitokea leo hii...hakika tunatakiwa kumwamini MUNGU Mkubwa..
  Leo hii nilikuwa nimeenda kununua mbao....pale BUGURUNI...kama kawaida nikajaribu kuwakimbia madalalali kupunguza bei....nikampata ndugu mmoja ofisini kwake kabisa..nikiwa na wadogo zangu wawili...tukashuka kutoka 430 mpaka 390 kwa feet..baadae tukaanza kuhesabu mbao kwa kuanza kupima kwa feet...nikashangaa akaja jamaa mmoja akauliza kichwani mguuni...la hasha sikujua kinachoendelea...tukaweka pembeni kama mbao 80...,nikanza kuangalia vizuri jinsi wanavyopima kwa kuangalia ile futi yao vizuri...uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nilitaka kuangua kilio nikaja kukumbuka kumbe sijatoa hela...nikaingia ndani kumuulizia yule mwenye ile sehemu tulioelewana naeakaja tulipofika nikashangaa kukuta baadhi ya watu tuliokuwa tunapima nao hawapo..nikamwambia unaweza kuangali hiyo futi yako vizuri...hatimae alipoiangalia akakana kwamba ile si yake ndugu zanguni UHUNI uliotumika ni huu

  ILE FUTI IMEUNGANISHWA UNGANISHWA....MWANZONI INASOMA

  1................6..KATIKATI INAINGIA 10............16...INAUNGWA NA 20.......24..KWA HIYO NDUGU ZANGUNI HUU MCHEZO NI KILA SEHEMU WANAPOUZA MBAO...UKIANGALIA 6....10 WAMECHOMOA 4FT
  16....20 IMECHOMOLEWA 4FT AGAIN...KWA UJUMLA UNAKUTA UKIPIMA KILA MBAO WANA FT KAMA 8 ZIKO MFUKONI...KWA HIYO UNAPONUNUA MBAO ZAIDI KAMA ZA MILLIONI MOJA UJUE WANA KAMA LAKI 4 MFUKONI......NAOMBA WATANZANIA TUANZE KUFUNGUKA KWA HILI NAJUA WENGI TUNAHANGAIKA KUPATA HELA ZA UJENZI...SASA SI VYEMA WATU WACHACHE KUJA KUCHUKUA KIRAHISI HIVI......

  LINGINE NI KWENYE MABATI.....
  USIDANGANYIKE KUNUNUA MABATI YAMEFUNGWA KWA BANDO...LOHHHHH
  NDUGU PALE JUU NA LABDA MANNE NDIO YAMEANDIKWA GAGE 28 ZINAZOFWATA NI 30--32 KWA MBELE

  LETS OPEN OUR EYES
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Kumbe kichwan ama miguuni yaani
  wakuibie kwa

  kichwani.......unaibiwa kwenye calculator.....

  Miguuni........unaibiwa kwenye futi........kazi kwetu
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Watz jamani! Hii janja iko kwenye vitu vingi vyenye kuhitaji ...vipimo ( weights and Measures) huwa ni tatizo.....Huwezi kununua kitu kwa wafanya biashara wa kibongo bila kukagua! THIS IS CRAZY!
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Bongo karibu kila mtu mwizi!

  Habari ndo hiyo!
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Pole sana. ndio maana pakaitwa BONGO
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hata wewe?
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mie sio Mwizi-Alhamdulillah..na sitamuibia mtu...!!

  Back to the Mada...Unajua ktk watu ambao wanauzi ni hawa TBS...Shirika la Viwango...wanafanya nini...? Natamani niwatukane...Wavivu..Wazembe....Vichwa Maji....Jamani Hata kama Haya tunahitaji Kikwete....?...Believe me nenda Tandika/K.KOO au Tandale utakuta Gunia linaitwa Lumbesa...!!

  Hivi kwanini Hatuna standards...? Hawa TBS walivyokuwa wahuni eti wanasema wameingia Mikataba na baadhi ya Kampuni kuchunguza Mizigo kabla haijaingia.....Huku wanaochek Magari Dubai na UK....Usipokuwa na Cheti chao..Angalia Zali...!!

  Ukifika K.KOO uliza Visadolin vya Nyanya...au Viazi..Utakuta Viazi vimesimamishwa kwa chini..ukipewa tu unaviona vidogo...Nafikiri TBS inabidi ifumuliwe...hawa ni Mafisadi numberi one...kwani ndio contact no.1 ya mtanzania wa kawaida...Kwanini tusitumie Kg za Uhakika...ktk kila measuremts....!!!

  Bahati mbaya sasa hata hawa wenye kutumia Kg nao wanabambika kichizi.....kwani wanakuwekea SUMAKU....Nenda kwa wauza nyama...Mzani washauweka Sumaku....kama una mzani wako nyumbani ukirudi pima kila ulichonunua kwa mzani...Utakuta sehemu kubwa umepigwa Changa la Macho..!!! Wauza Madhiwa nao.....

  ...inatia Hasira hadi kwa wauza ASALI.....washakuchanganyia matakataka ya mbao...wengine maji...ndani yake anakuwekea Nyuki wa kubabaisha ujue ni Halisi haijachanganywa...!!!

  Mkuu Pdidy Poleni sana.....!!! next time ukienda uwe na measurement yako...kumkoma Nyani Giladi...!!!
   
 8. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Chuma sio TBS wanahusika kuna jamaa wanaitwa Wakala wa Vipimo (Weight and Measures Agency) ndio wanahusika na mambo ya vipimo na ujazo. TBS wanahusika na viwango/ubora ila wanashirikiana kwa namna moja.
  Tanzania kuna mifumo ya makaratasi ila utendaji minus maana zero ni bora
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii ni style ipo kila sehemu, ukienda Petrol station badala ya litre moja unapata 3/4 mafuta na 1/4 hewa. Ukinunua litre 20 unapata 15 za mafuta na tano za hewa. Haya nenda sokoni kariakoo au Mwenge kanunue mchele Jiwe la kilo moja katikati limepigwa file na kutoa robo kilo halafu wanajazi risasi yenye low density na kuipataka rangi. Nenda Bar agiza kuku mzima, ujue atakatwakatwa vipande vidogodogo na robo itabaki atauziwa mwingine na kama wewe ni mlevi ukiwa chakari chupa nane utaambiwa kumi na tatu. Nenda kwa muuza chips agiza chipsi mayai ujue utawekewa yai moja ulipie mawili basi ili mradi bongo ni wizi kwenda mbele. Ila ukichunguza sana wanaofanya hivi si wenye mali bali ni day waka kama wanavyoitwa, kahesabiwa kitu auze na yeye anataka kupata faida.
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  wakati wenzao wanaangaika kuboresha huduma nzuri kwa wateja hili wafanye biashara zaidi,wao ndio wanazidi kutafuta mbinu ya kumuibia mteja alafu wanalalamika biashara mbovu biashara mbovu wakati ni uduma zao mbovu.unategemeaje pdiddy atarudi tena sehemu hio kama walikuwa wanataka kumuibia?
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  kazi ipo!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mzee umegonga ikulu;

  tusiishie hapo; soma baadhi ya ripoti zetu kwenda donor communities, ni copy paste na urongo kiasi; nenda madukani, bidhaa hazina bei watu wanakuangalia usoni.... Kila kitu bongo ni timing, ukilala tu, jamaa wanakula!!!
   
 13. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Duuh, sikujua hilo na nimeshanunua. Ngoja nitafute tape yangu nikarudie kupima!!!
   
 14. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du.....Ebwanaaeeee! Watu wana mavipaji yao ya ukweli.
   
 15. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tz kila mtu ana uhuru wa kumkandamiza mlaji nawaambieni, hakuna sheria wala mfuatiiaji sheria, imagine nimeenda mahali kubuy dining table imebandikwa bei laki 9.5 nikaongea na mhudumu akadai bro km unataka ntakuuzia kwa laki 4, but untanikabidhi laki yangu mapemaaa!! imagine huu km sio ufisadi, walaji tunabaki kuwa hoi hoi kwa matumizi na gharama ziszo za lazima, je wafanyabiashara wananeemmeka kikweli? kihalali? duh kila raia tz ni mwizi i believe!!
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli sisi taasisi nyingi watu wanaenda kazini kuripoti tu. Huwa hawana creativity wala moyo wa kufanya hizo kazi. Ndo maana karibu kila kitu kinaenda mrama. Lakini masuala mengine yanawezekana kubadilishwa kama nia ipo. Mojawapo ni hili la kudhibiti vipimo na ubora
   
 17. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Pdidy, Shukrani sana.Kwa hakika umenifungua macho.
   
 18. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pole sana Pdidy siku nyingine ukitaka mbao unaweza nistua tu.....wale vijana pale buguruni ndo kazi yao hiyo hasa kama una kiherehere i.e huja tulia lazima wakupe kifutu!
   
 19. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pdidy,
  Kwa suala la mbao,hasa pale buguruni ni kweli hata mie nilikwenda na fundi wangu na tukiwa na futi kamba yetu,kwani nilikuwa tayari na taarifa hizo za kutumia vipimo feki,Mwanangu wale jamaa ni kiboko wakati mie nipo ofisini naongea na mwenye mbao jamaa wakaomba kuoina ile futi kamba yetu wakatoka na fundi wangu kule nje mmoja akawa anamsemesha fundi wangu wawili wakaifungua futi kamba yetu na kuikata 8ft katikati na kuiunga na super-glue ni kitendo cha haraka bila kuchelewa kwa bahati mie nikawaona kupitia dirisha la ofisini,palikuwa hapatoshi kwa kifupi hiyo ndio deal yao wote wafanyabiashara wa mbao pale Buguruni.Nikaamua kwenda depo SAO HILL kununua mbao.
   
 20. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Pdidy,
  Asante kwa kutuwekea huu mkasa. But what can we do?

  Ngoja niwawekee avatar ya member mmoja hapa jamvini itupe some perspective,  Sorry, if you feel insulted.
   

  Attached Files:

Loading...