Siri niliyooneshwa kuhusu nchi yangu Tanzania

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,041
1,160
Ndugu zangu Watanzani, leo nimekuwa na tafakuri ndefu sana kuhusu nchi yangu, wakati nafsi ikielekea kulalamika juu ya hali halisi ya maisha yaliyopo mtaani, nikiwa kwenye chumba changu mwenyewe chenye utulivu mno , wakati nikiendelea kufikiria ni namna gani naweza kupigana na changamoto nyingi tu za maisha zilizopo mbele yangu ikiwa ni pamoja na kutokua na kazi maalum ya kujiingizia kipato cha uhakika, (Ajira Rasmi). Huku moyo ukiwa umejawa na mnyong’onyeo na kukosa furaha.

Nikasema acha nijipe muda wa kuwa mwenyewe leo nijifungie ili niweze kutuliza akili na mawazo kwa mahangaiko ya kila siku.

Ghafla nikiwa katika hali ya utulivu nikaona ndani mwangu napata uzito mkubwa sana, nikapitiwa na usingizi kidgo lakini nilivyozinduka nikajikuta mdomo wangu ukitaka kusema mambo mengi, lakini pia Moyo umejaa AMANI na FURAHA ya ajabu mno. Kila nikijiangalia najiona mimi sio yule wa siku zote, basi nikaendelea kukaa kwa utulivu, ghafla nikakumbuka mambo yote niliyoyaona. Nikaendelea kupata msukumo wa nafsi ukisema waambie watu haya uliyoyaona, yaandike sehemu.

Haraka nikashika kalamu nakuyaandika kwenye Diary yangu lakini pia msukumo uliendelea kunitaka niyaandike humu ili watu wengi waweze kufikiwa na haya.

Ndugu Watanzania, mimi sio kuhani wala Mchungaji. Mimi ni muumini kama walivyo waumini wengine, nahudhuria kwenye nyumba ya ibada kama Ndugu wengine. Nimesema hayo ili watu wasije wakaona labda ninafanya mahubiri hapa. Haya ni mambo ambayo mwenyewe kwangu yamekua mapya.

Lakini pia ni ukweli usiopingika kwamba ukipita kwenye mitandao yote ya kijamii utagundua mambo mengi sana na maoni mengi sana ya Watz yamekuwa ni lawama na Malalamiko mengi kuhusu hali halisi ya maisha.

Kabla sijaweka haya mambo naomba nieleweke kwa mara nyingine tena kuwa haya niyaonayo mimi hayana nia ama lengo lolote ama mlengo wowote wa kisiasa ama wa Kidini.

Ni maono yaliyokuja katika hali ambayo mimi pia bado inanishangaza. Nimeamua pia kuyaandika hapa ili vibaki kama sehemu ya maandishi kwa ajili ya kesho.

Ombi langu ni kuwa Mungu kama kweli haya ndiyo uwaelezayo juu ya Nchi hii na Watu wake basi naomba jambo hili na lisikawie ili FURAHA hii itimie mapema.

Basi haya ndiyo niyaonayo, Twende pamoja;

1. Nimeona Tanzania ikiwa nchi mpya, nimeona watu wengi sana wa nchi zingine wakitamani kuja Tanzania , wengi wanaomba kuja hata japo kutembea tu Tanzania.

2. Nikaona Vijana wakicheka, wengi wakifurahia maisha ya nchi hii. Tena michezo ikitamalaki kila upande wa Nchi hii.

3. Nikaona msururu wa Watanzania wengi walioko nje wakirudi kwa furaha kubwa sana huku wengi wao wakicheka nyuso zao zimejaa tabasamu

4. Nimeona Wamama wakifurahi na kutabasamu, wengi wamejaa kwenye nyumba za Ibada, wangi wakisindikiza misafara ya viongozi huku wakiwa na furaha kubwa sana. Wengi pia wakiwa wamevaa taji.

5. Nimeona wasichana wakibeba majani ya mimea wakishangilia wengine wakizitandika barabarani nao watu wenye kuendesha magari ya blue na meupe wakipita juu yake.

6. Nimeona Ardhi ya nchi hii ikitoa mazao, wengi wanakiifurahi sana, nimeona ukijani mwingi juu ya nchi yote.

7.Nimeona UPENDO kati ya Ndugu na Ndugu ukiimarika zaidi na zaidi.

8. Nimeona wanasiasa wakicheka na kushikana mikono, wengi wakiwa busy sana na kazi, nawaona wengine wakiwa wamekaa makundi makundi chini ya miti mikubwa wakijadili mambo ya nchi.

9. Nikamuona kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia huku nchi yote ikiwa KIMYA . Watu wakimfuatilia kwa makini lakini pia akishangiliwa kila pembe ya nchi.

10. Nimeona Nyumba nyingi za ibada zikifurika watu wengi wengi sana. Nimeona ongezeko kubwa la nyumba za ibada juu ya nchi.

11. Nimeona watoto wengi sana wakizaliwa, nawaona wakiwa na furaha wakicheza kila sehemu ya Nchi hili.

12. Naiona HAKI ikisimama juu ya nchi. Nawaona Watanzania wengi sana wakishikana mikono.

13. Nimewaona vijana wengi sana wakioa na kuolewa, mikusanyiko ya furaha imetapakaa kila sehemu ya nchi.

14. Nayaona magari mengi mengi mno. Kila sehemu naona msururu wa magari mengi mengi mno mno.

15. Nimeona muda wa jioni nchi yote imejaa nuru, taa zinamulika kila upande. Naona nchi iking’aa sana. Watu wanatembea katikati ya taa imulikayo kila upande wa nchi.

16. Nimeona watu wakila vyakula na kusaza. Hakika nimeona NEEMA kubwa juu ya Ardhi ya Tanzania.

17. Nimeona mifugo mingi sana juu ya Ardhi ya nchi hii. Nimeona vijana wa makamo wakichunga mifugo hiyo, lakini pia nimeona magari makubwa yakisafirisha mifugo hiyo kuelekea maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na nyumba zing’aazo.

18. Lakini pia nikaona misitu mikubwa na minene kwenye mabonde na katikati ya milima. Nawaona watu wenye kuvalia kofia katikati ya misitu hiyo.

19. Nimeona kukinyesha mvua kubwa sana juu ya Ardhi ya Tanzania.

Hakika Moyo wangu umejawa na Furaha isiyo na kifani. Nimeona hata kizazi kinachokuja kikifurahia nchi hii Nzuri.

Mpaka naamua kuandika haya yote bado nimejawa na furaha kwa Tanzania yangu niliyoiona. Hakika kama ndie Mungu aonyeshaye haya nimemuomba haya yatokee haraka kabla kizazi hiki hakijaondoka hapa.

Lakini pia hayo ndio machache ambayo nimeyakumbuka katikati ya mengi niliyoyaona.

Ahsante sana kwa kuyasoma na kuyaelewa.

Kama kuna sehemu nitakuletea shida kwa huo ujumbe wangu njoo inbox kwangu.

Goodluck
 
Kila ndoto huwa na maana. Umejisumbua kutaka kujua maana yake?
 
Hali NGUMU ulonayo ya kimaisha,ndio imekufanya kuyaota Yale unayoyatamani. Na unayoyawaza kila SIKU KTK MAISHA YAKO... NAKUSHAURI KUNYWA PEPSI BARIDI ,THEN TAFAKARI SANA, UNAKOKWENDA KIMAISHA.... MAANA KUNA siku utaiona Tanzania yenye malaika na shetani wakicheza pamoja.
 
kifupi ni kwamba hayo uyaonayo usingizini tayari yameanza kujidhihirisha,na wakati wa kuyasema ukifika ni hao wageni ndio watatusemea.

sifahamu miradi mizito inayoendelea itakwisha kujengwa lini,ila naamini sio muda mrefu kutokea sasa,na je,nini kitafuta baada ya hiyo miradi!

Ni maisha ya watu,au miradi mingine!!

tuombe uzima zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom