Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,600
- 65,051
Siri ndani ya ndoa ni chanzo cha matatizo
Unakuta mmoja wapo ndani ya ndoa anafanya mambo yake kwa kisiri, hasa yanayogarimu pesa bila kumshirikisha mwenzake. Mwingine inafikia hatua anajenga majengo, anaanzisha biashara, au kuweka fedha nyingi bank bila kumshirikisha mwenzake.
Hili ni tatizo inapokuja kutokea muhusika akafariki zile mali zake na fedha alizowekeza bank kwa siri, zinakuja kuwanufaisha wengine, na familia iliyobaki kuishi kwenye matatizo. Ndio maana tukizunguka huku duniani tunakutana na baadhi ya magofu ambayo hayajaendelezwa miaka na miaka, ukianza kutafuta chanzo unagundua mengine yalijengwa kwa usiri.