Utakatishaji wa Pesa ndani ya Ndoa

Utakatishaji wa Pesa ndani ya Ndoa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,304
Reaction score
93,354
UTAKATISHAJI WA PESA NDANI YA NDOA.

Na, Robert Heriel

Utakatishaji wa Pesa kama unavyofahamika kama Money Laundering ni moja ya makosa makubwa kisheria Tanzania na duniani kwa ujumla. Kabla sijafika mbali wengi wangependa nieleza kwa ufupi maana ya Utakatishaji wa Pesa(Money Laundering).

Utakatishaji wa Pesa ni mchakato wa kutengeneza pesa nyingi zinazotokana na shughuli za jinai, kama vile biashara ya dawa za kulevya au ufadhili wa kigaidi, biashaea za viungo vya binadamu n.k na kuziiingiza pesa hizo kwenye chanzo halali ili zionekane ni pesa safi. Chanzo halali huweza kuwa ni biashara halali yoyote iliyosajiliwa na kulipiwa kodi kabisa.

Wakili msomi ndugu yangu Osiah Lwinga Jr. atanisaidia kueleza kosa la utakatishaji wa fedha adhabu yake mahakamani ni kifungo cha miaka mingapi. Lakini itoshe kujua kuwa Utakatishaji wa Pesa ni moja ya makosa makubwa ambayo adhabu yake ni mvua ya kutosha.

Utakatishaji wa Fedha nimeugawanya katika aina mbili, nikizingatia ngazi; aina hizo ni;
i/ UTAKATISHAJI WA PESA NGAZI YA FAMILIA
ii/ UTAKATIHSAJI WA PESA NGAZI YA KITAIFA.

Aina hizi zinategemeana kwa kiasi kikubwa Kutokana na kuwa makosa huweza kuwa yale yale na mara nyingi hufanana. Utofauti ni pale ambapo baadhi ya makosa hayawezi kuhusiana na mambo ya kiserikali bali mambo ya kifamilia.

Leo nitaeleza habari za utakatishaji wa pesa ngazi ya familia.

Katika ngazi hii, pesa chafu(pesa inayotokana na shughuli haramu) huingizwa katika chanzo halali cha familia.

Mume na Mke baada ya kuoana huishi maisha kwa kufanya kazi. Kazi hiyo inaweza kuwa ni kuajiriwa au kujiajiri. Kazi ni kipimo cha utu lakini sio kila kazi ni kipimo cha utu. Zipo kazi ambazo za kinyama, na zakishetani ambazo hudhuru au kudhulumu haki za watu wengine.

Pesa zinazotakatishwa ndani ya ndoa ni zile zote zinazotoka katika vyanzo vya siri ambavyo mwenza mmoja wapo havijui, huenda ni Mume au mke. Pesa yoyote ya siri ndani ya familia ambayo inaingizwa na mmoja wa wanafamilia kutoka chanzo cha siri hata kama ni chanzo halali tunaiita pesa hiyo ni haramu. Hakuna sababu ya ziada na muhimu ya kumficha mwenza wako vyanzo vya fedha zako.

Utakatishaji wa pesa ndani ya ndoa zamani ilizoeleka unafanywa na wanaume kwa kufanya shughuli haramu kama vile ujambazi, uuzaji wa madawa ya kulevya, n.k lakini siku hizi wanawake ndio wamegeuka watakatishaji wakubwa wa pesa.

Unakuta umeoa mke, alafu kumbe anafanya umalaya na ukahaba bila ya wewe kujua. Kwenye umalaya huhongwa vijizawadi vya hapa na pale na wanaume wanaotoka naye. Vipesa hivi huingizwa katika familia kwa namna ambayo mwanamke anaona hatashtukiwa kuwa fedha hizo ni matokeo ya umalaya wake.

Pia wapo wanawake walioolewa ambao wao ni makahaba. Yaani hawa hufanya ngono ili kupata pesa. Wanawake wengi sasa hivi ni Makahaba. Umalaya unapungua, ukahaba ndio unazidi. Mwanamke yoyote anayetanguliza pesa mbele kwenye mapenzi huyo ni kahaba. Mke wako kama ni kahaba, hufanya ukahaba wake huko na kupokea posho yake kisha pea hiyo anaiingiza ndani ya familia kwa mfumo ambao hatashtukiwa.

Mbinu nyingi za kutakatisha pesa ndani ya familia ni zile mbinu halali ambazo watu hawatakuwa na mashaka.
Kwa mfano:
1. Mbinu ya kutumia Vikoba au vikundi vya kinamama.
Wanawake wengi walioolewa hutakatisha pesa ndani ya ndoa kwa kutumia vikundi au vikoba vya wanawake. Unakuta anakuja na kitu amenunua au anatarajia kununua atakuambia anapokea mchezo wake mwisho wa mwezi na atanunua gari, au jambo lolote atakalolipenda. Wewe kwa vile ni hamnazo; utafurahi na kuchelea mpaka jino la mwisho kumbe pesa hiyo anaitoa kwa mwanaume mwenzako.

2. Mbinu ya sherehe
Wanawake walioolewa hutakatisha fedha zao ndani ya familia kupitia sherehe. Usishangae siku hizi sherehe za kuzaliwa ni nyingi kwa wanawake. Mke wako anaweza kuandaa sherehe ya kuzaliwa iwe yake au ya mtoto kwa ajili ya kuitakatisha pesa aliyokuwa nayo aliyoipata kwa njia haramu. Hapa ataandaa watu wa kumletea vijizawadi na majizawadi, miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na alizozipata kwa njia haramu. Wewe utakuwa hujui lolote.

Watakatishaji wa pesa hawaishiwi na sherehe, hawawezi kaa miezi mitatu au sita bila ya sherehe yoyote. Sherehe hizo huwa ni bandia lakini kwa jicho la nje ni za kweli. Lengo ni kupewa zawadi na pesa walizozichuma kwa njia haramu na kuziingiza kwenye mfumo halali.

Hii hutumika kwenye harusi bandia nyingi ambazo hazidumu miezi sita utashangaa wameachana, mwanamke huyo hutafuta mwanaume mwingine tena, akipata dili haramu hufanya harusi tena, hivyo hivyo. Mambo haya kugundua ni mpaka uwe umetulia sana.

Wengine huandaa kipaimara, kumbukumbu za ndugu zao waliofariki, n.k.

3. Mbinu ya Wafanyakazi wenzake.
Mke wako huenda ni mfanyakazi serikalini au kampuni binafsi. Huweza kumpanga mkakati na baadhi ya wafanyakazi wenzake waandae sherehe kazini kisha atunukiwe mfanyakazi bora na kupewa mapesa mengi au hata zawadi ya gari. Kumbe zawadi hiyo chimbuko lake ni chanzo haramu kama ukahaba wake, rushwa, madawa ya kulevya au ukuadi.

4. Mbinu ya kutumia Ndugu.
Mke wako anaweza kutakatisha fedha kupitia mama yake au ndugu zake. Hapa atapiga dili na Mama au dadaake kisha atajifanya kama amekopeshwa na mama au dadaake kumbe pesa hizo ni zake alizozipata kwa ufuska wake.

5. Mbinu ya kucheza bahati nasibu.
Mke wako pia anaweza kutakatisha pesa ndani ya ndoa yako kwa kujifanya anacheza bahati nasibu hatimaye hujishindia kitita cha pesa. Huongea na watu aliowapanga, watampigia simu nakujifanya wanamuuliza kuwa amecheza bahati nasibu, yeye atajibu ndio, ataambiwa umejishindia laki sita, au milioni moja kwa kadiri pesa aliyoifake ilivyo. Wewe utabaki umebung'aa.

6.Mbinu ya kufanya biashara.
Mke wako anaweza kutakatisha pesa ndani ya nyumba kwa kujifanya anaanza biashara ndogo huenda ni genge, au mama ntilie, hiyo huitwa geresha tuu. Unashangaa mkeo anaanza kupendeza kwa kasi ya 4G, nguo anazonunua haziendani na kipato cha genge lake. Ukimuuliza atakuambia biashara yake ndio inamsadia kununua vitu vyote hivyo ilhali ni changa la macho.

7. Mbinu ya kupewa Msaada.
Mke wako anaweza kutakatisha pesa kwa kuwaalika watu aliowapanga waje kumpa msaada hapo nyumbani kwako. Wanakuja watu watajifanya ni wainjilisti watajifanya kumshauri na kumuinua mwanamke mwishowe atapewa pesa yake ambayo aliwapa waje wamletee hapo nyumbani.

8. Mbinu ya kutumiwa pesa kimakosa.
Mkeo anaweza akatakatisha pesa kwa kumuambia mtu amtumie pesa, kisha atakaa na wewe pesa hiyo itaingia na kujifanya kushtuka. Atasema hairudishi na kwa haraka ataenda kuitoa kukuzuga, nawe utaona kweli kumbe pesa hiyo katumiwa na mchepuko wako wewe umezubaa zubaa hapo na ndevu zako.

9. Mbinu ya Kupata pesa kutoka kwa mzazi mwenza.
Kama umeoa mke mwenye mtoto tayari asiyewako, hawa hutakatisha pesa kwa namna ya kujifanya kila pesa ametumiwa na mzazi mwenzake, hata kama ametumiwa na mchepuko aliyelala naye jana atakuambia hivyo. Wewe utakuwa umezubaa zubaa tuu kama popoma.

10. Mbinu ya kumkopesha mtu na kuchukua rehani aliyoiweka.
Wanawake wengine hujifanya kumseti rafik yake ajifanye anakuja kumkopa nyumbani, huenda ni laki moja au milioni moja. Tena mume akiwepo kabisa, kisha mke humkopa huyo rafikiake. Rafikiake huweka rehani huenda ni Flat Screen, au simu kali, au chochote alichohongwa au kukinunua kimagendo.Wanapatana siku za deni kulipwa, rafiki yake atashindwa kulipa deni, mke wako ataenda kuchukua hicho kitu kilichowekwa rehani, muda huo hiyo laki moja alisharudishiwa kinyemela wewe ukiwa hujui. Wewe bila kujua unajua hiyo Flat aliyoichukua mke kwa rafikiake ni kweli ilikuwa ni rehani.

Kwa ujumla wanawake wanambinu nyingi za kutakatisha pesa ndani ya ndoa ambazo mpaka mwanaume ajue anapaswa atulize bichwa lake. Na pesa hizo hutokana na ufuska anaoufanya mke wako huko nje bila ya wewe kujua.

Leo nimejikita kwa kinamama lakini nafahamu kuna kinababa ambao nao hutakatisha pesa walizozichuma kutokana na maovu wayafanyayo kama Umario, unakuta mumeo ni mario kwa mwanamke mwingine, anapewa pesa na kulelewa, hizo pesa ndio analeta ndani ya familia. Ushoga, wapo wanaume ambao wameoa ambao ni mashoga bila ya wake zao kujua. Hawa hujiuza kwa wanaume wenzao na kupewa pesa ambazo huziingiza ndani ya familia huku wakijifanya wamezipata katika kazi za kawaida wazifanyazo, uuzaji wa madawa ya kulevya n.k

Mwisho, huu ni wakati wa kuangalia kila hatua uipigayo. Mambo ni motoo.

Taikon wa fasihi nimemaliza, mwenye swali anaweza kuniuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300 au 0711345431
 
Back
Top Bottom