Siri mpya EPA: Vigogo BoT waliamua 'kufa na mafisadi'

Hii naweza kusema ni made in Tanzania.

Hivi kweli tuna viongozi?

Account zote ktk mabenki zinajulikana wanamiliki akina nani bado JK na waziri Mkuu wanatwambia hawashikiki.

Hivi tuliwachagua hili wafanye nini?

Kama kazi imewashinda warudi wawaeleze wananchi wao wananchi watajua cha kufanya.

Hawa EPA kila kukicha tunawazungumzia nafikiri labda kama na viongozi wetu ni sehemu ya EPA vinginevyo mimi nitashindwa kuelewa maneno yao kabisa.

Inatakiwa waweke watu pale panapotakiwa, vinginevyo hata sioni haja ya kuwa na viongozi ni bora kila mutu ajihamulie anavyotaka basi.
 
Gavana mpya wa BOT amejigamba kwamba Uchumi wa Tanzania uko ktk hLI Y kufufuka! Sijui kwa kigezo gani.

Naye pia ni mmoja kati ya wakumbatiao mafisadi otherwise asingekubali kufanya kazi na Mgonja ambaye ni fisadi toka enzi ya ndugu yake Daniel Yona.

MUNGU AWALAANI....
 
uchumi wetu unashuka haupai tena, inlation rate imefikia 9% soma east african, shilingi ya kenya leo ilikuwa tshs 22 hapa moshi mjin. huyo gavana anaota ndoto za lowasa za ndege ya uchumi inayopaa. tusiwalaumu bure wananchi wanaoowapokea mafusadi huko vijini, mafisadi wananunua wananchi kwa cash na materials, mapokezi ya chenge tunaambiw akuwa ametumia angalua vijisenti kama 234m! we must address two issues in parallel, ufisadi na umaskini wa wananchi wetu, tukiweza kupambanakuushinda ufisadi na hali ya uchumi ikiimarika, wananchi wataweza sasa kuwa huru, hata wakishiriki uchaguzi watashiriki kwa utashi wao na wala si kwa njaa zao
 
Hili suala la kushuka kwa thamani ya shilingi mimi naomba ufafanuzi kwa wataalamu wa mambo ya uchumi nilimsikia mbunge mmoja mstaafu akisema kuwa thamani ya pesa inashushwa na Gavana wa benki kuu kwa shinikizo la wamiliki wa migodi ya dhahabu ili watakapobalisha fedha za kigeni hapa waweze kupata fedha nyingi
 
Kweli inasikitisha jinsi kiongozi wa dini wa wadhifa wa Askofu (Laizer) alivyokubali kuwa mshirika katika hekaheka za kisiasa. Alipaswa kusoma upepo kwanza ili kujua kondoo wake wengi wako upande gani, upande wa MAFISADI au upande wa UZALENDO wa kupambana na kuukemea ufisadi. Kwa elimu na upeo wake alipaswa kujua kuwa kondoo wake wako upande wa UZALENDO. Tatizo anasumbuliwa na NJAA ya pesa bila jasho (kamanyola)!!!! Mwenyezi Mungu uibariki Tanzania na ushushe miujiza yako MAFISADI wazidi kuumbuka mchana kweupe. Twasubiri bunge la BAJETI ambapo yai la EPA litanguliwa na mafisadi wataumbuka na kuaabika zaidi!! Amen!!!

Hawa baaghi ya viongozi wa dini siyo waaminifu kama Kakobe amekuwa akiwa akiwaibia waum ini wake kwa kuwadangaya kuwa kuwa wataokoka na kuwataka waache sadaka hata ya baadhi ya mapambo kama mikufu ya dhahabu na kadhalika na baadaye yeye kuviuza
 
Kuna haja ya kuanzisha usalama wa taifa wenye nia halisi ya kulinda masilahi ya taifa la sivyo kuna vita kubwa inakuja tanzania kati ya wanatanzania wenye uchungu na mafisadi hawa wasio na haya hata kidogo.

Currently as to my understanding, hawa jamaa wa usalama wa taifa wana jukumu moja tu..kufanikisha yale yote ya wanaowapa kula na madaraka ya kusimamia taasisi hiyo..Usalama ilikuwa zamani..hao akina chenge na lowasa wangekuwa wanaongelea jela..hata kwa fununu tu..lakini siku hizi aahh..kama ilivyosemwa hapo awali..hadi makanisani tunawapisha kwenye viti maalum..ni kero lakini ndo maisha..mwenye nguvu mpishe
 
Back
Top Bottom