Siri mpya EPA:Vigogo BoT waliamua 'kufa na mafisadi'
*Benki 3 ziligoma kulipa,Balali akalazimisha
*Barclays ilijivua lawama, ikarejesha fedha
*Benki zilizohusika na ufisadi sasa zajitetea
Na Waandishi Wetu
MKAKATI mpana, uliotumika kuhakikisha kampuni tata ya Richmond isiyokuwa na uwezo wala rekodi yoyote katika sekta ya nishati popote duniani, inashinda zabuni ya mabilioni ya kufua umeme wa dharura nchini huku ikibebwa na vigogo Serikalini, Majira Jumapili leo linawathibitishia Watanzania kuwa ulitumika pia katika uchotaji wa sh. bilioni 133 kwenye akaunti ya EPA ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Siri hizo mpya kutoka vyanzo vya ndani vinavyofahamu yaliyoendelea wakati wa mchakato wa kuchotwa fedha hizo na nyaraka nzito ambazo gazeti hili limezinasa wiki hii, kwa pamoja zinazidi kuonesha jinsi utendaji wa aliyekuwa Gavana wa Benki hiyo, Dkt. Daud Balali ambaye Serikali wiki hii ilisema muda utakapofika, ikimtaka, itamkamata, ulivyokuwa na shaka
Kwa mujibu wa nyaraka hizo jumla ya benki 10 za hapa nchini ndizo zilizothibitika kutumiwa na waliochota fedha hizo ambapo kwanza walifungua akaunti za haraka haraka na za dharura na kisha ndipo katika hali iliyozishangaza nyingi kati ya benki hizo, BoT ikaingiza malipo ya mabilioni kupitia akaunti hizo.
Benki hizo na kiasi cha fedha zilizopitishwa kutoka BoT kikiwa kwenye mabano ni Bank of Baroda (T) Ltd (sh. 5,912,901,644), Barclays Bank of Tanzania Limited (sh. 1,548,897,757), CRDB Bank Limited (sh. 35,968,182,854), Diamond Trust Bank Limited (sh. 2,381,529,339) na Eurafrican Bank (T) Limited (6,300,402,225).
Benki nyingine ulikopitishwa mgao huo ni Exim Bank (T) Limited (sh. 2,225,035,393), Kenya Commercial Bank (Tanzania) Limited (sh. 18,188,468,486), NBC Limited (sh. 3,931,766,300), Standard Chartered Bank Tanzania Limited (sh. 48,350,913,759) na United Bank of Africa Limited (UBA) ambako zilipitishwa sh. 8,207,088,464.
Kutokana na kiwango hicho kikubwa kuingizwa kwenye akaunti za benki hizo, benki tatu kati ya 10 ambazo ni Barclays, Kenya Commercial Bank na Standard Chartered zilitushwa na hali hiyo hivyo zikafuata matakwa ya sheria kwa kutilia shaka fedha hizo kwa kutaka maelezo ya uthibitisho kutoka BoT.
Barua ya Novemba 2, 2005 ya benki ya Barclays ilijibiwa haraka na BoT iliyothibitisha na kuhakikisha pasi na shaka kuwa fedha hizo walikuwa wakizitambua na ni halali.
"Pamoja na uthibitisho huo kutoka BoT, Barclays iliamua kuzirejesha BoT fedha hizo na kisha ikaamua kufunga akaunti hiyo ya mteja wake huyo mpya," kimedokeza chanzo chetu. Haijafahamika mara moja baada ya Barclays kurejesha fedha hizo kiasi cha sh. bilioni 1.5 na kuifunga akaunti hiyo, zilikwenda kupitishiwa wapi?
Benki ya Kenya Commercial, kama ilivyokuwa kwa Barclays, ilistushwa na kiwango cha fedha ambacho mteja wake mpya alikuwa ameingiziwa kutoka BoT nayo ikaandika barua kuhoji uhalali wa fedha hizo kiasi cha sh. bilioni 18.
Kwa mujibu wa barua yao yenye kumbukumbu namba KCBTZ/MD/01/37 kwenda Kitengo cha Uchunguzi wa Fedha cha BoT, benki hiyo ilitaka kujua uhalali wa fedha hizo na walijibiwa kuwa ni halali, hazina matatizo.
Huku wakivunja matakwa ya kisheria kwa mujibu wa sheria ya Taasisi na Vyombo vya Fedha (The Banking and Financial Institution Act, 2006) watendaji wakuu wa BoT wakiongozwa na Dkt. Daud Balali aliyekuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea, kwa staili ile ile ya Richmond walionekana 'kuwa tayari kufa' wakihahakisha kampuni mahsusi zilizoteuliwa, zilikipata kila zilichokuwa zikikitaka kutoka akaunti ya EPA.
Vyanzo hivyo vinazidi kubainisha kuwa baada ya uchunguzi wa baadaye wa kina kubainisha kuwa malipo hayo yalikuwa yana utata, aliyekuwa Dkt. Balali katika vikao viwili vizito, alipobanwa, kwanza alizikingia kifua fedha hizo kuwa zililipwa kihalali lakini baadaye alipoona mambo yanakuwa mamgumu, alimsukumia mzigo aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bibi Zakia Meghji kuwa ndiye aliyekuwa akijua kila kitu kuhusu fedha hizo.
Sheria ya Benki Kuu (The Bank of Tanzania Act, 2006) inaipa majukumu BoT kuwa msimamizi wa mabenki mengine na inayataka mabenki yatoe taarifa yanapobaini kuwepo fedha zenye utata.
Kubainika kuwa hata pale ilipoulizwa kuhusu utata wa malipo hayo, BoT iliyatetea, wanasema wataalamu wa masuala ya utawala, ni anguko kuu la kiutendaji kwa Serikali iliyoko madarakani ya CCM.
"Timu ya ukaguzi ilikosa ushahidi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Fedha cha BoT kama kilifanya uchunguzi wowote kilipopewa taarifa za malipo yasiyo halali.Hata tulipokutana na kujadiliana na Dkt. Balali, hakuonesha kutaka kulishughulikia suala hili.
"Pia timu ya ukaguzi ilishangazwa na namna viongozi wa BoT walivyokuwa wakichukua muda mrefu kujibu au kushughulikia masuala yote yaliyoonekana kuwa yenye utata kwenye akaunti ya EPA," kilisema chanzo chetu.
Malipo hayo ambayo jumla yake ni takribani sh. bilioni 133 yalilipwa kwenye benki hizo kati ya mwaka 2005/2006 huku yakihusishwa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, baadhi ya taarifa zikieleza kuwa zilitumika kwenye kampuni za ubinge na urais.
Hata hivyo viongozi waandamizi karibu wote wa CCM wa sasa na waliostaafu, waliwahi kuliambia gazeti hili kuwa chama hicho kina vyanzo vya kujitosheleza kuendesha uchaguzi na kamwe hawakufaidika na fedha hizo kama inavyodaiwa.
Kutokana na staili hiyo ya BoT kukiuka majukumu yake ya msingi, hivi sasa, Majira Jumapili limebaini, benki zote zilizohusika katika sakata hili, zimepata utetezi wenye nguvu.
Maofisa waandamizi wa baadhi ya benki hizo walipoulizwa wiki hii kuhusu benki zao kuhusika katika upitishaji wa fedha za EPA waliitupia lawama nzito BoT yenyewe kuwa ndiyo tatizo si wao.
Hoja yao kuu ya kwanza katika kujivua lawama, wanasema kwamba isingekuwa jambo rahisi kwao kuzitilia shaka fedha hizo hasa kwa kuzingatia zilitoka BoT ambao ndio wasimamizi wakuu wa mabenki yote ya nchini.
Mmoja wa maofisa waandamizi wa CRDB aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti ya kutotajwa jina lake kwa sababu si msemaji, alisema inawezekana benki zilizokataa kupokea fedha hizo zilipata tetesi kuhusiana na utata wake, zikajitoa matatizoni mapema.
"Sisi isingekuwa rahisi kuweza kuzishtukia kwa sababu zilitoka BoT ambao ndio wasimamizi wa shughuli zote za kibenki," alisema na kuongeza:
"Isingewezekana kuzikataa wakati zimetoka kwa mtu anayekusimamia na badala yake kuanza kumuuliza kama zina usalama."
Chanzo hicho kilieleza zaidi kuwa hata hivyo mtu akienda benki kuweka fedha hata kama zinatiliwa shaka, inabidi akubaliwe ziwekwe kwanza kwenye akaunti ndipo baadaye ufuatiliaji ufanyike BoT ili kujua kama si batili.
Alisema ikifanyika kinyume na hivyo mteja aliyepeleka fedha zake benki na kukataliwa anaweza kuishitaki benki husika, akidai ametuhumiwa kwa wizi.
Maofisa wa benki ya Exim nao walipoulizwa walisisitiza kuwa pia kwao ingekuwa ngumu kwa sababu ya uaminifu walionao kwa BoT.
"Wewe unachouliza hapa ni sawa na kumpa mtoto wako fedha lakini badala ya kuzipokea anaanza kukuuliza ulipozipata," kilidokeza chanzo chetu cha habari na kuongeza: "Baba ndiye anayepaswa kumuuliza mtoto amezipata wapi kama amezitilia shaka na si vinginevyo."
Ofisa Habari wa Benki ya NBC, Bi. Nector Pendaeli Foya naye alipoulizwa ili kutoa msimamo wa benki yake, alijibu: "Suala hilo siwezi kulizungumzia mimi, hebu nipe namba zako za simu nitakuunganisha na msemaji mkuu aweze kukujibu." Hadi tunakwenda mitamboni bado viongozi wa benki hiyo hawakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia suala hilo.
Source: Majira