Siri Mauaji Iringa Zaanza Kufichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri Mauaji Iringa Zaanza Kufichuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rosemarie, Sep 12, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  POLISI WALIOTEKELEZA OPERESHENI WADAIWA KUSAFIRISHWA KUTOKA MIKOA MINGINE, WAANDISHI WA HABARI IRINGA WASUSIA MKUTANO WA DCI MANUMBA
  INADAIWA kwamba askari waliokuwa katika operesheni ya kuzuia mkutano wa Chadema katika eneo la Nyololo wilayani Mufindi, Iringa na ambayo ilisababisha kifo cha Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi walitolewa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Mbeya.

  Tayari tukio hilo limeibua mjadala mzito kiasi cha kumfanya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kuunda tume huru kubaini chanzo cha tukio hilo. Marehemu Mwangosi alizikwa juzi nyumbani kwao Tukuyu, mkoani Mbeya.

  Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema kuwa polisi hao kutoka mikoa hiyo mitatu wakiwa wamesheheni vifaa mbalimbali likiwamo gari la maji ya kuwasha, walisafiri siku moja kabla ya mkutano huo wa Chadema na baadaye kuzuka vurugu zilizosababisha kifo hicho.
  Marehemu Mwangosi aliuawa kwa mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu ambao ulisambaratisha vibaya sehemu kubwa ya mwili wake.

  Chanzo cha habari kutoka mkoani Dodoma kilisema: "Hapa kwetu kuna askari 10 na tunawafahamu kwa majina. Waliondoka hapa siku moja kabla ya tukio hilo wakiwa na gari la washawasha."
  Chanzo hicho kilisema kwamba awali, hawakuwa wakifahamu kama baadhi ya wenzao walichukuliwa na kupelekwa Iringa. "Tulikuja kuona kwenye gazeti picha na tulipofuatilia tukaelezwa kuwa ni kweli Dodoma ilitoa askari kwenda Iringa."

  Askari mwingine aliyekuwa katika operesheni hiyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma, alikiri kuwa hadi jana baadhi yao walikuwa bado wako Iringa na kwamba walikwenda kwa agizo la wakubwa wake wa kazi.
  "Sisi ni Watanzania, lakini tumelazimika kuyafanya hayo kwa sababu ya mkate (malipo). Kwa kweli haikuwa haki, kuwatoa askari na silaha kutoka mikoa mitatu kana kwamba wanakwenda kupigana vita!"

  Alidokeza kwamba, askari wote waliotoka Dodoma walikuwa njiani kurudi mkoani humo, jana lakini gari la maji ya kuwasha liliendelea kubaki huko Iringa likiwa na dereva wake na askari mmoja mwenye cheo cha inspekta. Askari huyo alisema kwamba gari hilo lililazimika kubaki kutokana na hitilafu.

  "Wengine wamerudi lakini, kuna wengine wenye gari la kuwasha bado walikuwa Iringa, gari lao limepata hitilafu kidogo," kilisema chanzo hicho kutoka mjini Dodoma.

  Mmoja wa askari hao alidaiwa kwamba hiyo inaweza kuwa moja ya sababu ya askari hao kumshambulia marehemu Mwangosi wakati mwenzao anayemfahamu akijaribu kuwazuia. "Hii inaonyesha kuwa askari hao waliompiga walikuwa hawamjui na huyu aliyekuwa akiwazuia, alimjua."

  Makamanda watupiana mpira

  Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen hakukubali wala kukanusha na badala yake alisema: "Mambo yote hayo yanatakiwa kujibiwa na Kamanda wa Iringa."
  Aidha, alisema sakata la kifo cha mwandishi huyo kwa sasa liko katika vyombo vya uchunguzi hivyo asingekuwa tayari kulizungumzia.

  "Siwezi kusema kama askari wangu walikwenda huko au hawakwenda, isipokuwa ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo lipo katika vyombo husika hivyo waachiwe wao au Kamanda wa Iringa ndiye mwenye majibu."
  Alipotajiwa jina la mmoja wa askari aliyeonekana katika picha za video na magazeti za tukio hilo kwamba anatokea katika moja ya vituo vyake, kamanda huyo alisema: "Mimi yakitokea Dodoma nitazungumza wala siyo mtu mwingine kwa hiyo, mambo ya Iringa siwezi kuyazungumza na kama tutaanza kila Kamanda kuzungumza jambo hilo hamuoni kuwa itakuwa ni kama vurugu?"

  Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alipopigiwa simu yake iliita tu bila kupokewa.
  Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alisema kwa kuwa tukio hilo limefanywa na polisi, mambo mengi yatazungumzwa lakini akasisitiza kwamba hajapeleka askari Iringa.
  Alisema hakukuwa na agizo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wala ombi kutoka Polisi Iringa kutaka askari wa kuongeza nguvu... "Taarifa hizo ni za uzushi kwani hazina ukweli wowote."
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani alikanusha pia kuwapeleka askari wake Iringa akisema: "Hizo taarifa siyo za kweli. Hakuna askari yeyote aliyekwenda Iringa wakati wa vurugu zile."

  Mkutano wa DCI wavunjika

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema: "Hayo yote yameundiwa tume ngoja tuiachie ifanye kazi yake."
  Awali, DCI Manumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari mkoani Iringa, ambao hata hivyo, ulivunjika baada ya kutokea kutoelewana baina yao.

  Manumba alitaka kueleza ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, lakini waandishi hao walikataa kumsikiliza wakisema hawauamini uchunguzi huo kwa kuwa ulifanywa na polisi peke yao.

  Kabla Manumba, hajaanza kuzungumza, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Iringa (IPC), Frank Leonard alisema kutokana na msimamo wa waandishi wa habari wa mkoa huo hakutakuwa na uhusiano wa kikazi na polisi hadi pale tume zilizoundwa kuchunguza kifo hicho zitakapotoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo.

  "Msimamo wetu ni kusitisha uhusiano wa kikazi baina yetu na jeshi la polisi hususan Mkoa wa Iringa, tumekuja hapa kwa sababu DCI umetuita na kama unataka kutupa taarifa ya kifo cha ndugu yetu basi waambie hao maofisa wa jeshi wa Iringa watoke nje," alisema Leonard.

  Akijibu madai hayo Manumba alisema: "Nia yangu ni kutoa taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, ndiyo maana niliwasiliana na mwenzenu ili tuweze kuzungumza, Polisi Iringa wataendelea kuwepo na waandishi wa habari mtaendelea kuwepo, matukio kama haya yapo na yataendelea kuwepo."
  Licha ya maelezo hayo, hakuna mwafaka uliofikiwa na mkutano huo ukavunjika.
  Akizungumza kwa simu na gazeti hili baadaye, DCI Manumba alisema: "Ni vyema wao wangenisikiliza kujua ninataka kuwaambia nini. Lakini, kwa kuwa kuna mkanganyiko, nimeona ni vyema jambo hili lisubiri tume ndipo watakuja kulizungumza."

  Waikataa Tume ya Nchimbi
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeiponda tume ya Dk Nchimbi kikieleza kuwa imeundwa ili kurudisha uhusiano kati ya Polisi na waandishi wa habari na si kutafuta chanzo cha tatizo.

  Juzi, Dk Nchimbi alitangaza kamati ya kuchunguza mauaji hayo inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Steven Ihema na wajumbe, Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga, Mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Mtaalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu.

  Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alisema Dar es Salaam jana kwamba: "Hii si tume ya kuchunguza mauaji, bali ina lengo la kurudisha uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari ili kuwasahaulisha wananchi kwa sababu imeundwa na waziri ambaye naye anatakiwa kuhojiwa." "Tunamwomba Rais Jakaya Kikwete ateue tume kama anavyoelekezwa na Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 1992, ambayo inaruhusu kumhoji yeyote kasoro yeye Rais."

  Lissu alisema Rais Kikwete angeunda tume hiyo na Waziri Nchimbi na IGP Said Mwema wanatakiwa kujiuzulu ili kupisha uchunguzi akidai kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba walitoa amri ya mauaji hayo.
  "Dk Nchimbi anatakiwa kumuiga Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye alijiuzulu akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kutokea mauaji, akijiuzulu atajijengea heshima tofauti na sasa kwani wananchi wamesikitishwa na mauaji hayo," alisema Lissu.

  Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando alidai kwamba kuna mkakati uliowekwa na Serikali wa kukidhoofisha Chadema baada ya kuonekana kwamba ni tishio kwa CCM.

  Mbali na Chadema, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), pia limesema halina imani na kamati hiyo likisema imekuwa kawaida kwa Serikali kuunda tume ambazo hazileti ripoti kwa wananchi.
  "Tume zimekuwa zikiundwa bila faida yoyote, huku zikipewa muda kuchunguza yaliyotokea lakini matokeo yake huwa hakuna ripoti wanayorudisha," alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya.

  Kaaya alisema tume zimekuwa zikiundwa na kuigharimu Serikali fedha nyingi za walipa kodi, lakini ripoti zake zinaendelea kuwa siri.

  Imeandikwa na Habiel Chidawali, Dodoma, Hamida Sharrif Morogoro, na Tumaini Msowoya, Iringa na
  Lasteck Alfred na Juliana

  MJENGWA BLOG HIYO WAKUU
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kweli hakika kazi ipo!

  Serikali legelege ya Jk ndio hii!

  Hili la Marehemu Daudi litawafikisha pabaya hakika!
  Haikubaliki hata kidogo ktk UTU wa kibinadamu!

  Itawachimbia kaburi serikali tawala!
   
 3. G.T.L

  G.T.L JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ewe mwenyezi MUNGU utusaidae
   
 4. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kwa hili, serikali/ccm wamelikoroga big time!

  waandishi wa habari wakiamua kwa umoja kuwageuzia mgongo, huo ndio utakuwa mwisho wao.
  katika hili serikali/ccm inataka kukaba hadi penati...mbele ya umati wa watazamaji
  huyo RPC na wote waliokuwepo eneo hilo hawajakamatwa tu! achilia mbali kujiuzulu

  waandishi komaeni hapo hapo hadi kieleweke,lazima watu wote nchi hii kuanzia mkuu wa nchi hadi mkulima kijijini wajue nguvu ya kalamu na kamera zenu ni kubwa kubwa kuliko nguvu ya mabomu. mimi ni mmoja wa wale wanaowasapoti kwa asilimia 200.

  tunarudi palepale..hakukuwa na sababu yoyote ya kundi la maaskari kumpiga mwandishi wa habari ambaye alikuwa kazini kama wao, na hakuwa na silaha yoyote. alikuwa mikononi mwao kwanini hawakumpeleka rumande kama alifanya kosa lolote, na kama hilo halitoshi mtu anathubutu ku point silaha yake na kufyatua bila utu wala aibu, na mwingine kashika bastola nje nje pembeni madness madness madness. Tanzanians, when and how did we get to this point???? Hivi kweli madaraka ya Tz matamu kiasi hiki??
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mod unganisha habari hii na iliyotangulia, hii si mpya, tumeshaisoma mara nyingi hapa JF.

  Asante kwa kutuletea habari hii usivunjike moyo mdau mwenzetu kwani huenda hukujua kama ni habari iliyorudiwa.
   
 6. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo kunauwezekano polisi walifikiri wanamshughulikia kibaka na sio mwandishi wa habari.Ni wakati sasa wandishi wavae nguo zinazowatambulisha.Kosa la marehemu sasa hili.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Hapana wale walidhamiria hata kama kibaka,walitakiwa kumuua kosa la kuwa pale kwenye mkutano au kuandamana kosa lake kifo siku hizi??
   
 8. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mkuu, hivi angekuwa ni mdogo wako au kaka yako, wud u comment the same thing,(kosa la marehemu!) especial saa hizi,hata machungu hayajaisha?Mke na watoto wake unahisi watajisikiaje,ukiwatamkia hivi usoni?
  Je, ni suala la kuvaa uniform,au ni polisi kupunguza nguvu katika kuwakabili raia? Je,wat if Marehemu,hakuwa mwandisi wa habari,kama ilivyotokea kwa Marehemu Ali wa Morogoro?
  So raia wawe na uniform, wauza magazeti pia, na waandishi. Je kwa hali ya kulelewa kwa jeshi letu la polisi ilivyo sasa, nani ni target wa polisi kuua?ambae hana uniform? Who has the right from God,kumtoa mwenzie uhai?
   
 9. Mwache77

  Mwache77 Senior Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Polisi wenyewe wanapiga mabomu iliwaibee, sasa km imefikia wanaua ili waibe ni hatari sana
   
 10. A

  Akili kweli New Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ishu ni kwamba wanajaribu kuficha uozo kwa kutumia uozo,thats why mambo mengi yanatokea.
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...kwa hiyo ni Haki kwa Polisi kumuua Kibaka kwa kutawanya utumbo wake kwa Bomu??? Kuwa Great Thinker, Mkuu!:nono:
   
 13. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  kwa nini watu hawaruhusiwi au wanaogopa kuzungumzia jamba ambalo linachunguzwa? mimi nilidhani kama mtu anahabari za ukweli kuhusu swala hilo, anatakiwa azungumze ili kuwarahisihia wachunguzi
   
 14. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...G.T.L hiyo avatar yako co mchezo!!
   
Loading...