Siri Kubwa ya Coca yagundulika Baada ya Miaka 125 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri Kubwa ya Coca yagundulika Baada ya Miaka 125

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Duduwasha, Jul 24, 2012.

 1. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hiyo alcohol imekaaje! na hizi Soda Jamii ya Cola niliziacha yapata miaka 15 hivi iliyopita na wala sina hamu nazo...
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  [​IMG] JF Senior Expert Member Array

  Join Date : 3rd February 2009
  Location : European Union
  Posts : 13,681

  [​IMG]
  Utafiti: Unywaji soda husababisha kansa ya tezi kongosho?
  Utafiti wasema unywaji wa angalau soda mbili kwa wiki huongeza hatari ya kupata kansa ya tezi kongosho; viwanda vyadai utafiti una walakini.

  [​IMG]Mapema mwaka huu iliripotiwa na majarida kadhaa sehemu mbalimbali duniani kuwa, kwa mujibu wa utafiti mpya, unywaji wa angalau chupa mbili za vinywaji baridi (soda) kila wiki huongeza uwezekano wa kupata kansa ya tezi kongosho.

  Tezi kongosho lipo nyuma ya tumbo likiwa na kazi ya kuzalisha homoni ya insulin ambayo hufanya kazi ya kuchochea seli zinyonye sukari kutoka katika damu mara baada ya mtu kula au kunywa kitu chenye sukari. Pia hutoa vimeng'enyo ambavyo husaidia katika usagaji wa vyakula vyenye mafuta na protini.

  Walio fanya utafiti huo wanasema kuwa watu wanywao chupa mbili au zaidi za vinywaji baridi kama soda kwa wiki wana uwezekano wa karibu alimia 87 wa kupata kansa ya tezi kongosho ikilinganishwa na wale wasiotumia vinywaji vya aina hiyo. Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la Cancer Epidemiology, Biomarkers & Preventionlinalomilikiwa na chama cha tafiti za saratani cha Marekani.

  Hata hivyo makampuni yanayohusika na utengezaji wa vinywaji baridi wameupinga utafiti huo wakidai kuwa ulikuwa na walakini na makosa mengi, huku wakiegemea katika matokeo ya tafiti zilizowahi hapo kabla ambazo zilionesha kutokuwepo kwa uhusiano wowote kati ya unywaji soda na kansa ya kongosho.

  Katika utafiti wa sasa uliojumuisha watu 60,524 wenye asili ya Singapore na China na ambao ulitumia karibu miaka 14 kukamilika (kuanzia mwaka 1993), watafiti walichunguza vyakula na vinywaji wanavyokula waliohojiwa na kama walipata kansa katika kipindi chote cha ufuatiliaji.

  Watafiti waliuliza washiriki kuhusu vitu wanavyokula ikiwemo soda (ingawa hawakugusia kuhusu diet soda kwa vile kwa wakati huo matumizi ya diet soda nchini Singapore yalikuwa chini sana) na juisi na iwapo vinywaji hivyo vilikuwa vya kawaida au vilikuwa na vitu vya kuongeza ladha (utamu).

  Washiriki waliwekwa katika makundi matatu, wale wasiokunywa kabisa vinywaji baridi (soda au juisi), wanaokunywa chini ya chupa mbili kwa wiki, na wale wanaokunywa chupa mbili au zaidi kwa wiki. Katika kipindi cha miaka 14 ya ufuatiliaji, watafiti wanadai walikuta washiriki 140 wakiwa na kansa ya tezi kongosho. Aidha watafiti wanadai kuwa, wale waliokuwa wanakunywa chupa mbili au zaidi kwa wiki walikuwa na hatari ya kupata kansa kwa karibu asilimia 87. Hata hivyo, hakukuwa na uhusiano wowote kati ya unywaji juisi na hatari ya kupata kansa ya kongosho.

  Watafiti hao wanaamini kuwa sukari iliyomo katika soda husababisha ongezeko la homoni ya insulin kutoka katika tezi kongosho, hali ambayo hufanya tezi hilo kufanya kazi kupita kiasi na hatimaye kupata kansa.

  Hata hivyo wanasayansi kutoka baadhi ya viwanda vya soda wamekosoa matokeo ya utafiti huo wakisema kuwa utafiti huo ulikuwa na mapungufu na udhaifu mwingi sana. Mojawapo ya mapungufu hayo, wanadai wanasayansi ni kuwa idadi ya watu waliogundulika kuwa na kansa ya kongosho ilikuwa ndogo mno na hata miongoni mwa hao 140 waliogundulika, bado washiriki 110 waliripotiwa kuwa katika kundi la wale wasiokunywa kabisa soda, 12 walikunywa soda chini ya mbili kwa wiki wakati ni watu 18 tu waliokuwa katika kundi la wanywaji soda mbili au zaidi kwa wiki. Hii inaonesha kuwa kulikuwa na idadi ndogo mno ya watu waliokutwa na kansa ikilinganishwa na umati ulioshiriki katika utafiti huo.[​IMG]
  Utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2008 ulishindwa kuonesha uhusiano wowote kati ya matumizi ya soda na kutokea kwa kansa ya kongosho; wakati mtafiti mmoja kutoka kituo cha saratani cha Yale nchini Marekani alisema kuwa matokeo haya hayana budi kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa kwa kuzingatia idadi ndogo ya watu waliogundulika kuwa na kansa na kushindwa kwa utafiti huo kuonesha jinsi unywaji soda unavyoweza kusababisha saratani.

  Hata hivyo pamoja na tafiti nyingi kutofautiana na matokeo ya utafiti huu, zipo baadhi ya tafiti ambazo zilitoa matokeo yenye kuonesha kufanana kiasi fulani. Kwa mfano mtafiti Laurence N. Kolonel kutoka Kituo cha Utafiti wa Saratani katika chuo kikuu cha Hawaii, Honolulu huko Marekani alisema kuwa matokeo ya utafiti huu kwa kiasi fulani yanafanana na ya utafiti wao wa mwaka 2007 ambapo waligundua kuwepo kwa uhusiano kati ya utumiaji wa vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose na saratani ya kongosho. Anasema kuwa kwa vile vinywaji baridi vingi vinatumiafructose kwa ajili ya kuongeza ladha, matokeo ya utafiti wao yanafanana sana na matokeo ya utafiti huu.

  Tatizo jingine linaloonekana katika matokeo ya utafiti huu ni kushindwa kwa watafiti wake kuonesha ni kwa vipi walifikia hitimisho la kuwepo kwa uwezekano wa 87% wa mtu kupata saratani kutokana na unywaji wa soda, tukitilia maanani ukweli kuwa saratani ya kongosho ni ugonjwa unaotokea kwa nadra sana duniani kote (huwapata wastani wa watu 12 kwa kila watu 100,000).

  Kwa maneno mengine ni kuwa matokeo ya utafiti huu hayawezi kutumika kutoa hitimisho kuwa unywaji wa soda unasababisha saratani ya tezi kongosho isipokuwa yanaonesha wanywaji wa soda huelekea kupata saratani ya kongosho zaidi ya wale wasio wanywaji.
  Tafiti za afya


  nimeipata kule jf doctors​
   
 3. b

  bigbumper Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  More on TIME.com:

  The recipe:
  Fluid extract of Coca: 3 drams
  USP
  Citric acid: 3 oz
  Caffeine: 1 oz
  Sugar: 30 (unclear quantity)
  Water: 2.5 gal
  Lime juice: 2 pints, 1 quart
  Vanilla: 1 oz
  Caramel: 1.5 oz or more for
  color
  The secret 7X flavor (use 2 oz
  of flavor to 5 gals syrup):
  Alcohol: 8 oz
  Orange oil: 20 drops
  Lemon oil: 30 drops
  Nutmeg oil: 10 drops
  Coriander: 5 drops
  Neroli: 10 drops
  Cinnamon: 10 drops
  The This American Life team
  enlisted experts and ordinary
  citizens alike to taste-test the
  original formula. It was pretty
  close — some people couldn’t
  differentiate it from the real
  thing — but the radio show
  couldn’t hit the nail on the
  head. And no matter what,
  they’ll never quite achieve the
  level of marketing that has
  made Coca-Cola so beloved.
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  lol! kufa tutakufa tu wallah! ukikosekania huku, unapatikania kule!
   
 5. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  acheni ku-overreact, kuna mtu aliyewahi kulewa baada ya kunywa Coca?!!
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  Mkuu una akili Sana Hilo Swali nimelipenda Mimi ni mmoja wapo kipindi naywa hizo soda nilikuwa nachangamka Sana yaani najisikia bien kwa Sana kuna mtu akaniambia hizo soda zinalevya ukinywa Zaidi ya nne...kwa mtu asiyekuwa anatumia vilevi kama uamini You Can try then ulete majibu.

  Je Ushawahi Kunywa Zamzam Cola?
   
 7. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sipendelei ladha ya coca, i prefer fanta/7up lakini ntajaribu for lolz. bado siko convinced kwamba ukinywa chupa XX za coca utaanza kuyumba njiani na kutukana kama mlevi aliyekunywa bia kadhaa. pia sijawahi kusikia/kuona zamzam cola :(
   
 9. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ila huwa nikinywa cocacola nikimaliza najisikia tofauti kidogo kama mchangamfu hili linaweza kuwa na ukweli ila ni kwamba kiwango cha kilevi ni kidogo sana so sio nafikiri sio dhambi kwa wale walokole wenzangu. halafu nahisi ndio maana wasabato huwa hawapendelei kunywa coca ukiwauliza walikuwa hawana majibu ya kuridhisha now kumbe nimeelewa.
   
 10. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh! hawaachi kutafuta kila njia ya kupunguza watu duniani kha! yani hapa lazima makabila flan ivi yanapenda sana soda aina ya coca ndio yamepatikana sana teh teh teh
   
 11. H

  Happy daniel Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nikinywa coca mtoto aliye tumboni anacheza sana,nikinywa M/dew simsikii kabisa na per day lazima ninywe coc3,ndo nakua saaaafii kabisa!
   
 12. K

  Konya JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
   
 13. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  Mountain Dew nayo Pia Ina Caffeine kwa wale wasiopenda Caffeine ni Bora Waache kwani Ukikwepa Caffeine kwenye Cola basi utakutana nayo kwenye Mountain Dew
   
Loading...