Siri kubwa CCM!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri kubwa CCM!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, Feb 28, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nafuatilia masuala ya CCM ni kwanini viongozi wake wengi wanakumbwa na tuhuma za ufisadi??? Nimeingia kwenye website yao nimesoma masharti ya uanachama ndani ya CCM ni pamoja na kuwa "mbu". Moja ya masharti ya uanachama CCM inasomeka hivi:

  Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake. Kuwa mbu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma, kulingana na miongozo ya CCM.

  Kwa uelewa wangu mtu mwenye tabia za mbu ni mnyonyaji na hafai katika jamii hivyo, huenda wanachama wake wanatimiza hili sharti.

  Aleast sasa sitoweza kumlaumu Lowasa, Rostam wala Kalamagi ila CCM yenyewe ibadilishe masharti yake.

  Source:Chama Cha Mapinduzi - CCM
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye MBU wangeongezea kuwa KUPE!
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM ni Joka.... by JK
   
 4. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unarukia mada bila hata kutafakari nini konaweza kukuta kisheria, hivi huoni kwamba mtoa mada amekitukana chama kwa kutoa maneno ya kichochezi? hata chama kikiwa hovyo vipi hakiwezi kikawa na sharti kama hilo.
   
 5. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una uhakika?
   
 6. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe siyo mwana CCM Unatafuta nini kwenye website ya CCM? Hauna hoja
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani niwe mbu?? Haiwezekani
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ina maana hiyo webisite ni kwa wana CCM tu?
   
 9. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  acha kuzusha amekitukana chama wapi? yeye si amenukuu moja ya sharti ya uanachama wa CCM? kama ni mfurukutwa basi umekubuhu
   
 10. CPU

  CPU JF Gold Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nadhani wewe ndio hauna hoja.
  Kwenye website yao kuna sehemu wametamka USIFUNGUE WEBSITE HII KAMA WEWE SIO CCM?
   
 11. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  du umenifumbua macho!! MBU of all the insects!
   
 12. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  MwanaCCM mimi nadhani tujadiri ukweli je hilo sharti halipo? Kwasababu nia yangu siyo mbaya ni kujua tu kwanini viongozi wa CCM wengi wanaandamwa na tuhuma za ufisadi, nikiwa nahangaika kujua sera za chama na malengo yake nikakutana na hilo sharti sasa unategemea hapa sijaupata ukweli?
   
 13. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Aisee hii kali sana yaani katika kutumia lugha ya picha wameona mbu ndo anafaa. Si bora wangetumia nyuki au mchwa ambao n wadudu hufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mkubwa.

  Mbu yuko mstari wa mbele kuleta magonjwa. Nadhani watairekebisha siku si nyingi

  Mtikilia yeye anasema alama za jembe na nyundo za CCM kazi yake ni

  • Nyundo inakugonga kichwani mpaka unakufa

  • Jembe - kazi yake ni kufukia na kuzika.

  Bora wabadilishe nazo hizo waweke picha ya trekta na .....
   
 14. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante lakini moyoni kwako hakuna jema, nyie ndo wale hata ukitendewa mema miamoja lakini kwa bahati mbaya ukatendewa baya moja tuu unasahau yooote
   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  CCM ni n'nge
   
 16. CPU

  CPU JF Gold Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hapo utakuwa umewasifia mkuu
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Du! mkuu bado unawakumbatia ccm tuu?
  Umepitwa na wakati jamaa yangu.
   
 18. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimeingia humo kwenye iyo website, ni kweli mbu imeandikwa but ukisoma vizuri utaona kuwa ni typing error. Ingekuwa wana maanisha hivyo, neno mbu lingetumika hata kwenye sentensi ya mwazo ya paragraph. CCM siwapendi kabisaaa but atleast haki yao nawapa pale wanapostaili.

  (Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake. Kuwa mbu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma, kulingana na miongozo ya CCM.)
   
 19. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sipendi kuita mawazo ya watu wengine CRAP, ila kama ningeweza ningeiita hii CRAP....ila siwezi.
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Angalia ndugu yangu huenda hawakumaanisha unavyotaka kumaanisha
   
Loading...