Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na Shetani

Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari[/QUOTE]

Ndugu, kama ufahamu wako ni mkubwa sana kuliko wangu, uonyeshe wazi huo ufahamu wako kwa kutoa hoja zako hapa, uwasaidie wengine. Hujasikia idadi ya watu waliokufa wakiwa njiani kwenda kwa babu, wakiwa kwa babu, na waliokufa baada ya kutoka kwa babu? Unasubiri watu waendelee kufa ndio uwasaidie? It will be too late. Faida unayopata kwa kujiunga na JF ni nini sasa kama hutoi hoja wala kujibu hoja kwa ufahamu wako mkubwa? Mimi ntaendelea kusema. Sioni ajabu ukipinga. Yesu alipokuwa hapa duniani aliwaambia watu ukweli. Wakampinga, wengine wakataka kumpiga kwa mawe, hatimaye wakamuua. Lakini ukweli wake bado unaendelea kutangazwa hata leo.[/QUOTE]

Sikuelewi! Unamaanisha wakati wa Yesu hakuna waliokufa? Vipi yule mtoto wa askari ambaye ilibidi afufuliwe? Ina maana watu huwa hawafi makanisani mwetu wakiletwa kuombewa? Ina maana hao wagonjwa wasingekufa wakiwa hospitali? Babu alishasema kwa hekima kabisa kuwa wagonjwa wasitolewe hospitali bila ushauri wa daktari. Sasa kama watu wanatoroka hospitali kama tulivyosoma kwenye magazeti bado tumsingizie babu? Sikuelewi!
 
Ati? Am I smelling a heresy here? I doubt your theological understanding! God commands that we receive everything with prayer and thanksgiving. And you say hakuna haja ya kufaifanyia maombi ... Hapa si kama dawa inaponya au la; ila kila tukipokeacho twakipokea kwa shukurani na kwa kufanya hivyo hata sumu huhuishwa,
(1 Tim 4:4-5) For everything God created is good, and nothing is to be rejected if it is received with thanksgiving, 5 because it is consecrated by the word of God and prayer (NIV)
Kama hujaelewa, uliza utajibiwa. Huyo babu anadai ameoteshwa na Mungu kwamba hiyo dawa ni ya kuwaponya watu magonjwa manne/matano. Sasa maombi ya nini hapo? Mtu anakupa mkate halafu unamwomba tena akupe mkate? Si ndio hapo uongo wa shetani unapodhihirika?! Kumbuka pia unapoomba sio lazima ujibiwe "ndiyo", na sio lazima ujibiwe papo hapo. Huyo babu anasema matokeo ya dawa mtu ayatarajie ndani ya siku saba. Majibu ya maombi ni lazima yapatikane ndani ya siku saba? Kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu awarudishie pesa za nauli na hizo mia tano mia tano alizowatoza wale waliokwenda kwake na hawajapona. Kila lisilo la haki ni dhambi. Biashara za ujanja ujanja hazikubaliki
 
Sio kweli kwamba Babu wa Loliondo ametumwa na Mungu kutumia dawa hiyo kuwaponya watu. Huyo Babu ametumwa na "mungu wa dunia hii(shetani) ili kuwadanganya watu waache kumtumaini na kumwamini Mungu wa kweli ili hatimaye waangamie siku ile ya mwisho. Soma 2 Wakorintho 4:4 na kisha tafakari kwa makini hoja zifuatazo utathibitisha ukweli huo.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu. Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Jamani Watanzania “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo"
Siri imefichuka! Hoja hizo na maandiko hayo ya Biblia yanathibitisha wazi kwamba huyo Babu hajatumwa na Mungu. Ila ni shetani anamtumia kuwadanganya watu. Tusikubali kudanganywa. Hata waganga na wachawi wa leo na wao huwaambia wateja wao kwamba wanaponya au kufanya miujiza kwa uweza wa mungu. I dare to talk openly Huyo mungu wanayemtaja ni mungu wa dunia hii (shetani). Mwenye masikio na asikie.

Mbona tunajua makanisa yenu yamedoda watu wanakimbilia kwa babu sasa hivi.

Hapa tunaelewa fika sadaka mlizo kuwa mnakusanya kwa wanyonge sasa zimepungua mme waibia vya kutosha.
 
Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari

Ndugu, kama ufahamu wako ni mkubwa sana kuliko wangu, uonyeshe wazi huo ufahamu wako kwa kutoa hoja zako hapa, uwasaidie wengine. Hujasikia idadi ya watu waliokufa wakiwa njiani kwenda kwa babu, wakiwa kwa babu, na waliokufa baada ya kutoka kwa babu? Unasubiri watu waendelee kufa ndio uwasaidie? It will be too late. Faida unayopata kwa kujiunga na JF ni nini sasa kama hutoi hoja wala kujibu hoja kwa ufahamu wako mkubwa? Mimi ntaendelea kusema. Sioni ajabu ukipinga. Yesu alipokuwa hapa duniani aliwaambia watu ukweli. Wakampinga, wengine wakataka kumpiga kwa mawe, hatimaye wakamuua. Lakini ukweli wake bado unaendelea kutangazwa hata leo.[/QUOTE]

Sikuelewi! Unamaanisha wakati wa Yesu hakuna waliokufa? Vipi yule mtoto wa askari ambaye ilibidi afufuliwe? Ina maana watu huwa hawafi makanisani mwetu wakiletwa kuombewa? Ina maana hao wagonjwa wasingekufa wakiwa hospitali? Babu alishasema kwa hekima kabisa kuwa wagonjwa wasitolewe hospitali bila ushauri wa daktari. Sasa kama watu wanatoroka hospitali kama tulivyosoma kwenye magazeti bado tumsingizie babu? Sikuelewi![/QUOTE]

Maana yangu ni hii: wengi wanaokwenda kwa babu wanaenda wakijua mia kwa mia kwamba watapona. Lakini mambo yako kinyume. Hawaponi wote. Na hii ni kwa sababu ya roho ya udanganyifu inayotenda kazi ndani ya huyo babu. Ndio maana nimeanzisha mada hii ili kuwatahadharisha Watanzania wenzangu wasikubali kudanganyika.
 
Kama hujaelewa, uliza utajibiwa. Huyo babu anadai ameoteshwa na Mungu kwamba hiyo dawa ni ya kuwaponya watu magonjwa manne/matano. Sasa maombi ya nini hapo? Mtu anakupa mkate halafu unamwomba tena akupe mkate? Si ndio hapo uongo wa shetani unapodhihirika?! Kumbuka pia unapoomba sio lazima ujibiwe "ndiyo", na sio lazima ujibiwe papo hapo. Huyo babu anasema matokeo ya dawa mtu ayatarajie ndani ya siku saba. Majibu ya maombi ni lazima yapatikane ndani ya siku saba? Kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu awarudishie pesa za nauli na hizo mia tano mia tano alizowatoza wale waliokwenda kwake na hawajapona. Kila lisilo la haki ni dhambi. Biashara za ujanja ujanja hazikubaliki

Nakuelewa sana. Wale wanaokuja kwenye mikutano ya injili ambayo huwa twabandika mabango kuwa waleteni wagonjwa na wenye udhaifu wote. Twaandika vipofu, viwete na wenye udhaifu ... Je hawa wasipopona twawarudishia nauli? Ni kweli sio lazima ujibiwe hapo hapo na ndio maana babu anasema ndani ya siku 7.
 
Suala la mtu kwenda kwa babu akijua atapona si ndio imani tunayohubiri? Hata hivyo uponyaji wenyewe si twamwachia Mungu?
 
nakuunga mkono na nina amini usemayo babu simkubali hata kidogo umetoa fact za ukweli ahsante sana mdau.
 
watanzania tumepoteza matumaini, na tunashambuliwa na maradhi ya kila aina, tutakaposikia kuwa kuna matumaini tutaenda angalau tuepuke shida za miili yetu inayoghadhabika na mateso, ndo maana ndugu zetu wanakwenda kwa babu, kama kuna kwingine unajua zaidi ya hapo ambako hawatoi hela koz unadai mia tano ni nyingi, tuelekeze tupeleke ndugu zetu,usiongee kwa sababu ya ushabiki wa kitabu cha bibilia, kama kweli umewai kuuguza ngugu yako kwa muda wa zaidi ya miaka 10,usiku na mchana, hata wewe ungejihimu kwenda kwa babu kumpeleka akanywe dawa. mwacheni babu
 
ole wenu nyie mnaotaka kuokoa miili yenu na kusahau kuokoa nafsi zenu.....kwani nyie ni mavuno ya shetani. Simkatazi mtu kwenda kwa babu but chekini hizi end times.......coz kuna maajabu mengi yanakuja na wengi mtapotoka....shetani anatumia hizi times kuvuna watu wake...so nyie mliochaguliwa kuona basi na muwe na msimamo na imani msijetikiswa na vituko vya shetani.....

Nyie shallow seekers mmekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..............

if interested in knowing something , follow this link and find 4 ya self....

False Prophets - Sananda - Maitreya - St. Germaine - Benny Hinn - Beast Prophets from Hell

peace and love

alifazza ze blakk wadada
 
Mbona tunajua makanisa yenu yamedoda watu wanakimbilia kwa babu sasa hivi.

Hapa tunaelewa fika sadaka mlizo kuwa mnakusanya kwa wanyonge sasa zimepungua mme waibia vya kutosha.

Mr Fidel, mimi sio Mchungaji. Hivyo hoja hiyo ya kuwaibia watu sadaka, hapa sio mahali pake. Isitoshe sadaka ni jambo la hiari. Sasa unaposema wachungaji wanawaibia watu sadaka sijui unamaanisha nini? Kiswahili kinakupa shida nini? Should we explain ourselves in English/French?
Anayewaibia watu ni huyo babu. Maana pona usipone lazima 500 zitakutoka(plus nauli ya kutoka Arusha, Bukoba, Mwanza, Kenya to Loliondo). Mh, poleni. Kama huyo babu mnaona ndio mkombozi wenu, si mumhamishie Arusha mjini? Abebe na miti yake yote? Kuliko watu waendelee kuteseka kumfuata porini? Waganga wengi wa kienyeji ndio wanaopenda kukaa porini porini au vichochoroni.
 
Sababu zote ulizotoa zinaonyesha huelewi huduma anayoifanya Mchungaji Masapila na pili unavyotumia Maandiko Matakatifu unaonyesha ufahamu mdogo sana. Nakushauri kabla hujasema ama kuandika jambo utafakari[/QUOTE]

Ndugu, kama ufahamu wako ni mkubwa sana kuliko wangu, uonyeshe wazi huo ufahamu wako kwa kutoa hoja zako hapa, uwasaidie wengine. Hujasikia idadi ya watu waliokufa wakiwa njiani kwenda kwa babu, wakiwa kwa babu, na waliokufa baada ya kutoka kwa babu? Unasubiri watu waendelee kufa ndio uwasaidie? It will be too late. Faida unayopata kwa kujiunga na JF ni nini sasa kama hutoi hoja wala kujibu hoja kwa ufahamu wako mkubwa? Mimi ntaendelea kusema. Sioni ajabu ukipinga. Yesu alipokuwa hapa duniani aliwaambia watu ukweli. Wakampinga, wengine wakataka kumpiga kwa mawe, hatimaye wakamuua. Lakini ukweli wake bado unaendelea kutangazwa hata leo.[/QUOTE]

.
Sasa kwa uelewa wako kinachowaua hao wagonjwa walio njiani kuelekea kwa babu ni nini?
Pia kanisani kwako unaposali kuna wafuasi wengi walishakufa toka ujiunge nalo ni nini kiliwaua?
.
 
Also nyie mnao sema "babu" .....mbona msiseme kuwa ni MUNGU ANAWAPONYA? funny apocalypse mind playing trixx shit. Repent!!!!!!!!!!!!! Coz watu wanakunywa "dawa" then bado ndo hao nawaona kila siku wakifanya mambo ya kishwaiiin mtaaani...so MUNGU anataka kuokoa nafsi ama mwili? Coz bila nafsi kukiri kuwa hicho "kikombe" ni dawa,,,,basi mwili hautapona.........

............................so ... nyie binadamu mnaosota kwa matatizo ya miili yenu, tubuni na muwe safi kwa undani kabla ya kusafisha kwa nje maana kuna haja gani ni bora kati ya safuria iliyo chafu kwa nje na ndani ni chafu au iliyo chafu kwa masinzi kwa nje ila ndani ni safi ????

kwenye hiki kizazi cha nyoka few will escape damnation of hell........

poleniiiiiiiiiii
 
Haka ni kafuasi ka ushabiki maandazi, kameposti humu ili kuzidi kujipendekeza kwa
mkuu wake ili kaonekane kanamsadia mkuu kazi ya Bwana.

Sio siri, wengi wa hawa wachungaji wa miujiza, wana capitalize kwenye shida za waumini wao, na makanisa yao yanafurika waumini wenye shida mbalimbali, ambapo tangu kuibuka kwa babu, waumini wao wenye shida wamekimbilia Loliondo hivyo wanagopa wakipona, hawatarudi tena makanisa yao, hivyo wao kukosa sadaka.

hapo panaukwel ndani yake.
 
Nafikiri huyo bwana anafanya biashara ya ARV na rostam Azizi. Anaona sasa wagonjwa wanapungua anaanza kumpiga vita babu. Si ulisikia hata Rostam anavyompinga babu.? Kama afya ni mgogoro kapige kikombe kwa babu fanya PM.
 
Mr Fidel, mimi sio Mchungaji. Hivyo hoja hiyo ya kuwaibia watu sadaka, hapa sio mahali pake. Isitoshe sadaka ni jambo la hiari. Sasa unaposema wachungaji wanawaibia watu sadaka sijui unamaanisha nini? Kiswahili kinakupa shida nini? Should we explain ourselves in English/French?
Anayewaibia watu ni huyo babu. Maana pona usipone lazima 500 zitakutoka(plus nauli ya kutoka Arusha, Bukoba, Mwanza, Kenya to Loliondo). Mh, poleni. Kama huyo babu mnaona ndio mkombozi wenu, si mumhamishie Arusha mjini? Abebe na miti yake yote? Kuliko watu waendelee kuteseka kumfuata porini? Waganga wengi wa kienyeji ndio wanaopenda kukaa porini porini au vichochoroni.

hayo maneno unayosema hujaumwa lakini kwa wale ambao wamepona wana haki ya kumshukuru Babu na Mungu wao.
 
hii dawa mimi siiamini, na siihitaji. hapa ofisini kwetu hata wasio wagonjwa wanaenda kunywa, sasa sijui ni kwaajili ya nini?
 
wewe unayeyafahamu maandiko vizuri yufafanulie sasa, sio kuponda tu na huleti wazo lolote la maana

Ndugu yangu ukisema neno la haki ya Mungu utaona jinsi wapingaji wanavyojiinua ,sema ngono uone watakavyo kusupport , neno la Mungu, 2wathesalonike 2:11 " kwa hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu wauamini uongo iliwahukumiwe wote ambao hawakuamini kweli bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu"
 
Mbona tunajua makanisa yenu yamedoda watu wanakimbilia kwa babu sasa hivi.

Hapa tunaelewa fika sadaka mlizo kuwa mnakusanya kwa wanyonge sasa zimepungua mme waibia vya kutosha.

Wala huna haja ya kutoa kashfa, JF ni uwanja wa hoja tu. If you cannot keep up with the pace of constructive arguments i suggest you read opinions and keep quiet.
 
watanzania tumepoteza matumaini, na tunashambuliwa na maradhi ya kila aina, tutakaposikia kuwa kuna matumaini tutaenda angalau tuepuke shida za miili yetu inayoghadhabika na mateso, ndo maana ndugu zetu wanakwenda kwa babu, kama kuna kwingine unajua zaidi ya hapo ambako hawatoi hela koz unadai mia tano ni nyingi, tuelekeze tupeleke ndugu zetu,usiongee kwa sababu ya ushabiki wa kitabu cha bibilia, kama kweli umewai kuuguza ngugu yako kwa muda wa zaidi ya miaka 10,usiku na mchana, hata wewe ungejihimu kwenda kwa babu kumpeleka akanywe dawa. mwacheni babu

Poleni. Nawaonea huruma ndio maana nimetoa muda mwingi kutoa hoja zangu hapa. Ukienda kwa babu si unaamini kwamba utapona kwa imani? Kama utapona kwa imani, kwanini usiyaamini maneno ya Biblia hapo hapo chumbani ulipo na mgonjwa wako kwamba mtapona? Uponyaji wa Yesu upo mahali popote na kwa dakika yoyote kwa mtu yeyote anayeamini. "Yote yawezekana kwake aaminiye" Yesu alisema ni baba yupi ambaye mwanawe akimuomba mkate atampa jiwe? hakuna! Vivyo hivyo tukimuomba Mungu Baba yetu kwa Jina la Yesu, atatuponya. Ila kama huwezi kuomba mwenyewe, bado kuna sehemu nyingi ambapo maombezi yanafanyika kwa wagonjwa na watu wanapona. Vipindi vingi katika redio na TV za Kikristo za hapa TZ na nje ya nchi vina maombezi kwa wagonjwa. Na wale wanaoamini wanapona hata katika sitting room zao tu Ila nimesema awali kwamba tatizo la wengi wanataka tu wapone halafu waendelee na dhambi zao. Wakiambiwa waokoke hawataki hata kusikia. Ndio sababu wanakimbilia kwa babu maana huko hawahubiriwi Injili inayochoma mioyo yao. Dhambi zao hazikemewi. (Matendo ya Mitume 2:37-43). Mungu anataka tupone mwili anataka pia tupone roho zetu kisha tuingie kwenye raha ya milele mbinguni. Ukipona kisukari, kansa, ukimwi leo, kisha kesho ukafa na kwenda jehanam, utakuwa umepata faida gani? Maisha yetu duniani ni mafupi. Miaka 70 au tukiwa na nguvu miaka 80. Tufikirie maisha yajayo yenye raha na uzima usio na mwisho. Shetani hapendi tuujue ukweli huu ndio maana anajaribu kila njia kutufumba macho ili tupotee pamoja naye jehanam, maana yeye tayari amekwishahukumiwa. Lakini Mungu kwa huruma zake amekupa nafasi hii ya kusoma hoja nilizoziandika ili uepuke udanganyifu wa shetani ndani ya babu wa Loliondo. Ni juu yako kukubali au kukataa.
 
Back
Top Bottom