Sipo hapa kuitetea CHADEMA - Baregu

mzee slaa akisikia msimamo wa baregu anatamani ammeze kwa kuwa yeye anapenda kuabudiwa.
 
Ukisoma falsafa vizuri inakusaidia kujenga hoja na kuitetea hata kama itakuwa ni kwa nchi yako ilimradi hoja yako iwe na misingi makini ...Kwa hili CDM tukubali hoja ya mwenzetu ili itupatie nafasi ya kuwabana na wengine wanaofata misimamo ya vyama badala ya matakwa ya wananchi walio wengi na ambao kimsingi hawana hata vyama...
katiba ni ya watanzania katika hili tuache siasa ambazo hazitalisaidia Taifa hili huko twendako
 
Kwa mtizamo wangu Prof kaonyesha kiwango kidogo cha ufahamu,
Katika hili kwanza alitakiwa kuwasikiliza kwanza ,ili aweze kuthibitisha kama hicho alichokifikiri ndicho walichomuitia.Kwani huwa hatukatai wito bali tunakataa neno.Na pengine haya majibu alitakiwa awape kulekule walikomuita.Lakini kuja nayo public na kutangaza ,naona ni usanii wa aina fulani wa kujitengenezea umaarufu, ili baadae ajione shujaa, na si ajabu siku ukimsikia karudi CCM.

Jambo la pili ,hili suala liliishapita siku nyingi ,kwa nini analirudiarudia kama mfano sehemu tofautitofauti kuna ajenda gani?

Kwangu mimi Huyu Prof,japo namuheshimu sana ,lakini kwenye hili napaswa kumuweka kwenye mabano,kama ana ajenda binafsi tutaiona mbele ya safari.
 

umesoma gazeti la majira lakini?
 
Nadhani viongozi wa CHADEMA walijaribu kutingisha kiberiti wakakuta kimejaa njiti.

Tanzania imebakiwa na wanasiasa wachache sana wanaofanya kazi kulingana na Sheria, kanuni, miiko na misingi ya kazi zao.

Prof. Baregu alionyesha kama ni mmoja wa wanasiasa hao.
 
Hilo ndo jambo la msingi, kwenye tume tunahitaji UTANZANIA wala siyo UCCM wala UCHADEMA!!!
 

sasA huyu afanywe kwama mansour wa ccm kwa kwenda kinyume na chama atimuliwe chadema
 
Kwani ni wapi tulisema yupo kwenye tume kutetea msimamo wa CHADEMA?

Mkuu. Tatizo kuna watu wanaangalia mambo kiushabiki sana bila mantiki, Chadema kuna mambo ya msingi sana tunayaunga mkono kwenye rasimu ya katiba ambayo mwenyekiti wake ni Warioba. haimaanishi kuwa kwa kuwa tunayaunga mkono basi tunamuunga mkono Warioba kwenye kila kitu na hiyo haimaanishi kuwa kwa kuwa kuna mambo tunayaunga mkono kutoka kwa Warioba basi tunaunga mkono ccm kwa kuwa Warioba ni kada wa ccm. Kinyume chake kwa Baregu.
 
Huyu kaja kuwapotezea muda nanyi mnaanza kuwaka bila kuwaza.Haya yalijitokeza mwanzoni sana wakati Baregu akisema maneno haya .Leo huyu kaamua kuwapotezea muda kwa kuleta kipande kidogo watu wameanza kulipuka .Mbona aweki habari nzima ?Ushabiki wa kijinga this is not news any more yalishapita ilikuwa pale mwanzoni Kamati ilipo mtaka ajitoe akajibu haya .
 
Tatizo ni pesa na si Utanzania anavyoda, mabilioni yanamkengeusha Baregu!!!!!!!!
 

Pamoja na msimamo wake huu mzuri (namuunga mkono 100%) angefika tu kuwasikiliza hao wna kamati kuu wenziye hoja zao na kuwapa msimamo wake.......kuwakwepa ni upungufu wa kimsimamo kwa upande mwingine
 

Kwani mtu akigoma kuitikia mwito wa kamati ambayo ni moja ya vyombo vya utendaji wa chama ambacho yeye ni mwananchama na kiongozi ndipo anapoonekana mzalendo? Kwanini mwandihi unatuletea habari nusunusu? Kama aliitwa kweli na kuigomea kamati ina maana alijua nini kamati ingemwambia? Hapa ndipo ninapopata shida na habari hii na kuiona kama uvumi maana kama ni kweli Profesa aliitwa na kamati na kwa bahati nzuri akapewa agenda za kikao na akakataa kuhudhuria amejinyima fursa ya kuwa Profesa na mwalimu mzuri maana angweza kutumia agenda hizo kutoa elimu kwa viongozi wengine wa CDM na Watanzania kwa ujumla. Kama anaamini siasa ni kukubali kutokukubaliana angekwenda akawasikiliza na kuifikia doctrine ya agree to disagree. Mimi naona hiki alichokifanya ni kuwa megalomenic
 
Na wajumbe ambao ni makada wa CCM, tuna uhakika gani kama hawatazingatia maslahi ya chama chao? Isije kuwa kwa Chadema tu wakati wenzake wa CCM wanapeta tu, Hatutamuelewa kwa kweli.
 
kama slaa na mbowe wana ubavu wamfukuze baregu kama madiwani wa arusha. Baregu ameidharau kamati kuu ya chdm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…