Sipendwi; jamani nina nini mie?!

huwa kuna kukataana tena baada ya kuwowana?

Ipo sana si ndio talaka ilipo zaliwa hapo!!! hata ukiwa mkatoliki basi utakataliwa sema tu hutaweza kuacha utakufa kishujaa!
 
Sidhani kama kila mwanamke aliyeolewa bs kaolewa na mwenye hela bs wanawake wote tungekuwa tunazo dunia hii hata makazini tusingeenda.

Mke mwema hutoka kwa Mungu wala usikate tamaa utampata tu na usiwe na haraka nao.
 
Calm down! Kubwa na zuri jaribu kutafuta msichana anayeendana na hali yako,anayekataa mwache aende.Najua mwaka huu utapata tu.
 
Pole kaka mke mwema anatoka kwa mungu subiri utapata wa kwako haijalishi umekataliwa na wangapi yakupasa kujua wa kwako ni mmoja tu atakaekupenda kama ulivyo wewe bila vigezo subiri vumilia mungu ataleta kheri yake.


Nayanda.

Umesema yaliyo kweli kabisa, pia akumbuke kumwomba mungu ili akumbuke hitaji lake na hayo mapungufu kama ufupi, pesa na mengine hayana kipimo katika kumpata mke ulieumbiwa na mungu kabla ya kuzaliwa.....NOTE; KAMA UNAWATAFUTA KWA KUTOA AHADI ZA UCHUMBA NA NDOA ITAKUCHUKUA MUDA MREFU KUPATA WA UKWELI.
 
mpe pole., ila mwambie mke mwema hutoka kwa Mungu fullstop!
 
kweli kei zinawehusha, zaweza mtoa mtu duniani bila kujua! haya nimejibanza hapa dirishani nachungulia, tiririkeni, lol!
 
Sasa kama huna hela kweli ulitaka wakwambiaje?saka mkwanja watajipanga wenyewe tu.
 
Hakuna wa kukataa ndoa siku hizi. Tatizo kubwa kwako ni kuchagua watu wa hadhi tofauti na yako. Tulia, chagua mwalimu mwenzako kisha tuone.
 
Mke mwema anatoka kwa MUNGU! Usiwe na hasira wala kinyongo! itafika wakati utawakimbia wewe mwenyewe.
 
nenda kasome may be inaweza kukuongezea kipato,kama huwezi kwenda shule nenda kijijini kwa babu zako huko utapata wanawake kwa urahisi kidogo,kwani kule bado hawajawa kimaslahi kuliko wa huku mjini
 
Duh walisema mwanamke mzuri sio sura ni tabia...sasa sijui kwa mwanaume kamsemo kake ni kepi?

Kaka usijali...utapata tu mwenza...subira huvuta kheri.

nani kakueleza ya kuwa haupendwi au waishi kwa hisia zako tu badilika ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo
 

Pole kaka, ufupi sio sababu, mbona hata mbilikimo wanapata wapenzi?. Wako yupo tu kijana, usiwe na haraka maana kiwanda chako kinaendelea kuzalisha mbegu hadi tone la mwisho. Ualimu pia sio tatizo, walimu wengi wameoa wake wazuri na maisha yanasonga. Swala la msingi kaka uwe na mipango ya kimaendeleo, ongeza kipato, ongeza elimu yako usibweteke na huo ualimu. Fungu la mara moja kwa mwezi kwa maisha ya wamama wa leo ni balaa, haiyoshi. Angalia matumizi yalivyoongezeka kwa akina mama, atataka simu nzuri, vocha uweke, saruni aende, kodi ya nyumba ulipe, umeme, maji, chakula...........n.k. Mwenzako nilikuwa teacher, nikafundishwa 1.5 yrs, nikaona ndoto zangu zitachelewa so nikachapa mwendo. Nikaajiriwa sehemu nyingine napo nikaona bado kazi ngumu, nika-fight kupata ufadhili, sasa namalizia ka-master kangu ng'ambo ya nchi. Wale wote waliokuwa wanajifanya wazuri hata e-mail zao sizijibu siku hizi, maana imekuwa kero. Kwa sasa nachagua tu kitu roho inapenda.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…