Sipendwi; jamani nina nini mie?!

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,520
764
Jirani yangu aliponikuta nasoma Jf alivutiwa sana jinsi wanaJF wanavyokuwa msaada na aliniomba niwasilishe kwenu tatizo lake kwa ushauri,,anasema
"Mimi ni kijana mwenye miaka 28 ni mtoto wa kwanza ktk familia.Tangu nimeamua kuoa hapo ndipo matatizo yalipoanza,kila mchumba alinikataa kwa sababu yake,,wa 1.alisema mi mfupi (ni kweli )
wa pili,,alisema sina pesa(kazi yangu mwl sek)
wa tatu,,alisema anaenda masomoni ila wiki chache baadae akaolewa pengine.
Nimefikisha wachumba 12 na kila mmoja aliondoka kwa sababu zake.
Naombeni ushauri wenu maana hitaji la kuoa linaniumiza naanza kukata tamaa au nimeumbwa kuishi pasipo mwenzi? Au nina nini jamani? Umri unaenda kuna faida gani mtu kuishi pasipo mwenzi? Sinywi pombe,sio mhuni,afya njema Tatizo ni nini,nisaidieni''
NAOMBA KUWASILISHA
 
Duh walisema mwanamke mzuri sio sura ni tabia...sasa sijui kwa mwanaume kamsemo kake ni kepi?

Kaka usijali...utapata tu mwenza...subira huvuta kheri.
 
hizo ni kama excuse zao tu.labda huna hela,maana wadada wa siku hizi wengi hupenda kupewa.kwa nini asitafute mdada kulingana na alichokuwa nacho?labda atafute wa uswahilini ambao hawana makuu
 
Duh walisema mwanamke mzuri sio sura ni tabia...sasa sijui kwa mwanaume kamsemo kake ni kepi?

Kaka usijali...utapata tu mwenza...subira huvuta kheri.

Mwanaume anaangaliwa kwa vitu viwili na wanawake je unapesa? Je una uwezo binafsi kwenye kungonoka/ngono/kumega?
Ukiwa na kimoja wapo ni siraha tosha kuwanasa warembo wote
 
wewe tatizo lako moja tuu mwana...huna mkwanja mwana. trust me bwana asikundanganye mtu mkwanja + dushelele ndio wanawake wanataka in that specific order.
mie mwenzio wakati nipo jobless kona nilikuwa natemwa balaa nikaja kukumbuka msemo wa mama mzazi ambao ndio moja ya signature yangu kuwa wen poverty enters thru the door love escapes thru the window. ina ukweli hiyo mwana.
sasa wewe naona itabidi ukubali ukweli kuwa hutapata mwenzi maana ndoa imekuwa biashara...only the highest bidders win!!!!
 
Pole kaka mke mwema anatoka kwa mungu subiri utapata wa kwako haijalishi umekataliwa na wangapi yakupasa kujua wa kwako ni mmoja tu atakaekupenda kama ulivyo wewe bila vigezo subiri vumilia mungu ataleta kheri yake.

Nayanda.
 
Tafuta hela wewe piga tution sana kusanya fedha fungua duka la urembo then utaniambia gafla tu utakuwa handsome na utawakimbiaaaa kazi ni kwako.
 
Atampata atakayemfaa. Ukizidi kutafuta wachumba utajikuta utakataliwa hata na right candidate kwa vile atajua kuwa wewe ni mcharuko
 
bro ni heri yako iyo, bora ukataliwe kabla kuliko kukataliwa ukishaoa

wenye tabia nzuri hawapendwi hata na walokole! Sijui kwa nini? Unakuta mdada kaacha mwanaume aliyetulia kaenda kuolewa na dude chakaramu aafu baadaye analalamika mumewe hajatulia. Umri wako bado unalipa, fanya maendeleo hawa viumbe wapo tu. Ila usiwe desparate aafu ukakutana na desparate girl!
 
Lakini haya mambo mie siyaelewi, kuna jamaa alikuwa kishakataliwa na mabinti 24 lkn mwaka huu mwanzoni kapata aliyempenda kama alivyo.Chakushangaza baada ya kujua amechumbia miongoni mwa wale24 waliomtosa before wameanza kurudi kwa kasi sana.Hivi hili huwa linamaanisha nn??
 
Uyu mchiz nimegundu tatizo lake ts seems he is too decent to these chicks akifikiri atapendw kw kua decent,pili hapo kwene hela..jitahidi uongeze vyanzo vya mapato,badili maisha yako du yo things viwe ktk mpango hata dem akija gheto apagawe,tatu inabidi uelewe kwmba hata kichaa akitaka dem anapata,ni strategy tuu.
 
Mimi nahisi ni shetani..adi wadau wananshangaaga..kuna kipindi nkiwa sina demu..kila demu nkimtokea anazingua,nkatafuta play boy mmoja hivi aliyeshindikana nkawa nahang nae out kuusoma mchezo nkagundu jambo la kijinga sana..the more unavyokua na mademu na ukasex nao ndo sijui wankuachia kapepo kakuvutia madem wengine cozi as nlipata dem,hapo hapo wengine ndo wakajileta,nkawa na watatu hata wale wlionikataa awali wakaja..nahisi madem wanafata harufu ya wanakogemuliwa sana..my take..usiogope mwanamke ni wa kawaida sana ht km kakuzidi umri
 
Pole kaka mke mwema anatoka kwa mungu subiri utapata wa kwako haijalishi umekataliwa na wangapi yakupasa kujua wa kwako ni mmoja tu atakaekupenda kama ulivyo wewe bila vigezo subiri vumilia mungu ataleta kheri yake.

Nayanda.

wealth and houses are inherited from fathers but prudent wife comes from the Lord.keep praying kaka kwani imeandikwa kila mtu atapewa wa kufanana nae,hivyo ata wewe utapewa wa kufanana na wewe.
 
Uyu mchiz nimegundu tatizo lake ts seems he is too decent to these chicks akifikiri atapendw kw kua decent,pili hapo kwene hela..jitahidi uongeze vyanzo vya mapato,badili maisha yako du yo things viwe ktk mpango hata dem akija gheto apagawe,tatu inabidi uelewe kwmba hata kichaa akitaka dem anapata,ni strategy tuu.

mkuu nimependa sana analysis yako, na like umepata tatizo ni jinsi unavyochanganya hizi lugha, sasa hapo nilipo bold sijapaelewa
dogo azingatie ushauri huu ni uko poa mazee
 
Lakini haya mambo mie siyaelewi, kuna jamaa alikuwa kishakataliwa na mabinti 24 lkn mwaka huu mwanzoni kapata aliyempenda kama alivyo.Chakushangaza baada ya kujua amechumbia miongoni mwa wale24 waliomtosa before wameanza kurudi kwa kasi sana.Hivi hili huwa linamaanisha nn??

Baadhi yao hawana maamuzi binafsi wanakuwa wanaangalia-angalia wanaishi kwa macho ya watu, wakiona umekubaliwa sehemu (ambayo wanaiona babu kubwa) basi ndio na wao watakuja mbio utadhani kuku wanaoshindana kuikimbilia punje moja ya mahindi.
 
hizo ni kama excuse zao tu.labda huna hela,maana wadada wa siku hizi wengi hupenda kupewa.kwa nini asitafute mdada kulingana na alichokuwa nacho?labda atafute wa uswahilini ambao hawana makuu

Nahisi kama umegundua tatizo!
Huyu mwalim atakuwa hajapata mchumba mchumba, nikimaanisha mchumba anaeendana na alivyo na kipato chake
wavulana wamekuwa wakuvutiwa na kuwaendea wasichana ambao wana style ya juu ya maisha. hili ni tatizo, yule
wa juu tunaita zali mpaka akupende wewe na hapo ujaribu kujinasua ukiona amekuganda pasi anakupenda kweli!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom