Sipendi kukosea kuandika haya maneno kwa ufasaha

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
63,622
112,699
Sipendi kuchanganya l na R katika uandishi, muda mwingine inabidi niepuke kutumia baadhi ya maneno ili nisiyakosee, naomba kueleweshwa haya maneno yanaandikwaje kwa ufasaha.

Je ni lipi sahihi
kachumbali au kachumbari?
Kulogwa au kurogwa
Mkwala au mkwara?

Nitaongezea nitakayokumbuka.
 
Sipendi kuchanganya l na R katika uandishi, muda mwingine inabidi niepuke kutumia baadhi ya maneno ili nisiyakosee, naomba kueleweshwa haya maneno yanaandikwaje kwa ufasaha.

Je ni lipi sahihi
kachumbali au kachumbari?

Kulogwa au kurogwa
Mkwala au mkwara?

Nitaongezea nitakayokumbuka.

Sahihi
Kachumbari
Kurogwa
Mkwara
 
Kusali / kusari??
au
Kuswali / kuswari??

(Nikiwa na maana kitendo cha kufanya ibada)
 
Sahihi ni Tafsiri

Fasili/fasiri maana yake nini?
kiswahili kipana mama
hebu cheki hapa
IMG_20180212_055508_698.JPG
 
ongeza pia

mkristo?
mkristu?

tafakuri
tafakari?
Mkristo/ mkristu, yote ni sahihi. Nimeona kristu hutumiwa zaidi na wakatoliki, na wengine husema kristo.

Tafakuri ni sahihi
Tafakari ni sahihi
Ni maneno tofauti kwa uelewa wangu, tafakuri ikiwa ni funzo/somo unalolipata katika au baada ya tafakari (kufikiri kwa kina).
 
ongeza pia

mkristo?
mkristu?

tafakuri
tafakari?
Tafakari na tafakuri nnavojua mie yote ni maneno sahihi ila maana zake ni tofauti.
Tafakari ni kitendo cha kuwaza na kuwazua
Tafakuri ndio hayo uliyoyawaza sasa, yani tafakuri imetokea baada ya kutafakari (sijui nipo sawa!!)

Mkristu na mkristo hapo nadhani ni utofauti wa namna ya kutamka kati ya sehemu na sehemu
 
Back
Top Bottom