Tusiwalaumu viongozi kutumia maneno yasiofaa, lugha ni tatizo na sio kizungu tuu, hata kiswahili

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,684
119,321
Wanabodi,

Tusiwalaumu viongozi wetu kutumia baadhi ya maneno yasiofaa au yasistahiki tukidhani viongozi hao, wanafanya makusudi, tuwasamehe bure viongozi hawa, maana kiukweli kabisa, kuna uwezekano, baadhi yao, na wengine wao, hawafanyi makusudi bali hawajui, ila hawajui kuwa wanakosea, kwa sababu hakuna anayewaambia wanakosea, waliowazunguka, wanajua wanakosea, kuwaambia kuwa wanakosea, wanaogopa, na badala yake, wanawaacha wazidi tuu kukosea. Huku sii kuwasaidia.

Kuna watu wanawabeza eti baadhi ya viongozi hawajui kutamka vizuri baadhi ya maneno ya lugha ya Kiingereza kwa ufasaha, yaani fluently, kusema ukweli, baadhi ya viongozi wetu, sio tuu hawako fluent kwa Kiingereza tuu bali hata kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, baadhi ya matamshi ya baadhi ya maneno ya Kiswahili, kuyatamka kwa Kiswahili sanifu na Kiwahili fasaha kwa baadhi ya viongozi wetu ni tatizo.

Leo nimemsikia kiongozi wetu mmoja, mkubwa tuu serikalini, akizungumza mahali fulani, akitamka neno "nimefulahi" badala ya "nimefurahi " au "watoto wazuli" badala ya "watoto wazuri", hivyo tatizo sio Kiingereza tuu pekee, kusema hii ni lugha ya watu, kumbe hata kutamka baadhi ya maneno ya Kiswahili fasaha ni tatizo kwa viongozi wetu, wanachanganya "L" na "R"
hivi hawa wasaidizi kazi yao ni nini?.

Ila pía na sisi waandishi tunachangia kuwachoresha viongozi wetu, wewe kama mwandishi unaejua matumizi sahihi ya matamshi, uko na kiongozi kwenye tukio, kiongozi amechapia, kwa kuchanganya L na R, kwani lazima uitumie hiyo clip ya kuchapia kama insert ya news ya kiongozi aliyochapia?!.

Waandishi tuna jukumu la kuepusha kuwachoresha viongozi wetu wanapochapia lugha ili tusiwadhalilishe, lakini wasaidizi wao wana jukumu la kuwasaidia, hata wakiwa wakubwa vipi, wakikosea, waelekezeni ili watamke maneno kwa ufasaha.

Najua kuna watu watanibeza kuwa kuchanganya R na L ni jambo dogo tuu, asirekebishwe, ukiaanza kuachia hivi vikosa vidogo vidogo, mbele ya safari kutatokea makubwa na kushindwa kurekebisha, kwa sababu, hata mbuyu, huanza kama mchicha.

Paskali
 
Wanabodi,

Tusiwalaumu viongozi wetu Kutumia baadhi ya maneno yasiofaa tukidhani wanafanya makusudi, tuwasamehe bure maana kiukweli wengine sio makusudi bali hawajui.

Kuna watu wanawabeza eti baadhi ya viongozi hawajui kutamka vizuri maneno ya lugha ya Kiingereza, kusema ukweli sio Kiingereza tuu bali lugha na matumizi sahihi ya maneno ni tatizo kwa baadhi ya viongozi wetu.

Leo nimemsikia kiongozi wetu mmoja akizungumza mahali akitamka neno "nimefulahi" badala ya "nimefulahi" au "watoto wazuli" badala ya "watoto wazuri", hivyo sio Kiingereza pekee ni tatizo kwa viongozi wetu, hata Kiswahili.

Ila pía na sisi waandishi tunachangia kuwachoresha viongozi wetu, wewe kama mwandishi unaejua matumizi sahihi ya matamshi, uko na kiongozi kwenye tukio, kiongozi amechapia, kwani lazima uitumie hiyo insert ya kiongozi aliyochapia?!.

Waandishi tuna jukumu la kuepusha kuwachoresha viongozi wetu wanapochapia lugha ili tusiwadhalilishe.

Paskali
Hapo kwenye "red" hebu na wewe rekebisha basi,unapotaka kumkosoa mtu jaribu kua makini zaidi.
 
Back
Top Bottom