Sipati wanaume wa rika langu

Sipati wanaume wa rika langu

Kama umeweza kuleta masikitiko yako JF, humu nina imani utakutana na vijana wenzako, sharti usiwe mchoyo. Safari moja huanzisha nyingine, karibu PM.
 
young_ma njoo pm tufanye utaratibu wa kufahamiana na kujuana taratibu ili baadae nilete posa.

kutoka: 22D Arnold st.
 
Jamani nisaidieni mimi ni binti wa mikaka 25, mara nyingi nipo nyumbani tuu. Wazazi wangu hawapendi nitoke tangu mdogo hivo nimekua mtu nsie na social life

Yani maisha yang ni nyumbani, kazi za nyumbani, yani sikutani na vijana wa umri wangu kabisa.

Na ninapo fanya kazi wengi ni watu wazima na familia zao
Hivyo mara nyingi naishiwa kutongozwa na waumme za watu.

Hichi kitu kinanivunja moyo kwani natamani siku nipate mwenza na kufunga ndoa.

Ila naona umri unaenda na nimekua single kwa mda mref sana.

Nyumbani posa zilikuja kama tatu ila sipendelei kuozwa na mtu nsomjua wala nsompenda.

Naombeni msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
uzoefu wangu wa kuzaliwa tanzania, kusoma tanzania na kuishi tanzania unaonyesha vijana wengi wa rika lako(miaka 25) bado hawajafanikiwa kimaisha kiasi cha kuwa na financial confidence ya kuja kukuposa.

ni vijana wachache sana wa umri huo waliofanikiwa kimaisha. majority ya vijana wa kitanzania wanaanza kufanikiwa na ku settle kimaisha wakiwa between 30 and 40 kwasababu hicho ndio kipindi ambacho wengi wanakuwa washamalizana na issue za masomo ya vyuo kikuu. ndio kipindi ambacho wale waliojaribu kuomba ajira katika taasisi mbalimbali wanakuwa tayari wameshabahatika kupata ajira.

hiyo ndio sababu inayofanya uwe approached na vijana wenye umri mkubwa zaidi yako.
 
Siku hizi hamna waoaji mdogoangu. Wala usihangaike na chochote kwamba kuna kijana atatokea kukuoa. Utasumbuka sana kisaikorojia ukifikiria hivyo. Bahati mbaya wasichana wengi wanaanza kujisikia vibaya kuanzia huo umri kujiuliza kwa nini haolewi? Na hicho ulichosema unaonekana na wazee tu,sio kweli,vijana nao wanakuona ila wanakuogopa kufuatana na hali yako kuwa labda ya uwezo wa juu. Lakini hata hivyo ukijichanganya na vijana wenzio kama wengine wanavyokushauri,utaishia kutongozwa na bodaboda sana,na ndio hao uliokataa posa zao. Suruhisho,anza kutafuta namna yoyote ya kujiimarisha wewe mwenyewe kimaisha yako,bila kumsubiri mwanaume. Jitahidi kutengeneza future yako iwe nzuri bila kusubiri mwanaume. Baadae ukiwa na maisha yako,uwezo wako,kwa hiari yako utapanga tu nani akuzalishe,hata watoto wawili au vile upendavyo. Lakini hakikisha hao watoto unawamudu wewe kama wewe,usimtegemee mtu. Hapo ukisahau kbs wazo la kuolewa inaweza kutokea mwanaume unamkubali akakuoa. Asipotokea endelea na mishe zako. Hiyo unayopitia wewe wasichana wengi wanapitia mwisho wa siku anajikuta amejitupa kwa lijitu tu ili mradi aolewe,na ndio maana ndoa nyingi ziko tabani. Nakushauri ondoa kabisa wazo la kuolewa,ishi maisha yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu ndoa ni bahati nasibu ni kama umechukua chocolate kwenye kopo
Hao uliowakataa wako jela leo wote au wana maisha yao?
Ndoa zipo za kila aina zilizodumu na zilizovunjika kwa hiyo wewe pia sio malaika una mapungufu yako
Utasubiri sana kama unachagua mwanaume
Kwa ushauri wangu kwako akija mwingine kwenu na kuomba akuoe ulizia tabia zake
Na sio eti hujampenda tu ukafikia uamuzi wa kukataa
Wana ndoa wengi wamependana kabla ya kuoana na wapo pamoja na wengine wameachana kwa ubaya
Wengine wamecheat wengine baada ya ndoa tu mmoja akafa
Sasa kama unaiona future ya mtu subiri

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Wa hivi mkishajua kujichanganya kwenye ule mchezo, mwenzako anataka kutulia na mke mwema, wewe ndo kwanza unaanza ile michezo alioachana nayo.

Ngumu sana kuvumiliana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom