Sipati picha Mawaziri wa Kikwete wanavyojisikia

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Habari wanabodi,

Kiukweli siku 100 za Magufuli madarakani nadhani ni za kumtoa jasho sana,anafanya kazi ngumu sana huyu jamaa.

Ila huwa najiuliza hivi hawa ambao walikuwa ni mawaziri wa Kikwete wanajisikiaje?

Mfano wizara kama elimu,uchukuzi,mambo ya nje,ajira na kazi,vijana na habari,afya ambako yametumbuliwa majipu ya kutosha sijajua wanajisikiaje!!

Hata Rais mstaafu Kikwete,Waziri mkuu mstaafu Pinda na Lowassa sijajua wanajisikiaje pale wenzao wanavotumbua majipu ambayo waliyashindwa wao.Hakika wanajisikia vibaya sana kwamba waliyalea majipu hadi yakakomaa sana.

Japokuwa sijajua maana ya utumbuaji wa majipu hayo kutokana na kwamba hayafirisiwi.
 
Wengi wa mawaziri wa JK si hao hao wa JPM mkuu. We sema wengine wamebadilishiwa wizara
 
Wanajisikia kama Nyerere alivyofanywa na Mwinyi! Maana ilikuwa ni Mwinyi aliyelitumbua Azimio la Arusha na Siasa ya kijinga ya ujamaa na kujitegemea, akawafungulia wawekezaji na mashirika ya fedha ya IMF na World Bank, tukaacha kujipanga foleni kwenye maduka ya vijiji kugombania sukari na sabuni! Miji ikapanuka na nchi ikafunguka, hata TV zikaanza
 
Magufuli alikuwa Waziri wa Kikwete pia,Samia nae alikuwa Waziri wa Kikwete,Hata Majaliwa nae pia alikuwa Naibu waziri wa Jk
 
Hawajisikii chochote kama ambavyo wale waliopo JF walivyokuwa wakimlamba JK na sasa hawaoni aibu tena kumsifu anaye mponda yule.
Hapa ule msemo kuwa ili uwe mfuasi wa chama fulani lazima uwe na akili za maiti
 
Wanajisikia kama Nyerere alivyofanywa na Mwinyi! Maana ilikuwa ni Mwinyi aliyelitumbua Azimio la Arusha na Siasa ya kijinga ya ujamaa na kujitegemea, akawafungulia wawekezaji na mashirika ya fedha ya IMF na World Bank, tukaacha kujipanga foleni kwenye maduka ya vijiji kugombania sukari na sabuni! Miji ikapanuka na nchi ikafunguka, hata TV zikaanza
Kwa nini usimalizie kuwa sasa hivi kuwa walalahai wachache na walalahoi ni wengi kuliko wakati wa Nyerere!
 
Habari wanabodi,

Kiukweli siku 100 za Magufuli madarakani nadhani ni za kumtoa jasho sana,anafanya kazi ngumu sana huyu jamaa.

Ila huwa najiuliza hivi hawa ambao walikuwa ni mawaziri wa Kikwete wanajisikiaje?

Mfano wizara kama elimu,uchukuzi,mambo ya nje,ajira na kazi,vijana na habari,afya ambako yametumbuliwa majipu ya kutosha sijajua wanajisikiaje!!

Hata Rais mstaafu Kikwete,Waziri mkuu mstaafu Pinda na Lowassa sijajua wanajisikiaje pale wenzao wanavotumbua majipu ambayo waliyashindwa wao.Hakika wanajisikia vibaya sana kwamba waliyalea majipu hadi yakakomaa sana.

Japokuwa sijajua maana ya utumbuaji wa majipu hayo kutokana na kwamba hayafirisiwi.
Kifilisi ni baada ya kesi kuthibitishwa mahakamani na hiyo ni baada ya uchunguzi kukamilka mhusika kufikishwa mahakamani na kutiwa hatiani.
 
Ni aibu sana kwao! Mda wote huo walikuwa wanafanya nini hadi rais mpya aje kuibua vituko vyote hivi?
 
Habari wanabodi,

Kiukweli siku 100 za Magufuli madarakani nadhani ni za kumtoa jasho sana,anafanya kazi ngumu sana huyu jamaa.

Ila huwa najiuliza hivi hawa ambao walikuwa ni mawaziri wa Kikwete wanajisikiaje?

Mfano wizara kama elimu,uchukuzi,mambo ya nje,ajira na kazi,vijana na habari,afya ambako yametumbuliwa majipu ya kutosha sijajua wanajisikiaje!!

Hata Rais mstaafu Kikwete,Waziri mkuu mstaafu Pinda na Lowassa sijajua wanajisikiaje pale wenzao wanavotumbua majipu ambayo waliyashindwa wao.Hakika wanajisikia vibaya sana kwamba waliyalea majipu hadi yakakomaa sana.

Japokuwa sijajua maana ya utumbuaji wa majipu hayo kutokana na kwamba hayafirisiwi.
Hawawezi kujisikia vibaya kwa lolote kwani almost ni wale wale tu! Mwakyembe alikuwa waziri wa uchukuzi na leo anatamba katika serikali ya awamu ya tano. Jenista Mhagama alikuwa naibu waziri wa elimu na ndiyo maana mawaziri wa JPM hawafanyi kazi kwa mwongozo bali kwa sifa na uoga!
 
Kinachowauma ni pale majipu na kansa zao zinapotumbuliwa. haiji akilini kwamba koki za mafuta zinanunuliwa kwa bei ya kupiga halafu hazifanyi kazi. shame on them.
 
Sijakuelewa hapa
Watendaji wengi wa serikali wanaangalia aliye pale juu kwa maana ya rais au waziri mkuu anaacti vipi! Kama ni uongoz legelege bas nao wanakuwa legelege.Mfano hata kwenye familia zetu wazaz wakiwa legelege watoto wanajiamulia kufanya wanavyojiskia.Mtoto mwingne anaweza aamke tangu asubuh ashindwe sebulen na rimoti tu, mwingne anaweza kwenda kwa rafiki zake kukaa na kulala hukohuko.
 
Hii ni sawa na kusema kipofu anajisikiaje wakati yeye ndio hivyo alivyo na hata hajui kama kuna watu wengine wanaona...
 
Habari wanabodi,

Kiukweli siku 100 za Magufuli madarakani nadhani ni za kumtoa jasho sana,anafanya kazi ngumu sana huyu jamaa.

Ila huwa najiuliza hivi hawa ambao walikuwa ni mawaziri wa Kikwete wanajisikiaje?

Mfano wizara kama elimu,uchukuzi,mambo ya nje,ajira na kazi,vijana na habari,afya ambako yametumbuliwa majipu ya kutosha sijajua wanajisikiaje!!

Hata Rais mstaafu Kikwete,Waziri mkuu mstaafu Pinda na Lowassa sijajua wanajisikiaje pale wenzao wanavotumbua majipu ambayo waliyashindwa wao.Hakika wanajisikia vibaya sana kwamba waliyalea majipu hadi yakakomaa sana.

Japokuwa sijajua maana ya utumbuaji wa majipu hayo kutokana na kwamba hayafirisiwi.

Ishu ni kuyabinya hayo majipu na kutoa kiini. Kutumbua ni rahisi sana.
 
Back
Top Bottom