Sioni maridhiano bila mediator kwenye mazungumzo kati ya CCM na CHADEMA

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Salaam alaikum Wana JF!
Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu nasikitika kusema kwamba kwa mwenendo wa kinachoitwa mazungumzo au maelewano kati ya pande hizo mbili CCM na CHADEMA; bila mpatanishi (mediator) sioni matokeo chanya na katika muda muafaka au muda mfupi ujao.
Iko hivi:

1. Kinachoendelea sasa ni sawa na mechi ya mpira kati ya Simba na Yanga bila refa!
Hivi kweli tutegemee fair play katika mechi kama hiyo?

2. Hiyo mechi inachezwa kwa siri au gizani bila watazamaji ambao ni wananchi. Je, tutaonaje bao la halali au la mkono? Au nani mchezaji halali au kacheza rafu?

3. Huku nje mashabiki wa pande husika wanaendelea kuzodoana kwa maneno ya chini chini na/au waziwazi kama ilivyo ktk mitandao ya jamii na vyombo vya habari nk.

4. Washiriki wa mazungumzo upande wa Serikali wana msemaji mkuu mmoja ambaye ni Mkuu wa Serikali na Mwanyekiti wa CCM, ambapo upande wa pili kuna F A Mbowe wa CHADEMA na Zitto wa ACT Wazalendo ambao inaonekana hawashirikiani! Na hapo hapo ZZK yuko beneti na Ikulu!
Na hili ni chanzo cha tatizo na udhaifu wa upande huu wa mazungumzo. Sijui nao wanahitaji mpatanishi kuwaunganisha au lah! Lakini hii inafanya mwelekeo wa mazungumzo kutoeleweka. Kwasababu wananchi hawajui nini kinaendelea kati ya Serikali na Mbowe au Serikali na Zitto!

5. Kadiri muda unavyoenda momentum ya mazungumzo inapoa na hatujui kazi itaisha lini. Lakini tungekuwa na mediator tungesikia toka kwake kama kuna vikwazo gani vinakwamisha maelewano.

6. Sijui kwanini mediator hatjashirikishwa ili awe kama refa kwasababu ndiyo njia pekee ya kufanikisha maelewano kama nia ipo. Mbona J. Kikwete alikuwa mediator kule Kenya na W. Mkapa alikuwa mediator kule Burundi?
Kwahiyo nauliza: Bila ya mpatanishi mediator kuna uwezekano wa pande husika kufikia muafaka?
 
Back
Top Bottom