'Mazungumzo yaendelee wakati Kitita cha zamani kikitumika, kuna athari za kuendelea na Kitita kipya bila marekebisho'

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kufuatia Kitita kipya kilichotangazwa na Serikali kuanza kutumika kuanzia Machi 1, 2024, baadhi ya Asasi za Kiraia zimedai kuwa endapo kitita hicho kinaendelea bila kufanyiwa marekebisho athari mbalimbali zinaweza kujitokeza ikiwemo huduma duni za afya kwa wananchi.

Baadhi ya athari zilizotajwa na wadau hao ni pamoja na Watu kupoteza maisha kwa kukosa huduma, usumbufu kwa wagonjwa na wanaohudumia katika kutafuta huduma, vituo vya umma kuelemewa wataokosa huduma kwenye vituo binafsi, Maelfu ya watu kupoteza ajira. Ikidaiwa kuwa hali hiyo inaweza kutokana na vituo binafsi kulazimika kupunguza wafanyakazi ili kuendana na bei mpya za kitita cha NHIF kwa sababu sehemu kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa ni wanufaika wa NHIF.

Athari nyingine ambazo zimebainishwa ni kuwa huduma nyingi zitatolewa chini ya kiwango ili kupunguza gharama za uendeshaji, kufungwa kwa vituo vingi vya kutolea huduma, ambapo wamedai kuwa wamiliki wa vituo hivyo wanaweza kubadilisha biashara ili kuepusha migogoro na Serikali.

Asasi hizo ambazo ni Jukwaa la Katiba (JUKATA), Umoja wa Kizazi cha Kuhoji (UTG), GH Foundation wameshauri Serikali kusitisha matumizi kitita kipya cha huduma ya NHIF, badala yake kitita cha zamani kiendelee kutumika wakati mazungumzo ya kutafuta suluhu yakiendelea, ambapo wameweka wazi msimamo wakuwa hawaungi mkono kauli ya Serikali kwamba mazungumzo yaendelee wakati kitita kipya kikitumika wakidai kuwa kufanya hivyo ni kuumiza mwananchi.

Akisoma tamko la pamoja lililogusia masuala mbalimbli kuhusu sakata la kitita jipya, Godlisten Malisa ambaye ni Mwenyekiti wa UTJ akiambatana na Mwenyekiti wa JUKATA, Bob Wangwe, Noel Shao Katibu wa UTJ, Wakili Dickson Matata ambaye ni Mjumbe wa UTJ na James Mbowe GH Foundation, amesema kuwa baadhi kutokana na ripoti mbalimbali kuonesha uwepo wa matumizi mabaya na kinyume ya fedha za wanachama wa NHIF, wanaikumbusha Serikali kuelewa kwamba pesa zilizopo NHIF sio zake.

"Serikali ielewe kwamba fedha zilizopo NHIF sio zake bali ni za wanachama wanaochangia kwa kukatwa mishahara yao ya kila Mwezi au kwa kulipa kila mwaka. Hivyo basi matumizi yoyote ya fedha tofauti na yaliyoelekezwa kwenye Sheria yanapaswa kupata ridhaa ya wanachama." amesema Malisa wakati akisoma tamko hilo leo Machi 4, 2023

Ambapo kati ya fedha za NHIF ambazo wamezitaja kuhusishwa na Serikali kinyume na utaratibu rasmi wa kisheria, wamesema kuwa Serikali imekuwa ikitoa huduma bure kwa Wazee bila kufidia gharama.

"Sera ya Wazee kutibiwa bure inafaa kuundiwa utaratibu mzuri wa utekelezaji. NHIF imekuwa ikilipia gharama za matibabu ya Wazee bila Serikali kurudisha kiasi hicho cha fedha kwenye mfuko."wadau hao wameeleza

Sanjali na hilo wamedai kuwa ndani ya NHIF kumekuwepo na matumizi mabaya ya fedha za wanachama hali ambayo inaadhiri utoaji wa huduma kwa wanachama hivyo wameshauri hatua mbalimbali zichukuliwe kuepuka changamoto hizo, ambapo wametolea mfano kuwa ripoti ya CAG ilibaini vitendo vya udanganyifu ambapo kiasi cha TSH Bilioni 14 kinadaiwa kililipwa kwenye vituo vya kutolea huduma kama malipo hewa.

"Watumishi 146 wa NHIF na 129 wa vituo vya kutolea huduma walituhumiwa kwenye malipo hayo hewa. Hata hivyo watumishi 17 tu walichukuliwa hatua " Tamko limeeleza

Lakini pia wakiinukuu ripoti hiyo ya mwaka 2022 wamesema kuwa kulikuwepo na fedha za NHIF ambazo zilitumika tofauti na makusudio. Ambapo ripoti hiyo wamedai inaonesha kuwa wafanyakazi wa NHIFwamekopeshana zaidi ya Bilioni 41.42 ambazo ni michango ya wanachama na kuwa kiasi hicho hakikuwa kimerudishwa mpaka wakati CAG anafanya ukaguzi.

Wametolea mfano mwingine kwa kusema "Vilevile kumekuwepo na matumizi mabaya ya fedha yasiyo na mipango wala utaratibu mzuri. Kwa mfano NHIF ilinunua jengo la NIC Morogoro lililopo jirani na shule ya msingi Mwele, zaidi ya miaka 10 iliyopita kwa ajili ya kitega uchumi lakini hadi leo hawajaliendeleza."

Mfano mwingine ambao wameutoa kama hoja ambayo imekuwa ikipelekea changamoto za kifedha katika huduma ni kuhatamisha huduma za afya kwa watumishi wote wa umma.

"Baadhi ya taasisi za Serikali ziliruhusiwa kuwa na bima kwenye makampuni binafsi, lakini mwaka 2018 Serikali ililazimisha watumishi wote wa umma kutumia NHIF. Hii inafanya mfuko kuelemewa kwa sabubu wengi walipohamia NHIF ilibidi watengenezewe vifurushi vyao vya 'VIP' ili kuendana na huduma za kule walikotoka. Matokeo yake NHIFikawa na mizigo mkubwa uliowashinda kubeba" amesema Malisa akisoma tamko hilo.

Hata hivyo kufuatia hoja hizo pamoja na nyingine wameeleza kuwa Ripoti ya CAG 2023 inaonesha kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakabiliwa na hali mbaya ya kifedha na kuwa ukwasi wake umepungua, hali inayotishia upatikanaji wa huduma kwa wanachama wake.

Aidha kufuatia hayo yote pamoja sakata la Kitita kipya wameshauri Mamlaka kuvunja Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NHIF na kusukwa upya kutokana na walichodai kuwa ni kushindwa kusimamia vizuri mfuko huo.
View attachment 2923429
IMG-20240303-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom