Sioni mantiki ya watumishi kuwa na TIN, wakati wana NIN na Cheque Number

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,312
Ujue kuna mambo yanashangaza, wakati dunia inaelekea kwenye centralization of works through digitalization, sisi tunazidi kufanya decentralization ya kazi zetu.

Kuna haja gani mtumishi wa umma kuwa na TIN wakati huohuo anayo National Identification Number (NIN) na Cheque Number ya mshahara ambazo zinaweza kutumika kwa kazi hiyohiyo? Nchi nyingi kwa sasa watumishi wake wanatumia Namba moja tuu kwenye michakato yoote ya kiserikali.

Mfano Marekani ukiwa na Social Security Number (SSN) inatumika kama TIN. UK ukiwa na National Insurance Number (NINO), au Unique Taxpayer Reference (UTR) inatumika kama TIN. Hong Kong, ukiwa na Hong Kong Identity Card (HKID) inatumika kama TIN. Pakistan, ukiwa na Computerised National Identity Card (CNIC) unaitumia kama TIN.

TIN ni namba maalumu ambayo inakutambulisha kama mlipa kodi. Mtumishi anaweza kutumia NIN ama Cheque Number yake kama TIN na kusiwe na shida yoyote. Hamna haja ya kupewa namba nyingine special kwa ajili utambulisho wa mlipa kodi.

Kwa kifupi NIN zilitakiwa zitumike kama TIN kwa watu wote hata wafanyabiashara binafsi(sio makampuni) kwa maana kila mtu ana NIN ambayo ni unique kwake tuu. Sasa kwa nini uanze kutengeneza TIN mpya wakati NIN zinaweza kutumika kwa kazi/lengo hilohilo na kukuwezesha kuokoa muda?

TRA kaeni chini mtafakari upya huu utaratibu wenu, unawaongezea mzigo badala ya kupunguza.
 
Mkuu, sidhani kama tatizo ni TRA. Kwa maoni yangu nadhani tulipaswa kuwa na National ICT policy (sina hakika kama ipo) ambayo inge address haya yote.

Kwa hali ilivyo sasa, ukiachilia mbali taasisi za serikali hata taasisi binafsi zinakuwa very limited ku-automate operations zao kwa kuwa at some points utahitaji ku-interact na govt organs ambazo haziko automated.

Binafsi nashangaa mfano, serikali inajenga majengo makubwa na ya kisasa ya ofisi za uhamiaji then Passport inaprintiwa makao makuu. Unajiuliza kwa nini hizo gharama za majengo wasinge deploy IT infrastructures kuwezesha uharaka na ubora wa huduma?

Na hii ipo almost taasisi zote za serikali, eti zama hizi unaambiwa "subiri hadi itumwe makao makuu labda uje kuangalia after two weeks", kweli?! Unajiuliza hawa vijana tunao wakopesha wasome IT sijui watatumia wapi taaluma zao.
 
Tuna safari ndefu sana mkuu.
 
Hata kwenye private sector tuliambiwa bila TIN # hupati mshahara wa October. Nina wasiwasi sana, isije kua tunaanza kulipa kodi nyingine. Kila mwenye ajira.
 
Back
Top Bottom