Sioni Mantiki Bajeti Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sioni Mantiki Bajeti Bungeni

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by zomba, Jul 13, 2011.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sioni mantiki ya kusomwa bajeti za wizara zote bungeni? kwani hakuna bajeti inayoweza kuzuiliwa hata kama haikubaliki.

  Kwanza, kwa kuwa wabunge wa chama tawala hawapingi chochote kinacholetwa bungeni na serikali hata kama hakiwaingii akilini.

  Pili, kwa kuwa wabunge wa upinzani ni wachache hata manapozuia shillingi, huzidiwa na wabunge wa chama tawala.

  Nadhani ingekuwa vyema ili kuokoa muda na gharama, pale inapopitishwa bajeti ya jumla ya wizara ya fedha, pangeishia hapo hapo na bunge lingetiki kuongelea mambo mengine yeneye maana. Hili la kusoma bajeti za wizara zote ni kudanganyana tu na kutumia fedha zetu (walipa kodi) bila huruma.
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  hivi kuzuia shilingi ndio nini?nafikiri ni mchezo wa kuigiza
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Maana nzima ya budget imepotea. Wengi wanafikiri kupitisha bajeti ni kama kutunga uzi mkubwa kwenye jicho dogo la sindano, wengine wanafikiri kupitisha budget ni kama kupata mapokeo ya kidini, wengine kupitisha budget ni kama ushabiki wa mpira.

  Mi nadhani budget tunazipanga hata majumbani mwetu kila mara. Tunachofanya ni kupanga malengo ya kufanya kisha kuwasilisha kwa wengine ili tupate maoni mbadala, usaidizi wa fedha, kuboresha hata kutambua mapungufu.
  Haina maana hoja ya msingi kushindwa kuungwa mkono eti tu kwa vile si ya kwetu hata kama inatupa maslahi sisi binafsi.
  Unategemea nini kama watu wanaanza kupiga meza hata hoja haijatolewa mawazo.
  Wizi mtupu! Tena wendawazimu
   
 4. t

  tumpale JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wakati mwingine tunawaonea bure, unategemea nini kutoka kwa mbunge aliyekuwa mganga wa kienyeji awali, anachojua yeye ni kuunga mkono kila jambo la serikali. nakubaliana na hoja ya kuacha kujadili bajeti ili kuokoa fedha na muda maana hakuna la maana linalofanyika. juzi tu wabunge wa upinzani walisema bajeti hii ni kiini macho itamuumiza mtanzania wakazomewa, ccm wakapitisha kwa mbwembwe na kumpongeza mkullo pamoja na vibaraka akina mrema. leo wote hali tunaiona mafuta ya taa hayashikiki, petrol na dizeli zinaendelea kupaa. upumbavu mtupu.
   
 5. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  For a parliament to be an effective legislating body and a public watchdog, there needs to be a genuinely constructive split of opinion. Unfortunately with the current setup, party allegiances take precedence over professional integrity. There is too much voting along party lines and with a marginal opposition (accounting for less than the required majority to block a bill) the best that can be done is political filibustering (time wasting). Kosa sio la bunge, hili ni kosa la sisi wapiga kura la kuwapa an overwhelming majority chama kimoja cha kidikteta chenye wabunge wanaokataa au kushindwa kuwa waadilifu kwa sababu moja au nyingine.
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli jamaa kaja na hoja,

  Inatia kichefuchefu kuona bajeti zinavyopitishwa kibabe. Tatizo wabunge wa ccm ambao ni wengi wamebadirika na kuwa wakala wa serikali badala ya kuisimamia serikali.

  Mawaziri wamekuwa na kibri kujibu hoja za wabunge (nina maana wa upinzani) wakijua hata asiporidhika hana cha kufanya maana mwisho wa siku zitapigwa kura. Inapofikia hatua hiyo wapo kina Vicky Kamata wa kusema Ndiyooooo!! na mchezo unaishia hapo kama maigizo vile.

  Lakini waelewe 2015 siyo mbali, na maamuzi yao naamini yanawagusa ndugu zao walioko vijijini. Ni aibu taifa lina miaka 50 hatuna hata madawa kwenye hospitali zetu.

  Tuliambiwa juzi kwamba kuna madawa ya thamani ya mabilioni yameharibika/yame expire yakiwa bohari ya msd huku watu wanapoteza maisha kwa magonjwa yanayotibika, ni aibu sana. Leo wabunge wa ccm mnapitisha budget kwa mbwembwe kwa sauti za ndiyooooooooooo.

  Halafu huwa najiuliza spika/mwenyekiti huwa wana mechanism gani masikioni mwao zinazotofautisha sauti: Eti utasikia: waliosema ndiyo wameshinda. Mambo ya kizamani sana.

  Nadhani itafutwe technology itakayomwezesha mbunge kupiga kura ya siri ili kureflect hali halisi. Hatuwezi kuendekeza haya mambo ya ndiyooo.
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kama hakuna "follow up" ya utekelezaji wa mambo yaliyopo kwenye "Hansard". Nasema hivi kwa kuwa michango ya wabunge inaandikwa kwenye "Hansard" na majibu ya waziri husika nayo huandikwa kwenye "Hansard". Naamini serikali ina utaratibu wa kufuatia utekelezaji wa ahadi zilizopo kwenye "Hansard". Kama hakuna utaratibu wa kufuatilia then hakuna haja kabisa ya kuwepo Bunge.
   
Loading...