Sioni Gen Z Wakifanikiwa

Sioni Gen Z Wakifanikiwa

wakati huu serikali inabidi ijenge mahusiano mazuri na nchi jirani, kama ikatokea nchi jirani ikawapa silaha gen z, hii nchi patachimbika vibaya saaana, yani huo mziki wake polisi hawauwezi
 
My people,

Haya ni maoni yangu binafsi na si lazima yafanane na wengi wenu,na kutofautiana na wengi wenu nisionekane napinga harakati za kuikomboa Tanganyika

Kuna msemo mmoja wa kiingereza unasema ukitaka kumuua mbwa basi mpe jina baya,maana yake ni kwamba kwa kawaida au akili ya kawaida huwezi kumuua mbwa bila sababu na hasa kwa jamii ambayo wanapenda wanyama wa kufuga.

Ili umuue na kuepuka maswali mengi basi mapema sana unampa jina baya,na Watawala nao wametumia mfano huo huo kuwapa Gez Z jina baya ili wahalalishe kudili nao bila kuwa na tashuwishu nyingi.

Ndio maana umesikia wameitwa wahuni au wezi wa kuiba mali za watu na kuharibu miundo mbinu kama ambavyo tumeyaona yaliyotokea tarehe 29/10/25

Kwahiyo hawa Gen Z ambao wanapanga tena kuandamana tar 9/12/25 siku ya uhuru hawatakuwa na sifa nyingine yoyote ile isipokuwa ni ile ile ya kuitwa WAHUNI NA VIBAKA

Hapo utatumika msemo ule ule ukitaka kumuua mbwa basi muite jina baya,hapo kuna vijana wengine tena watauwawa,tena safari hii kwa kutaka kuiangusha Mamlaka au Serikalli

Msione hii tume ya Maridhiano imeundwa haraka,watapitia humo humo kwamba Serikali ina nia thabiti ya kuleta suluhu lakini wahuni wachache wanakwamisha hizi juhudi na kuleta machafuko hapa nchini,kwahiyo hawatavumiliwa na watashughulikiwa

Vile vile Serikali imeahidi kwamba ndani ya siku 100 italeta au kuanza mchakato wa kupata katiba yenye kuridhiwa na wananchi,hiyo ni fimbo nyingine ya kuwachapia Gen Z ambao sasa wanajulikana kama wahuni wachache.

Kwahiyo ukiangalia kwa mapana yake ni kwamba Serikali imechukua hatua kadhaa ili kuleta kinachoitwa maridhiano lakini kwa upande wa pili lawama zitakuja kwa GEN Z kwamba ni wahuni wachache ambao wanataka kuharibu amani ya nchi,hapo watashughulikiwa,je watashughulikiwa kwa kutumia nguvu kama ya awali? Hakuna anayejua muda utaongea.

Pili sioni uungwaji mkubwa wa watu katika kufanikisha hayo maandamano,watu wameumizwa na yale yaliyo tokea 29 october,wamepoteza wapendwa wao na sidhani kama watakuwa tayar kupoteza wengine tena.

Tatu ile athari ambayo jamii iliipata kama matokeo ya kuzuiwa majumbani na kuacha shughuli zao ili waathiri watu wengi sana,sioni hamasa ya watu kuingia kwenye mazingira yale tena

Nataka kusema nini hapa,maana yake ni kikundi kidogo tu cha watu wataingia barabarani na kukosa uhalali au sapoti ya watu wengi hivyo kukosa ile nguvu ya maandamano ambayo ingetakiwa itikise watawala na hatimaye nguvu ya umma ipate kuonekana

My take, ni ngumu sana kuuondoa utawala kwa maandamano ambayo hayana kiongozi,kwahiyo wote tunataka mabadiliko lakini sioni kuleta mabadiliko kwa stahili hii,sana sana italeta maafa na vijana wengi kupoteza uhai

Naamini kabisa kilichofanyika tar 29 October kimeiamsha dunia na kujua nini kinaendelea hapa Tanzania,ubaya umeonekana na sauti zimesikika,naamini hili halita pita hivi hivi ila litakuwa na athari chanya siku chache zijazo

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
Kabla ya tarehe 29/10/2025, mwenzako mwingine huyu hapa👇🏻👇🏻👇🏻 alikuwa haamini kuwa Watanzania wanaweza kutoka kuandamana kupinga uchaguzi mkuu wa mchongo

View: https://youtu.be/1g2BvzdbS80?si=XIYajgygIH2S8yas
Nadhani huko aliko, amejidharau na kujiona kuwa ni bwege namba moja mtaani kwake

Na wewe jiandae kuitwa bwege kwa kuwa huamini ila unataka kuona kwa macho, na kwa hakika utaona kwa macho yako❗❗

Jiandae kuona yote, na jiandae kushuhudia ajuza wenu Chura Kiziwi a.k.a Iddi Amin Samia akichomolewa toka ikulu yetu kama kibaka wa kike.

We don't care watatuitaje majina gani.

Kama ni majina ya laana, basi hiyo laana tunairudisha kwenye vichwa vyao na vya watoto wao!!
 
acuvim.jpg
 
Aisee nmecheka sana ila pole sana! Ni kama Samuel Doe na Charles tylor
Yani saizi ukileta hoja isiyofungamana na upande ww mboga mboga😅😅! Itokee leo chama kingine kishike hatamu amin amin nakwambia mboga mboga watakutana na genocide.... ndo mana wazungu wanakwambia

He who fights with monsters should be careful lest he thereby become a monster. And if thou gaze long into an abyss, the abyss will also gaze into thee"​

the methods used to fight evil can corrupt the fighter, making them indistinguishable from the evil they oppose.
Mkuu lazima tukubaliane kwamba si kila mtu anatakiwa kuwa Mbogamboga na si kila mtu lazima awe kule Simba.
Kuwa Simba au Yanga isiwe sababu ya chuki iletayo mauaji.
Ni kwanini waandamanaji wanaamini wao Wana haki zaidi juu ya mawazo na itikadi za wengine ?
 
Kabla ya tarehe 29/10/2025, mwenzako mwingine huyu hapa👇🏻👇🏻👇🏻 alikuwa haamini kuwa Watanzania wanaweza kutoka kuandamana kupinga uchaguzi mkuu wa mchongo

View: https://youtu.be/1g2BvzdbS80?si=XIYajgygIH2S8yas
Nadhani huko aliko, amejidharau na kujiona kuwa ni bwege namba moja mtaani kwake

Na wewe jiandae kuitwa bwege kwa kuwa huamini ila unataka kuona kwa macho, na kwa hakika utaona kwa macho yako❗❗

Jiandae kuona yote, na jiandae kushuhudia ajuza wenu Chura Kiziwi a.k.a Iddi Amin Samia akichomolewa toka ikulu yetu kama kibaka wa kike.

We don't care watatuitaje majina gani.

Kama ni majina ya laana, basi hiyo laana tunairudisha kwenye vichwa vyao na vya watoto wao!!

Mimi sipingi au sikatai kwamba hawataandamana ila sioni serikali kuangushwa kwa stahili hii

Muda utaongea
 
Kitendo tu cha kuwaita wahuni waliojiingiza madarakani kwamba ni serikali tayari huo ni ujinga.

Hatuna serikali bali genge la wezi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Hatuja mchagua rais wala muwakilishi yeyote, waliojiweka hawana uhalali kufanya lolote kwenye taifa hili.

Huwa siipendi hii lugha ya kuwaita waandamanaji wote ni GenZ, wewe ambaye sijui ni Gen X , Y or millenia hutaki mabadiriko ya mfumo mbovu uliopo, wewe una furahia utekwaji, upotezwaji na uuwaji unaofanywa na ccm na polisi wao?

waandamanaji siyo Gen Z pekee bali ni wananchi wanao kerwa na uovu unao fanywa na ccm kushirikiana na polisi wao.

Na kama wewe huto shiriki, mimi nitashiriki siogopi kuitwa, muhuni, kibaka, AI, mkenya, mgeni au jina baya.

Nutaandamana kuwaondoa ccm na vibaraka wao wote kwa njia yoyote lakini failure siyo option kwenye hili.
 
Back
Top Bottom