Sio vizuri walinzi wa benki kuhudumia wateja

Sio vizuri walinzi wa benki kuhudumia wateja

Hizi benki nadhani waweke mfumo mzuri wa customer care sio walinzi
 
  • Thanks
Reactions: lup
Mkuu kwenye ATM ndio kabisa , kuna mmoja pale hapo........... balaa, yeye utamsikia ''' oooo boss nakuona unakuja kuchukua mshiko aise sisi hapa vyuma vimekaza sana aiseeeeee''' sasa hapo ukiwa na tatizo kidogo labda na password au unafikiria amount ya kuchukua atafika na kukuswalika'' vipi kuna shida? bonyeza hapo, au hiyo machine haitoi risiti.... maswali kibao , mpaka unaondoka eneo hilo hujui kama password iko salama!!! wengine mizinga wanapiga fasta kabla hujaondoka eneo la tukio, kuna huyu mmoja nikimkuta huwa navunga na kuondoka kwenda sehemu nyingine
Wale suma wa atm ya crdb kariakoo sokoni pale ofisi ya posta wanagonga mizinga vibaya mno.. ukiingia tu anafungua mlango anachungulia anaanza kulia shida..
 
Labda anakuulizia ili akudirect uelekee wapi kulingana na shida yako,pia kiusalama ni nzuri pia kuhoji km majukumu ya kazi zake
 
Kastama keya ni zero. Yote wamewaachia maaskali.
 
Makampuni ya ulinzi hua yana mikataba tofauti..kwenye taasisi nyingi za kifedha (si zote) Makampuni husika yanakua nadhamana ya shughuli zote kuanzia wateja, parking magari nk..Kitendo cha mlinzi kukuuliza ni sehemu ya majukumu yake kwakua hata ikifika SAA kumi mlinzi wa zamu ndiye mwenye mamlaka ya kutoa greenlight mteja apate huduma ama vinginevyo..na hata branch manager hana sauti kwakua ni swala la kisheria zaidi..kwamba wewe umeingia bank una shangaa shangaa ghafla ufanye tukio..ni nyeye aliyekua lindoni ataoza jela na kampuni yake iliyo muajiri itakula hasara! tuache dharau..pesa ni zako ndiyo lakini kujishusha japo Mara moja si dhambi! hayuko mule ndani kwa bahati mbaya! na wewe uache uswahili hujaona kibao au sehemu ya Enquiries?
 
kila mtu yupo kwa nafasi yake all is about security issue. mtoa post inaonyesha unadharau kaz za watu
 
Za asubuhi hii.

Leo katika majukumu ya kila siku nililazimika kwenda bank moja hapa kwenye jengo maarufu jijini Mwanza. Nikafika benki moja nikawa nahitaji kuchukuwa pesa niliyotumiwa kutoka nje.

Wakati nataka kwenda kwa mhudumu wa wateja nikaulizwa na mlinzi wa ndani shida yangu ni nini. Ukweli sikupenda lile swali maana nilijua sio wajibu wake nikataka kwenda sehemu niliyotaka lakini alionesha kutaka kujua shida yangu kama vile ndio anaweza kutatua na kutolea majibu.

Nikaona isiwe shida nikamwambia hitaji langu cha kushangaza ni kama ni kitu kipya kwake na hajui chochote.

Hii tabia ipo kwenye mabenki mengi na ukweli huwa inakera wateja. Unakuta mlinzi amekomaa kuhoji wateja hadi anawajazia form
Sijaona shida iko wap ww kuulizwa...... mnawadharau sana hao walinzi sijui kwann aisee.....Heshimu kaz ya mwenzako kama unavyoiheshim yako
 
  • Thanks
Reactions: lup
Sijaona shida iko wap ww kuulizwa...... mnawadharau sana hao walinzi sijui kwann aisee.....Heshimu kaz ya mwenzako kama unavyoiheshim yako
Sijamdharam MTU yeyote ila kulingana na utaratibu wa Nazi na mgawanyo wa madaraka na vitengo..yeye yuko pale kuhakikisha usalama wa watu waliomo ndani,mfano kupanga mstari kuangalia MTU kama anadalili za wizi na vitu kama hivyo lakini sio kuuliza kila kitu ambacho mteja anahitaji kufanya
 
Kuna walinzi wa kanpuni moja ya simu huwa wanatusaidia hata kujaza form ya kurenew line. Ukimshikisha buku unakuwa mfalme, anakurusha hata kwenye foleni hukai, unakuwa VIP
 
  • Thanks
Reactions: lup
Nimepitia thread zako nimegundua tatzo ni dharau, na Kama ungejua majukumu ya mwanausalama usingepost huu ushuzi hapa, na hizi ni tabia za watu maskini na wenye vijisenti vyao vya laki3 bank wanadharau balaaa, Ni tofauti na matajiri hao Wana ustaarabu wanajua thamani ya kazi ya mtu....Tena huyu jamaa asingepaswa hata kujibiwa huwa nawachukiaga Sana watu wenye kujishaua Kama huyu jamaa kiss wameenda kuchukua vilaki3 bank

Back
Top Bottom