Mkuu kwenye ATM ndio kabisa , kuna mmoja pale hapo........... balaa, yeye utamsikia ''' oooo boss nakuona unakuja kuchukua mshiko aise sisi hapa vyuma vimekaza sana aiseeeeee''' sasa hapo ukiwa na tatizo kidogo labda na password au unafikiria amount ya kuchukua atafika na kukuswalika'' vipi kuna shida? bonyeza hapo, au hiyo machine haitoi risiti.... maswali kibao , mpaka unaondoka eneo hilo hujui kama password iko salama!!! wengine mizinga wanapiga fasta kabla hujaondoka eneo la tukio, kuna huyu mmoja nikimkuta huwa navunga na kuondoka kwenda sehemu nyingine