Sio mke mmoja tu, hata hao wanne hawatoshi pia

Sio mke mmoja tu, hata hao wanne hawatoshi pia

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
12,312
Reaction score
18,186
Kumekuwa na kauli ambayo inaegemezwa na uislamu ya kuwa mke mmoja hatoshi kwa hiyo bora wa nne.

Kwanza kauli hii sio sahihi ni kauli ya waislamu na sio kauli ya uislamu ni waislamu wanasema hivyo na waislamu wanasema Mengi tu sio hili peke yake.

Mwanaume hajawahi kutosheka na mwanamke kamwe hata Allah hili jambo analijua ndio maana akatuachia japo huo upenyo wa ruhusa japo wanne tupate.

Lakini kiuhalisia tukija kwenye tafsiri ya kutosha basi hao wanne hawatoshi kwa sababu kila siku wanazaliwa warembo wapya ambao utawaona wazuri zaidi ya mkeo na unatamani wangekuwa wake zako na hao, hii pia ni dalili kuwa mwanaume hatosheki na wanawake lazima atawatamani tu.

Tukirejea katika historia za hadithi za Mtume sala na salamu ziwe juu yake utakuwa kuna watu aliwasilimisha wakiwa na wake kumi.

Mwanaume mmoja wanawake kumi yaani alizidi hasa mpaka hao wanne, mtume akamuambia waache sita ubakia na wanne.

Laiti ingekuwa wanawake wanne ndo wanatosha basi pasingepatikana watu kama hawa hapo zamani wenye wanawake zaidi ya wanne.

Tumeruhusiwa kuwa na wake wanne sio kwa sababu ndo wanatosha hapana bali kwa sababu Dini imetaka tukomee hapo na sio vinginevyo.

Wewe fikiria mfano tu una wake saba
1. Sanchoka
2. Poshi kwini
3. Marehemu Mmasogange
4. Hamisa Mobeto
5. Beyonce
6. Vera Sidika
7. Rihanna.

Hivi kama wewe utatosheka na wanne tu au utabaki nao hao wote saba ?

Bila shaka utamiliki ngoma zote saba hapo na utaenda nazo vizuri tu.

Kuchoka kupo kama ambavyo mtu anachoka akiwa na mke wake mmoja.

Hivyo dhana ya kutisheka ni pana mno na wala dini haikusema tuoe kuanzia wawili ati kwa sababu mmoja hatoshi, hizi ni tafsiri zetu tu.

Kuna watu wana wake wanne bado wanatoka nje kuzini, kuna watu wana mke mmoja na wanatulia.

Hivyo kuzini ama kutozini ni state of mind kuamua kwa sababu hata kama huna mke dini haijakuruhusu uzini ati kwa kuwa huna mke bali dini imekutengenezea uwezo wa akili yako kuepuka zinaa.
 
Wake wanne ni sawa, ila sio kweli kwamba ni kwa kigezo wanaangukia kwenye aina zote za wanawake.

Kuna aina melfu za wanawake, hasa hii maarufu ya wenye mgongo.
 
wake wanne ni sawa, ila sio kweli kwamba ni kwa kigezo wanaangukia kwenye aina zote za wanawake.

kuna aina melfu za wanawake, hasa hii maarufu ya wenye mgongo.
Sahihi kabisa unaweza ukaoa wanne na bado ukawa hujamaliza aiina zote.

Mfano aina kama ya sanchoka ni tofauti na aina kama ya vera sidika.

Wawili hao tayari.

Aina kama ya rihana ni tofauti na aina kama ya Hamisa Mobeto, wawili wengine hao jumla wanne.

Sasa angalia umebakiza vyuma vingapi mzee ambavyo vinawazidi urembo hao tuliowataja.

Ukija uswahilini ndo kabisa unakutana na vyuma vyenye kila aina zaidi ya aina nne mkuu.
 
Sijakuelewa kaka. Ukomo wa wake wanne sio Takwa la uislam?
Ni takwa la uislamu.

Hoja ni kuwa sio kwamba tumeambiwa mwisho wa nne ati kwa sababu hao wanatosha no.

Kuna watu wanasema mke mmoja hatoshi ati ndio maana dini ikataka wanne,kwa hyo wanataka kuaminisha watu kuwa uislamu umeona mke mmoja hatoshi ndio maana ukataka iwe wanne.

Sasa uzi unakataa jambo hilo,mke mmoja anatosha na wanne wanatosha pia,mmoja hatoshi na wanne hawatoshi pia ikiwa utaamua.
 
Naomba kuelimishwa pia, vipi mwanamke anayevutiwa na wanaume sampuli tofauti, anaruhusiwa naye kufanya polyandry?
hizi ndio double standards ambazo tunapigia kelele hapa.

kimsingi swala la kuoa ni la kibinaadam zaidi sio la kimwili.
ndio sababu ili kuishi kwenye ndoa unatakiwa utumie utashi wa kibinaadam ndoa idumu.
 
Mjadala mzur na wenye kufikilika, kwa kawaida mwanaume anafikilia ngono mara nyingi zaid kwa siku huku mwanamke anafikilia mara 1 tu kwa siku, na mwanaume anaweza kungonoka na wanawake hata 10 kwa siku km akiusikiliza moyo wake kitu ambacho mwanamke awezi kuwa na hamu iyo labda awe na tamaa ya pesa tu, kiimani ya dini wanne wanatosha lkn kitamaa ya moyo awatoshi eeh!
 
Mungu atujalie mwisho mwema tuu inshallah,.yote haya ni ubatili.
Mkuu haya ni mambo ya kiimani zaidi.

Kuna mambo tunayaona lau tungewasimulia ambao hawajayaona wasingeliamini kabisa.
 
Emu weka picha za hao uliowataja kwanza kabla sijachangia chochote
 
Back
Top Bottom