Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Igweeeeeeeeee!!!
Natumaini mu wazima wanaJF wenzangu. Ikiwa ni tofauti na hivyo basi Mungu awafanyie wepesi katika changamoto mnazopitia.
Kumezuka tabia ya watu siku hizi kulazimisha mapenzi. Utakuta mtu anatumia nguvu kubwa kulazimisha mahusiano. Jambo ninalotaka kuleieleza hapa ni kuwa sio lazima awe wako.
Wanaume wapo wengi halikadhalika wanawake ndio usiseme. Kama hakutaki muache aende. Hukuumbiwa yeye wala hana ushahidi wowote kuwa iliandikwa sehemu yakuwa utakuwa wake.
Wapo watu huwatoka mapovu kila uchwao, Jasho linawatiriri kwa sababu ya mahaba. Machozi na makamasi mepesi hudondoka katika pua zao Kama watu waliorukwa na akili. Aliyekuambia ni lazima awe wako ni nani. Mambo mengine sio ya kuyaendekeza.
Mimi nilishashtuka mapema tokea nikiwa Sekondari.
Huwaga nawaambiaga kuwa Ahsante kwa kushiriki. Kama hajaridhishwa na tabia yangu namwambia wanaume wapo wengi halikadhalika wanawake hivyo kila mtu na apeperuke apendapo.
Nasemaga wazi wazi sijazaliwa kwaajili ya Mtu hapa duniani. Sipo kwaajili ya kumfurahisha yeyote wala kumkwaza yeyote. Ikiwa umependa pigo zangu basi kaa Kama hutaki pita kule. Sio unilitee upuuzi eti wa kunibadilisha tabia.
Kanuni hiyo imenisaidia Sana.
Hivyo ewe mwanaume/ Mwanamke usilazimishe mapenzi kwani sio lazima uwe awe wako.
Akizingua na wewe zingua tuu. Muda wa kuendekeza ujinga wa moyo ulishapitwa na wakati.
Jitu linakusumbua akili na wewe unalitolea macho tuu na kulichekea tuu. Tupa kule.
Kuna mambo mengi ya kufanya, wapo wengi wanaokusubiri ambao wataendana na wewe.
Achana na huyo mjinga ambaye anadhani upo kwaajili yake.
SIO LAZIMA AWE WAKO.
~kwa hisani ya kiumeni